Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kama unafuatilia vyombo vya habari,utaona ni kwa kiasi gani Mataifa mbalimbali yanavyofanya maamuzi magumu kukabiliana na ugonjwa huu yakiwemo hata Mataifa jirani kama Rwanda na Uganda.
Kwa mfano,Rwanda wameshatoa tangazo la kuzui ndege kuingia nchini mwao kuanzia kesho isipokuwa ndege za mizigo na ndege zitazokuwa zinafanya safari za dharura pamoja na kuzuia shughuli za ibada.
Uganda na Botwasana, licha ya kutokuwa na mgonjwa hata mmoja,nao wamechukua maamuzi magumu ya kuwaweka katika karantini ya wiki mbili wageni wote wataoingia katika nchi hizo kutoka katika mataifa yaliyoathirika vibaya na ugonjwa wa Corona.
Cha kushangaza,sisi pamoja na idadi ya wagonjwa kuongezeka,bado tunasita kuzui wageni kuingia nchini kutoka katika mataifa ambayo yameathiriwa vibaya na kinachonishangaza zaidi ni kuwa licha ya serikali kuzuia mikusanyiko,iko kimya kuhusu mikusanyiko ya watu kwenye nyumba za ibada.
Nasema hivi kwasababu kesho ni Ijumaa,keshokutwa ni Jumamosi na mtondogoo ni Jumapili, hizi zote zikiwa ni siku za watu kukutana na kuabudu.
Labda tujiulize,mikusanyiko inayohusiana na mikutano,semina,n.k,ina tofauti gani na mikusanyko ya watu katika kufanya Ibada tena nchi nzima?
Nimemsikia kiongozi mmoja wa Kiisilamu kupitia kituo kimoja cha Radio akitetea uamuzi wa kuzuia madrasa kwa hoja kuwa hata Mtume alizuia watu waliokuwa wananuka midomo kwa kutafuna vitungu wasiingie katika nyumba ya Ibada ili wasikwaze wengine akitumia mfano huo kuhalalisha zuio la madrasa akimanisha hata Mtume hakutaka Ibada itumike kukwaza waumini/kuleta madhara kwa waumini.
Je,wadau nyie nini maoni yenu kuhusu Ibada kuendelea katika kipindi hiki?