Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Katika kusaidia kudhibiti Maambukizi ya virusi vya Corona, kukitokea any good practice, lets share ili na wengine waige.
Leo nimetembelea makao makuu ya kampuni ya mafuta ya Total, Total Tanzania, ukifika pale
Huu ni utaratibu mzuri sana, sijui ile mashine inauzwa kiasi gani, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu angetangaza public corporations zote zinazotembelewa na watu, zaidi ya kunawa mikono, zinunue mashine hizo na asubuhi wafanyakazi wote wapimwe, na wageni wote wapimwe, wapewe face mask bure na zinunue sterile cabinets barua zote ziwe sterilised kabla ya kupokelewa.
Najua it's a cumbersome procedure lakini kwa wenzetu wanaojali, it's worth to spend little on prevention than much on cure.
Hongera sana Total Tanzania kuonyesha mfano, nadhani kwa sababu hii ni kampuni ya kimataifa, vikampuni vyetu locals, let's learn mambo mazuri kwa wenzetu waliotutangulia, Corona inazuilika.
Paskali

- Hatua ya kwanza ni lazima unawe na maji moto tiririka hapo nje na sabuni, wamejenga kabisa sink la kunawia na liko permanent. Wewe hugusi chochote, ukiweka mkono sink lina sense maji tiririka ya moto yanatoka, ukiweka mkono kwenye sabuni sabuni nayo inatoka. System hii niliiona Kempinski na Serena. Ukimaliza unaingia kwenye blow drier kukausha mikono, na kumalizia kwa sanitizer.
- Hatua ya pili baada ya kunawa, unakutana na wahudumu wawili wa kike na kiume, wameshika mashine kama zile la traffic kupimia pombe madereva, unapimwa joto na mashine kwa kukupima maeneo mawili, kwenye paji la uso na kwenye mshipa mkubwa wa damu wa mkono huku umekunja ngumi. Kipimo cha joto la kichwa kisipotally na joto la mkono, safari yako kuingia Total inaishia hapo. Ukiwa fit, unaingia hatua ya tatu.
- Ukimaliza unapewa hand gloves unavaa, kisha unapewa face mask unavaa.
- Hatua ya nne ni kupewa escort, haushiki chochote, milango ni kufunguliwa ndipo unaingia ndani na kumsubiri mwenyeji wako kwenye chumba maalum sanitized. Unakaa kwenye kiti, mwenyeji wako akifika, anakaa umbali wa mita 1.5, kama umeleta barua yoyote au kitu chochote kinapokelewa na kupotishwa kwenye sterilisar tray ndio inapokelewa kama barua za ubalozi wa Marekani au UK!.
- Ukimaliza yule askari aliyekuleta anakusindikiza hadi pale nje, zile gloves na face mask ni zako, nje kuna dust bin ya kukanyaga inafunguka unavua na kutupa, au unaweza ku sepa nazo.