Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Kama unafuatilia vyombo vya habari,utaona ni kwa kiasi gani Mataifa mbalimbali yanavyofanya maamuzi magumu kukabiliana na ugonjwa huu yakiwemo hata Mataifa jirani kama Rwanda na Uganda.

Kwa mfano,Rwanda wameshatoa tangazo la kuzui ndege kuingia nchini mwao kuanzia kesho isipokuwa ndege za mizigo na ndege zitazokuwa zinafanya safari za dharura pamoja na kuzuia shughuli za ibada.

Uganda na Botwasana, licha ya kutokuwa na mgonjwa hata mmoja,nao wamechukua maamuzi magumu ya kuwaweka katika karantini ya wiki mbili wageni wote wataoingia katika nchi hizo kutoka katika mataifa yaliyoathirika vibaya na ugonjwa wa Corona.

Cha kushangaza,sisi pamoja na idadi ya wagonjwa kuongezeka,bado tunasita kuzui wageni kuingia nchini kutoka katika mataifa ambayo yameathiriwa vibaya na kinachonishangaza zaidi ni kuwa licha ya serikali kuzuia mikusanyiko,iko kimya kuhusu mikusanyiko ya watu kwenye nyumba za ibada.

Nasema hivi kwasababu kesho ni Ijumaa,keshokutwa ni Jumamosi na mtondogoo ni Jumapili, hizi zote zikiwa ni siku za watu kukutana na kuabudu.

Labda tujiulize,mikusanyiko inayohusiana na mikutano,semina,n.k,ina tofauti gani na mikusanyko ya watu katika kufanya Ibada tena nchi nzima?

Nimemsikia kiongozi mmoja wa Kiisilamu kupitia kituo kimoja cha Radio akitetea uamuzi wa kuzuia madrasa kwa hoja kuwa hata Mtume alizuia watu waliokuwa wananuka midomo kwa kutafuna vitungu wasiingie katika nyumba ya Ibada ili wasikwaze wengine akitumia mfano huo kuhalalisha zuio la madrasa akimanisha hata Mtume hakutaka Ibada itumike kukwaza waumini/kuleta madhara kwa waumini.

Je,wadau nyie nini maoni yenu kuhusu Ibada kuendelea katika kipindi hiki?




 
Pia kufunga mipaka na kuwataka watu wote kusalia majumbani kuanzia kesho kwa angalau siku 14?
 
Unapaswa kujiongeza wewe mwenyewe kwa sababu haulazimishwi kwenda msikitini au kanisani!
 
Anayehusianisha siasa za uchadema na uccm na janga hili ambalo Chancellor Merkel kaliita changamoto yake kuwa kubwa kuliko za Vita vikuu vya pili ni juha kuliko kawaida, hajui anachoongea na ni wa kupuuzwa kama mwenyewe anavyojitanabaisha.
Hatari sana mkuu hizi siasa zetu,maana kabla hata ya kutangazwa mgojwa mmoja wa corona kuna watu walikuwa wanaomba hili gonjwa lije na kuwauwa maccm halafu mtu huyo huyo ndio analalamikia serikali kuwa haiko serious kukabiliana na corona.
 
Siyo kila kinachofanywa na jirani tuige. Mu7 kaagiza ukikutwa na Corona unawekwa karantini wiki mbili na kila siku unajigharamia takribani laki na nusu je nayo tuige?
 
Sasa wazuie ibada,lakini mipaka haijafungwa? Ndege zinaingia kila siku....inasaidia nini?sioni haja ya kuzuia ibada,kufunga mashule at the same time wageni wanaingia kila siku kwa usafiri wa anga!

Mpk sshv Uganda hakuna maambukizi sbb wamezuia usafiri wa anga na kufunga mipaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wachina hawaamini kama kuna Mungu. kirusi chao cha korona ni kwa ajili ya kuhalalisha wanachoamini. kama tunafika mahali tunaambiwa tusiende misikitini kwa ajili ya Swala ya Ijumaa au tusitakiane amani kwa kushikana mikono kwenye Misa ni kama tunaambiwa hakuna Mungu kama Wachina wanavyomini.
 
Kiufupi Tanzania ni kichekesho tuu , hili janga inawezekana mamlaka husika na watawala hawana uelewa nalo , au wameamua kupuuza , hata hvyo hii awamu suala la Afya sio kipaumbele hata kdogo ...
 
Salary Slip,
Mkuu hebu acheni woga usio na maana jamani..kama corona iko serious ianzie Magogoni!..rate ya kufa Africa ni ndogo sana!
 


Leo Warwanda kibaoo wamekuja dar ..kuna kazi hapo?
 
Salary Slip,
Kuigaiga tutaiga udicteta. Tuhifunze kuthamini vyakwetu ikiwa ni pamoja na akili, utamaduni na utaratibu wetu.
 
Nawashauri mfute maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu ili bajeti ya sherehe hizo muielekeze kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

Mmefanya sherehe hizo mwaka 2016, 2017, 2018 na 2019 na mgeni rasmi mnayemualika hajawahi kuwapa neno la faraja zaidi ya kuwaongezea STRESS na ugumu wa maisha.

Kwa busara zenu, naomba mwaka huu muahirishe ili:

> Fedha itakayookolewa isaidie katika mapambano hayo;
> Msiwatie presha watumishi pale watakaposikia ngonjera zilezile maana

BAJETI YA MISHAHARA kwa mwaka huu wa fedha haina jipya.
 
Hio ndio siku ya watu wengi pale kupiga pesa...wakiifuta inamaana watashindwa kupiga mpunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…