Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Mkuu wa mkoa anaongea saa 5 ya kingereza au? yaani saa 11 au mbona giza tu na sasa ni saa tano inaelekea na nusu au kaahilisha.
mwenye kujua atujuze popcorn zinaisha
Saa 5.30 ndo ananza kuongea..!
 
Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa sawa je mbinu alizotumia zilikuwa sahihi kuwatangaza hazarani ? je hao aliowataja ni nani aliefungwa ? kama hawajafungwa kwa nini aliwataja ? kwa nini pia anatumia sana kituo ambacho pia kinahusishwa na inshu ya madawa ? ukitaka kumkosoa mwenzako anza kwanza na wewe MAKONDA ni mtoo wa masikini anavyosema yeye nini juu ya ukwasi alionao kautolea wapi ? au na yeye anahusika na ngada ? anataka kuwaharibia soka hawa ili nae watu wake wapige kazi kwelikweli ?
Well said
 
Ukimya wa Mwigulu kuhusiana na swala hili unatia mashaka sana.Jamani hata pamoja na bosi wake kuliongelea,yeye hajaamsha hata mdomo!Why?Kweli ni vigumu kujua nia halisi ya RC. Makonda katika hili swala,lakini yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani alipaswa kutoa msimamo wake hata kama ni kwa ku-pretend tu.
Uko sahihi kabisa kuna kitu kikubwa kimejificha ngoja tuone
 
Angalieni Clouds TV ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anaelezea mkakati wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya. Huu ni mkakati wa awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza ilihusisha baadhi ya watumiaji wa madawa hayo wakiwemo wasanii.

Tuwe pamoja

UPDATES
*Makonda: namshukuru Rais kwa kuniunga mkono katika mapambano haya dhidi ya madawa ya kulevya. Alifanya hivyo wakati wa siku ya sheria na ameniunga mkono wakati akiwaapisha wakuu wa vyombo vya dola

*Makonda: Tulipata taarifa juu ya watumiaji wa madawa ya kulevya wakiwemo wasanii. Niliwaita waje Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ili tupate maelezo ya kina. Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kukamata ila anaweza kumuita mtu yeyote wakati wowote na mahala popote
* Makonda: Nawashukuri sana walioitikia wito huo akiwemo TID ambao waliitikia wito huo na kukiri kutumia madawa ya kulevya

Makonda: Naishukuru Mahakama na Jeshi la Polisi chini ya Kamanda Siro katika mapambano haya dhidi ya madawa ya kulevya. Wanafanya kazi kubwa na usiku na mchana katika mapambano haya
Makonda: Nilikaa nao wote niliowaita kuanzia saa nane hadi tisa usiku na wote wamekiri kuwa wanatumia madawa na wameanidi kuwa Raia wema

MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA AWAMU YA PILI
*Makonda: Tumemaliza awamu ya kwanza. Tunaingia awamu ya pili ambayo itakuwa ngumu kidogo.inahitaji watu wenye vifua na wenye hofu ya Mungu
Makonda: Tunajua njia zote zinazotumika kuingiza madawa ya kulevya nchini na tutazidhibiti
 
Ukimya wa Mwigulu kuhusiana na swala hili unatia mashaka sana.Jamani hata pamoja na bosi wake kuliongelea,yeye hajaamsha hata mdomo!Why?Kweli ni vigumu kujua nia halisi ya RC. Makonda katika hili swala,lakini yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani alipaswa kutoa msimamo wake hata kama ni kwa ku-pretend tu.
Wanasiasa na wafanyabiashara ndio wanafaidika na hii biashara ya madawa ya kulevya ndio maana tunasema hii vita ni ngumu,Makonda anahitaji support kwenye hili.Baada ya Makonda kukamata baadhi siku ya pili Nape akaanza kuwatetea siku ya 3 mbunge Goodluck Mlinga akasema anawajuwa atawataja baadae tena Msukuma akaanza kutoa tuhuma kwa Makonda.Muda unavyokwenda mengi yatajulikana I hope Makonda ataendelea kuwasha moto tuyafahamu mengi
 
Ukimya wa Mwigulu kuhusiana na swala hili unatia mashaka sana.Jamani hata pamoja na bosi wake kuliongelea,yeye hajaamsha hata mdomo!Why?Kweli ni vigumu kujua nia halisi ya RC. Makonda katika hili swala,lakini yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani alipaswa kutoa msimamo wake hata kama ni kwa ku-pretend tu.
hii vita sio ya kuropoka ropoka. hili sio swala la sukari au mahindi ya njaa. tusimjudge mwigulu
 
Back
Top Bottom