Vita dhidi maambukizi ya corona Tanzania, kampuni ya Total Tanzania mfano wa kuigwa!. Ukifika lazima unawe, upimwe na mashine ndipo uruhusiwe kuingia!

Vita dhidi maambukizi ya corona Tanzania, kampuni ya Total Tanzania mfano wa kuigwa!. Ukifika lazima unawe, upimwe na mashine ndipo uruhusiwe kuingia!

Kwangu kampuni ya mfano Tanzania ni Jamiiforums tu .
Walichofanya ni sahii kabisa kukabiliana na huu ugonjwa .Ili mradi hao wafanyakazi wao wajifungie kweli majumbani wasiwe wanadhurura mitaani kama hawa wanafunzi wetu shule zimefungwa ila wao kiguu na njia kutembeleana
Kimsingi Serikali inatakiwa kushutdown/ lockout nchi nzima kwa siku 14 au zaidi
Watu wasitoke nje.
Hao wafanyakazi wa total wanaweza pata maambukizi wakiwa kwenye public transport wakiwa wanatoka au wanarejea makazini .
Huu ugonjwa solution yake ni kuifunga nchi kwa siku 14 au zaidi. Tujiridhishe wagonjwa ni kina nani
Wafanyakazi wasio na ulazima wakae nyumbani bila mshahara.
Wafanyakazi muhimu kama majeshi na wahudumu wa afya ndio wafanye Kazi na kulipwa
Makampuni yasitozwe kodi, waliopanga nyumba wasitozwe kodi. Katika kipindi hicho
Serikali kupitia hifadhi ya chakula isambaze mahindi na maharage na mafuta.
Ifadhi yetu ya fedha itumike wananchi tuambiwe tufunge mkanda hakutakuwa na chips kuku wala ma humberg kutoka serikalini.
Wagonjwa wowote waliopo majumbani kwa sasa wahamishiwe mahospitalini Ile waweze kupata huduma ktk kipindi hiki

Baada ya siku 14 wagonjwa wote watakaokuwa wanaugua korona watakuwa wanajulikana na watengwe na wahudumiwe.
Bila ya hivyo hili gonjwa litatulipukia na tutaanza vilio na kusaga meno kama italy
You just save may words.
Kwangu Mimi solution ya huu ugonjwa ni kulockdown nchi nzima
 
"Total hata Sheli zao"you are mixing 2 different things ili paswa useme "Total hata vituo vyao au petrol station zao" ziko vizuri.Shell ni kampuni ya mafuta km Total ni sawa na kusema "Blue band ya Tan bond siku hizi ni nzuri" wakati zote ni margarine aka Siagi.
total hata sheli zao tu ni [emoji91] mzungu huyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha kaka Pascal Mayalla naomba nikuulize maswali yafuatayo.
Hicho kipima joto kina pima joto specific la Corona virus au joto tu ili mradi joto la mwili?

Pili, unaweza kunisaidia kuelewa, ni wakati gani mgonjwa wa hii Corona anapandwa joto , na ni baada ya muda gani mtu akiambukizwa joto linapanda na kwa kiasi gani?,

Ni kweli nimesikia wanaosambaza maambukizi ni wale walio na virusi lakini hawana dalili zozote za ugonjwa, ikiwa ndivyo , je ni baada ya muda gani mtu aliye ambukizwa ataanza kuonyesha dalili za ugonjwa? na hili joto linatofauti gani na joto la mgonjwa wa malaria?, Na ikiwa utapimwa hapo total petrol station,na kisomeo kikasoma joto ni kubwa, hawa wamejiandaa kukuhudumia au wana fanya kwa sababu waliona huko kwingine wanapima joto?

Hiki kipima joto unachokiomba kuna wananchi wengine wanadhani kinapima Corona virus kwenye mwili wa mtu aliyeambukizwa. Lakini ni kipima joto tu.

Wewe kama mwandishi wa habari, unge watafuta wataalam wenye taaluma hiyo ukawauliza maswali mazuri ukatuletea hapa jukwaani nasi tuelewe kupitia makala zako.

Kipima joto siyo sasa kitambuzi cha maambukizi ya Corona, kuna watu huonyesha dalili tofauti zaidi ya kuongezeka joto la mwili, hivyo binafsi sioni kwanini kila mtu sasa analilia kipima joto kila sehemu.

Kuna uzi mmoja niliona watu wanalalamika kwamba Rais na mawaziri wanapimwa wao Corona sisi wananchi hatuna pa kwenda. Lakini niliona picha humu Rais akipimwa joto kuingia kwenye ukumbi wa mkutano wa baraza la mawaziri.Pale hakuwa akipimwa Corona virus, bali joto la mwili. Kuna watu wamepimwa na kukutwa na virus wa corona lakini joto la mwili wao halikuwa juu, bali lilikuwa kawaida.

