Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

kwani ni lazima tuige ki;a kitu kutoka kwa watu wengine? Kama wengine wanaiogopa hiyo colona basi wakalale lakini hii kwetu iwe fulsa tumepewa neema hatujafa kwa kolona ni muda wa kupiga kazi
 
Africa tumeshapitia majanga mengi sana ya hatari kuzidi hii corona. ..hatuna sababu ya kuogopa hili nalo litapita. .jamani uusikie huu ugonjwa unaoitwa ebola..watu wa liberia wanaelewa zaidi
 
Ukitazama hatua ambazo Rwanda, Uganda na Kenya wamechukua kweli unapata kipimo kizuri cha Serikali yetu. Hatua tulizochukua ni hafifu mno. Hii si sawa kabisa kwa Watanzania. Huwezi weka kitu chochote mbele ya afya ya watu wako.

Serikali inafikiria nini hadi inashindwa kuchukua hatua zaidi?! Tunaweza tukawa hatujafikia hatua ya "mitigation measures", lakini hata hii ya "containment measures" ya kuwa strict na wanaoingia nchini haijakaa sawa, inazidi kujenga hofu vile inatekelezwa.
 



Kema kaandika
Rwanda wagonjwa 17-lockdown tayari

Kenya wagonjwa 15- lockdown tayari

Uganda mgonjwa 1-lockdown tayari

Tanzania wagonjwa 12- tuchape kazi

 
Rafiki yangu huko Italy kanitumia hii.


“Tumepoteza matumaini ya kulidhibiti janga hili.Tayari tumeshakufa kimwili na kiakili na majibu yote duniani yamekwisha.Tumaini la mwisho lililobaki litatoka angani tu (mbinguni)”
Giuseppe Conte
Waziri Mkuu wa Italy

Mimi ni muumini wa kweli, ila kwenye ukweli tuambiane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyefundishwa kuchamba huwa anachamba sana hadi anajiumiza
 
Waafrica tunaonekana ni wepesi sana kuamini ndio maana africa ndiko kwenye dini za kila aina na matapeli wengi wa dini.

Bado tunasua sua kufunga sehemu za kuabudia kama misikiti na makanisa kwa kama sehemu ya kupambana na corona


Mimi binafsi naunga mkono sehemu hizi zifungwe watu wafanyie ibada majumbani.

Najua viongozi wa dini wanapinga hili kwa sababu wanakula kwenye hizo ibada na mapato yao yanategemea mikusanyiko.

Tusiweke vidingizio eti kuna dua au sala za corona.. hata majumbani tunaweza kufanya.


Wala tusiwatishe waamini kwamba watakufa wasipo kujanibadani.. huu ni utapeli mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafunga sehemu wanayokutana kwa wiki Mara moja unaacha usafiri wa umma, masoko, vilabu, bar, vijiwe vya kahawa nk.

Ukifunga kanisani basi Kila mmoja abaki kwake.
 
Zifungwe tu ila mwahaikishie makasisi manabii na wazebedayo wanapataje sadaka zao....watawaunga mkono 100 asilimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninajua waziri wa Tamisemi mh Jaffo na RC Makonda mnapita sana humu Jf.

Naomba mnipatie jibu la sawali langu kuhusu msongamano wa abiria ndani ya mabasi ya mwendokasi wakati huu wa Corona, Mnafeli wapi?

Ni hilo tu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ninajua waziri wa Tamisemi mh Jaffo na RC Makonda mnapita sana humu Jf.

Naomba mnipatie jibu la sawali langu kuhusu msongamano wa abiria ndani ya mabasi ya mwendokasi wakati huu wa Corona, Mnafeli wapi?

Ni hilo tu.

Maendeleo hayana vyama!
ni kweli wangeweka utaratibu mzuri ambao hautakuwa na hasara kubwa kwa wamiliki wa mabasi na mwendokasi ili kupunguza msongamano kinga ni bora kuliko tiba..
mfano trafiki wasitoe faini yoyote kwa daladala mwezi mmoja isipokua ile iliyozidisha abiria wajikite kwenye kutoa elimu tu na kwa upande wa mwendokasi serikali ifidie hasara itayopelea kwa kupakia level siti si kuna pesa za mwenge jaman zifanye hiyo kazi.
 
Nilimsikia kondakta mmoja akisema

Basi refu la Mwendokasi linabeba abiria 38 waliokaa, lile Fupi linabeba 24. Ila likipakia kwa kusimamisha refu wanafika mpaka 200 na fupi linabeba 120. Kama takwimu hizi zina ukweli, changanua mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…