Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Kufunga makanisa na misikiti ni kukosa imani. Njia pekee ya kukabiliana na Corona ni kuwa na Imani na kumtumainia Mungu.

Bado tuna nafasi ya kumlilia Mungu kwa kuonesha dhamira ya dhati kukusanyika nyumba za ibada. Hapo Imani yetu itatuponya.
Kwa hiyo wengine wanaokufa hawana imani? Acheni upoyoyo na dini zenu feki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufunga makanisa na misikiti ni kukosa imani. Njia pekee ya kukabiliana na Corona ni kuwa na Imani na kumtumainia Mungu.

Bado tuna nafasi ya kumlilia Mungu kwa kuonesha dhamira ya dhati kukusanyika nyumba za ibada. Hapo Imani yetu itatuponya.

kama imani iko hvi. yale maji na sabuni milangoni pa makanisa yetu ni ya nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini serikali yetu imeacha kudhibiti mikusanyiko ya kidini kunusuru maisha ya watanzania dhidi ya corona. kwanini Jamani tunaendelea kunyamaza? Kwann nyuo na mashule yamefungwa lakn makanisa na misikiti imebaki? Kwann viongozi wetu dini wameshindwa kuwa wazalendo? Kweli sadaka ni bora kuliko uhai ya watu?.je ni kweli Mungu yuko makanisani na misikitini tu.
Mkuu kama ungalijua ukuu na karama za Mungu, utisho wa gonjwa la Corona ungaliuacha tu mikononi mwake. Hoja pengine ingalikuwa ni kwa viongozi wa dini kuendesha ibada zao kwa utaratibu maalum kwa ajili ya "social distancing".

We tambua tu, kuna baadhi ya mikusanyiko kutokana na umuhimu wake haikwepeki. Ya Kaisari mwachie Kaisari na yake Mungu mpe Mungu. Mungu huwakirimia wote wema na waovu kwa rehema na neema zake, ndiyo maana hubaki kuwa Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufunga makanisa na misikiti ni kukosa imani. Njia pekee ya kukabiliana na Corona ni kuwa na Imani na kumtumainia Mungu.

Bado tuna nafasi ya kumlilia Mungu kwa kuonesha dhamira ya dhati kukusanyika nyumba za ibada. Hapo Imani yetu itatuponya.
Mungu hakai kanisani au msikitini.
Hiyo ni mikusanyiko kama mikutano mingine.
Kuikataza hakutenganishi watu na Mungu.
Kwa kutokumjua Mungu wa kweli na kukosa maarifa, waafrika tumeshika dini hadi kuweza kuwa maangamizi yetu wenyewe.
Shetani kupitia hapo hapo kwenye huo ujinga, akapenyeza mawakala wake kuwa viongozi katika hayo hayo makanisa na misikiti.
 
Ni kweli Mungu yupo kila mahali( Omnipresent) lakini Mungu anachoangalia ni Imani yetu kwake. Kuacha kwenda kanisani au msikitini ni kukosa imani kwa sababu ukienda unahofia Corona.
 
Leo Waziri ametangaza ongezeko la watu Walioambukwizwa corona lakini .jana watu wamejazana makanisani wakiambikizana. shule na vyuo vimefungwa lakini misikiti na makanisa imebaki ikiendeleza kusambaza.
Jana Maaskofu wamepongeza hatua ya rais wetu kuacha makanisa yaendelee na ibada na kuwa watu wachape kazi. Sijui kama ombi lako litasikilizwa.
 
Ni kweli Mungu yupo kila mahali( Omnipresent) lakini Mungu anachoangalia ni Imani yetu kwake. Kuacha kwenda kanisani au msikitini ni kukosa imani kwa sababu ukienda unahofia Corona.
Unarudi pale pale kwenye tatizo la msingi. Uhusiano wetu na Mungu upo hata bila uwepo wa makanisa na misikiti.

Pale ni kusanyiko la waaminio tu.
 
Kufunga makanisa na misikiti ni kukosa imani. Njia pekee ya kukabiliana na Corona ni kuwa na Imani na kumtumainia Mungu.