Nadhani kuna haja ya jamii kueleweshwa, siyo joto la mwili pekee linaweza kuwa indicator ya kuwa na virus vya Corona, ila ni moja ya vitu vilivyo kuwa vimefahamika mwanzo. Bali kuna dalili nyingine mgonjwa anaweza kuzionyesha na joto lisiwemo, na akawa positive.

Mkuu siyo nia yangu kutoa maelezo meengi bali nilitaka kukazia kwamba, vipima joto siyo lazima, bali elimu ya watu kunawa mikono, na kuepuka misongamano isiyo ya lazima yaani social distancing, pia kukohoa kwa kukinga kinywa, na kujitoa kwenye public kama huna hulazima wa kuwa huko, yaani self Quarantine.
 
Hongera Total napenda kujaza mafuta katika vituo vyao na hili itabidi niwaunge mkono kila wakati.
Mkuu Ngongo, kwa watu sensitive na mlio wa engine za magari yao, na kiwango cha uchomaji wa mafuta, wakijaza mafuta vituo vya Total wata notice the difference, gari inatulia, mlio safi, na unakwenda mwendo mrefu kwa mafuta kidogo sababu mafuta ya Total yameongezwa kiambata cha excellium.
Msikilize hata huyu jamaa


P
 
Wanabodi,
Katika kusaidia kudhibiti Maambukizi ya virusi vya Corona, kukitokea any good practice, lets share ili na wengine waige.

Leo nimetembelea makao makuu ya kampuni ya mafuta ya Total, Total Tanzania, ukifika pale
  1. Hatua ya kwanza ni lazima unawe na maji moto tiririka hapo nje na sabuni, wamejenga kabisa sink la kunawia na liko permanent. Wewe hugusi chochote, ukiweka mkono sink lina sense maji tiririka ya moto yanatoka, ukiweka mkono kwenye sabuni sabuni nayo inatoka. System hii niliiona Kempinski na Serena. Ukimaliza unaingia kwenye blow drier kukausha mikono, na kumalizia kwa sanitizer.
  2. Hatua ya pili baada ya kunawa, unakutana na wahudumu wawili wa kike na kiume, wameshika mashine kama zile la traffic kupimia pombe madereva, unapimwa joto na mashine kwa kukupima maeneo mawili, kwenye paji la uso na kwenye mshipa mkubwa wa damu wa mkono huku umekunja ngumi. Kipimo cha joto la kichwa kisipotally na joto la mkono, safari yako kuingia Total inaishia hapo. Ukiwa fit, unaingia hatua ya tatu.
  3. Ukimaliza unapewa hand gloves unavaa, kisha unapewa face mask unavaa.
  4. Hatua ya nne ni kupewa escort, haushiki chochote, milango ni kufunguliwa ndipo unaingia ndani na kumsubiri mwenyeji wako kwenye chumba maalum sanitized. Unakaa kwenye kiti, mwenyeji wako akifika, anakaa umbali wa mita 1.5, kama umeleta barua yoyote au kitu chochote kinapokelewa na kupotishwa kwenye sterilisar tray ndio inapokelewa kama barua za ubalozi wa Marekani au UK!.
  5. Ukimaliza yule askari aliyekuleta anakusindikiza hati pale nje, zile gloves na face mask ni zako, nje kuna dust bin ya kukanyaga inafunguka unavua na kutupa, au unaweza ku sepa nazo.
My Take
Huu ni utaratibu mzuri sana, sijui ile mashine inauzwa kiasi gani, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu angetangaza public corporations zote zinazotembelewa na watu, zaidi ya kunawa mikono, zinunue mashine hizo na asubuhi wafanyakazi wote wapimwe, na wageni wote wapimwe, wapewe face mask bure na zinunue sterile cabinets barua zote ziwe sterilised kabla ya kupokelewa.

Najua it's a cumbersome procedure lakini kwa wenzetu wanaojali, it's worth to spend little on prevention than much on cure.

Hongera sana Total Tanzania kuonyesha mfano, nadhani kwa sababu hii ni kampuni ya kimataifa, vikampuni vyetu locals, let's learn mambo mazuri kwa wenzetu waliotutangulia, Corona inazuilika.

Paskali
Wasukuma bana.Haya ngoja nitaweka kwangu
 
Fanyia kazi vichwa vyako vya habari. Ni virefu mno, yaani kichwa cha habari kinakuwa kama habari kamili.
Mkuu Abitali Mwerevu, hapo kwenye vichwa virefu ndipo power yangu ilipolalia, ukiisha soma tuu kichwa kinajisheleza kufikisha ujumbe kusudiwa na sio lazima usome bandiko. Kuweza kufikisha ujumbe mzito kwa sentensi chache, kiuandishi hii inaitwa sending "Power Messages" ukisoma tuu heading umemaliza ujumbe umekufikia.

Mtindo huu ni muhimu sana kwa busy world kuwafikishia watu ujumbe kamili, kisha wakipata muda ndio waje wasome.
P
 
Back
Top Bottom