… ili tushinde vita hii uliyoianzisha, ningeshauri pamoja na hatua ulizochukua fanya haya ya msingi ili yatusaidie kupiga vita dawa za kulevya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla:
Kwanza : Akamatwe mara moja AGNESS JELARD MASOGANGE, mtanzania aliyekamatwa na dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioi 6.8 nchini Afrika Kusini mwaka 2013, alifikishwa mahakamani na kupatikana na hatia na kuhukumiwa. Kwa sasa yupo hapa Dar es Salaam. AKAMATWE, aisaidie polisi ili tujue wapi alitoa shehena hiyo kubwa ya dawa za kulevya (sitanii…, niko “serious “)
Pili : JACQUELINE CLIFFORD FITZPATRICQUE (JACK PATRICK) aliyefungwa gerezani nchini Macau-China kwa kosa la kusafirisha mzigo wa dawa za kulevya kutoka Tanzania, AKAHOJIWE huko huko au tuwasiliane na serikali ya huko itusaidie kumhoji ili tujue ni wapi alipata huo mzigo aliokamatwa nao
Huo ndiyo ushauri wangu kwa leo, Mhe. Makonda.. I hope.. hii itakufikia tu..