Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Leo Waziri wa Afya ametangaza virusi hatari vya Corona kuwepo nchini mwetu. Mgonjwa mmoja amethibitishwa kwa vipimo vinavyofanywa kwenye maabara moja tu hapa nchini kwetu.

Maana yake kuna uwezekano wa kuwepo wengine wenye virusi hivyo ambao hawajabahatika kufanyiwa vipimo hivyo au ni carriers.

Cha ajabu, baada ya tangazo hilo, kiongozi wa chama kimoja kikubwa cha siasa katangaza kufanyika mikutano ha hadhara nchi nzima kila siku bila kikomo kuanzia wiki ijayo hadi Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Tusifanye mzaha na virusi hivi vya Corona. Na vikiendelea kuwepo hata Uchaguzi mkuu wa mwaka huu lazima tutauahirisha.

----
Serikali ipige marufuku machinga mjini


-----
Misongamano kwenye usafiri wa umma idhibitiwe

----
Maeneo ya kufunga na mambo ya kuzuia ili kuepusha coronavirus Dar es Salaam

 
Vyombo vya ulinzi na usalama vizuie mikutano ya CHADEMA tu.

Mikutano ya CCM iruhusiwe kipindi hiki ambako kuna hatari ya ugonjwa wa CORONA.
Tatizo lako Daktari umeshaingiza hapo hisia za kisiasa badala ya weledi wa kazi yako. Mh. Mbowe alikuwa tayari ameshajiandaa na mkutano wake siku ya leo, pasipo kuwa na habari yoyote ile kuhusu kauli ya serikali itakayokuja kutolewa leo na waziri mwenye dhamana. Sasa unaanzaje kutoa hukumu juu ya matukio hayo mawili yaliyokuwa hayana mfungamano wowote ule wa kitaarifa!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumba za ibada je mfano makanisa ya RC huwa kuna MAJI ya BARAKA unayagusa uingiapo Na utokapo Na Kwa waislamu Yale ya kutawadhia sijui itakuwaje hapa
 
Kwa nguvu kubwa ya tahadhari dhidi ya Corona nje na ndani ya nchi. Je, siyo wakati muafaka wa kutojaza kwenye mabasi hasa MWENDOKASI? Naona bado ni pomoni pomoni. Au sisi Tanzania tuna ka-immunity fulani?
 
Vyombo vya ulinzi na usalama vizuie mikutano ya CHADEMA tu.

Mikutano ya CCM iruhusiwe kipindi hiki ambako kuna hatari ya ugonjwa wa CORONA.
Vita dhidi ya corona haina chama wala dini wala ukabila. Kuna uwezekano hata ibada za siku kuu za Pasaka mwaka huu hazitakuwepo.

Huko Italy na Vatican, wananchi wote wako under house quaranteen (hawatoki nje ya nyumba zao) isipokuwa watoa huduma wa hospitalini tu na polisi. Sisi tunataka kufanya maandamano na mikutano ya hadhara isiyo na kikomo kila siku kama ile ya UKUTA ya 2017! Hata jumuiya za kimataifa zitatushangaa!
 
Mipango itaendelea tu labda mzuie mawasiliano. Kama univesities lectures zinaendelea on line seuse mawasiliano ya Mwamba na wanachama 😂
 
Dr Akili,
Hivi hujui kwamba viongozi wa CHADEMA na wanachama wao wana pumzi yenye virusi vya corona?

Na wanachama wa CCM pumzi zao ni safi na zinaweza kukukinga na corona?
 
Nyumba za ibada je mfano makanisa ya RC huwa kuna MAJI ya BARAKA unayagusa uingiapo Na utokapo Na Kwa waislamu Yale ya kutawadhia sijui itakuwaje hapa
Kwenye vita hii hayo maji hayaruhusiwi. Hata kuhudhuria ibada za kanisani na misikitini hairuhusiwi. Ni kubaki nyumbani tu.

Simu za mkononi ni petri dish za corona. Ukinawa mikono halafu unashika simu yako (ambayo hujainawisha na huwezi kuinawisha) work done inakuwa zero! Hivyo baki nyumbani kwako tu.
 
Hivi hujui kwamba viongozi wa cdm na wanachama wao wana pumzi yenye virusi vya corona?

Na wanachama wa CCM pumzi zao ni safi na zinaweza kukukinga na corona?
Acha mzaha. Corona ni kitu ingine.Ni baba lao. Wakina HIV ni cha mtoto. Corona tukiichezea basi itakuwa ndiyo mwisho wa dunia.
 
Miongoni mwa mambo ambayo yanatakiwa kufanywa kupunguza au kuweka tahadhari juu ya maambukizi ya corona virus ni

(1) Kuwekwe sheria ya kuzuia gari yoyote kusimamisha abiria kupunguza miingiliano ya mtu na mtu.

(2) Taasisi zote za elimu zifungwe mapema kabla janga halijawa kubwa hasa primary na secondary schools ambapo uelewa wao ni mdogo.

(3) Mkutano na mikusanyiko mbalimbali ifanywe kwa njia ya mitandao ikiwezekana kuzuia muingiliano wa mtu na mtu

(4) Sanitizer na mask ziingizwe bila kodi ili ziwe katika bei ya chini kabisa kwakuwa hili limekuwa janga la kitaifa zaidi ya nyanya.

Serikali yetu inabidi ifanye maamuzi ya haraka sana hizi habari za kuwaza mapato mtaishia kupoteza walipa kodi.

Ni muda wa kuiga wenzetu walioathirika zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…