Bado tuna nafasi ya kumlilia Mungu kwa kuonesha dhamira ya dhati kukusanyika nyumba za ibada. Hapo Imani yetu itatuponya.
Walio tuletea imani za dini wameshafunga makanisa yao. Jana waliendesha ibada online,tulio pokea imani tukajana makanisani... Waafrika sijui tuna shida gani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wangu wa dini nawasihii kwa unyenyekevu mkumbwa. Corona ipo kabisa!

Msongamamo ninauona kwenye nyumba za ibada si wa kuridhisha. Kumbukeni kuwa coronavirus anaweza kukaa kwenye hewa kwa muda wa saa nane. Sasa hiyo misongamano tunayoona haiwezi kutusababisha maambukizi? Pomoja na Serikali kuturuhusu tuendelee na ibada, tulipaswa tutumie hekima kuwakinga watu wetu.

Serikali wametupa uhuru, lakini tulipaswa kutumia uhuru wetu kwa hekima.Tutaua watu jamani tuchukueni hatua. Kama tuna hofu ya kukosa sadaka, Mungu atatunza kwa namna anaejua yeye. Mbona aliwatunza wana wa Israel kwa miaka arobaini jangawani?

Tunahofia nini kufunga nyumba za ibada? Wizara ya Afya wasema kwamba mtu akikohoa, anaweza kusafirisha hewa yenye makohozi kwa mita nane. Pia mtu akipinga chafya anaweza kusafirisha hewa hio kwa mita sita. Sasa huo umbali tunaouona kwenye nyumba za ibada huzidi hata setimita nane!

Tafadhali, tutadaiwa na Mungu kama tutasababisha vifo kwenye nyumba zetu za ibada!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasaka imepita bila hatua yeyote kuchukuliwa mimi ni catholic mpaka jana watu walikuwa wamejazana maelfu kwa maelfu makanisani maana serikali hawakupiga marufuku na ugonjwa ndio sasa unashika kasi na tare 23/24 ndugu zetu waislamu wataanza mfungo wa ramadhani.

Je ukija kupiga marufuku uku badae wakiwa kwenye mfungo hauoni tutaleta double standard kwao na watasema wameonewa? maana ugonjwa ulianza muda?

Ushauri wangu ndugu zetu kwanza wanapenda sana kuswali ukiwapiga stop uko mbeleni lazima italeta mgogoro nashauri usizuie tena watu kukusanyika kusali na kuswali endelea na msimamo wako maana kama ni kubugi ulikosea mwanzo usilete double standard kwa umma tukomae hata tuwe na wagonjwa elf kumi.

Tumsifu Yesu Cristo Mungu Ibariki Tanzania.
 
Dini yangu inanifundisha Mungu ni muweza wa yote ,hata Corona ipo ndani ya uweza wake hivyo kinachohitajika ni suala la Imani tu kwa Mungu.
Dini yako imekupotosha kuhusu Mungu. Mungu ameweka kanuni na sheria za kimaumbile ili ziendeshe ulimwengu.

Kwa mfano ukitaka kupaa kama kunguru hutaweza hata kama una imani kubwa sana kwa Mungu.

Covid 19 inaambukiza, ili kupunguza maambukizi sharti tupunguze au kusiwe na mikusanyiko ya watu.

Hiyo ni law of nature iliyowekwa na Mungu, ukipinga unakuwa unapingana na huyo Mungu.

Ndio maana sikuamini pale Gwajima aliposema Covid-19 haitafika Tanzania wakati mipaka ilikuwa wazi kabisa. Nilijua kanuni za maumbile zitam prove wrong.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu janga hili la CORONA liingie nchini kwetu nmekuwa nikisikia watu na sirikali ikitusisitizia kutokufanya mikusanyiko ISIYO YA LAZIMA.

Mpaka sasa mi napata mkanganyiko, mikusanyiko ya LAZIMA ni ipi kwa mfano na ile ISIYO ya lazma ni ipi kwa mfano.

Mi nahisi kwenda kanisani nako ni Mkusanyiko usio wa lazima[emoji34][emoji34]ila sijui waumini mnaonaje.

Nipo nasikia DW, Kuna mchungaji nmemsikia akisema kwenda kanisani ni Mkusanyiko wa lazima[emoji56][emoji56][emoji56].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine huyo hapo
Huyo mchungaji nimemsikia maana nimesikiliza hiyo DW..nimefikiria nini kimo rohoni mwake kinachomwongoza kuongea namna hiyo
Screenshot_2020-04-13-14-04-43.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom