Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Kuna series Hapa..Naicheck Inaitws Narcos..Naifananisha na makonda anachokifanya Sasa
 
Tumalize kwanza la madawa baada ya hapo hilo lingine litafuata!! Wanataka kumpunguza kasi!!
 
Sisi tutakuwa watu wa aina gani??
Akitajwa Idd Azan tunasema sawa..

Wakiitwa makada wengine akina wema sepetu tunasema sawa..

Wakati huo wengine wanadai kwanini "Riz-one"..

Akiitwa Mbowe tunalalama na kudai ni vita ya kisiasa..

Hii nchi ngumu sana!
 
Mkuu Tetty,nimemsikiliza RC Makonda lakini kuna mahali sijaelewa mantiki yake. Pale anapotaja majina ya akina fulani lakini anashindwa kutaja majina mengine na kusema tu mmiliki wa a,b,c,d na kuendelea,maana yake ni nini? Hapa kuna tafasiri nyingi,lakini mbili tu ni kwamba mmoja aliyetajwa jina binafsi ni mhusika wa moja kwa moja na yule aliyetajwa kama mmiliki ni kuwa inawezekana katika biashara yake kuna kitu kama hicho,hivyo yeye anahitajika kama kuweka "clarification". Ni vyema ingetumika, "mmiliki wa club ya usiku na casino fulani kama ilivyotokea kwa wamiliki wengine.
 
Hahahaha ngoja episode iendlee. Nimevlia namsikiliza lucky dube na ngoma yake inaitwa rasta man's prayer, kuna sehemu anasema

"Those that smoke
marijuana
Wanna thank you father
For making it grow
internationally,
They wanna thank you
lord
Even though police cut it
down,
Sometimes they burn it
down
But it grows again
Thank you father"

so ngoja tuendelee kushuhudia hi mv
 

Huyu RC ana busara sana na anajua nini anaongea, wakati gani, namna gani kwa utaratibu upi.... Pia anajua nini kianze na kipi kifuhate..... Tumuunge mkono........ Sasa wanaopiga kelele (Wanajijua kama wana maslahi ama kwa ushabiki tu) baadaye kidogo mtaamua wenyewe kwa busara zenu kuchagua ushabiki wa kijingakijinga ama ukweli wenye faida kubwa kwa maslahi ya nchi hii kupunguza hili tatizo ama kulimaliza kabisa..... Madawa ya kulevya hayana maana kabisa anayeshabikia hii biashara ni wa kuwamwonea huruma sana sana..... Waathirika wenyewe wanaomba kusaidiwa maana ni sawa na utumwa, unakuwa mtumwa hata kama hupendi, hali ile ni mbaya kabisa, Hasara zake ni nyingi mno; inachangia uhalifu kwenye jamii, inapoteza nguvu kazi muhimu, upeo wa kufikiri unashuka chini (Elimu) Inachangia kuenea kwa magonjwa (Afya) nk ...........Big Up RC! Tuko pamoja sana
 
ina maana wote wamesingiziwa au mbowe peke yake?
 
mwigulu hawez kuwa rais.. zamu ya anaefata ni muislamuuu.. na hadi zamu ya mkristo irudi mwigulu ashafika miaka 60 ambapo kwa ccm ni hawakupi nafasi ukiwa above 60
 
Hiii Vita Makonda ametangulizwa tu, hata waliotajwa wenyewe wanajua Makonda ni mjumbe tu kwenye hili sakata.
 
Naona hata Polisi wenye hukumu.la kufanya interview watuhumiwa jukumu hili linafanywa na Mkuu wa Mkoa.Ni bora Tuambie kwamba ameteuliwa kuwa IGP au Waziri wa mambo ya ndani.

Naona jinsi jamaa atakavyoanguka vibaya
 
Umenena vyema ndugu
hii vita si ya Makonda pekee
 
Ukiangalia suala la Lema ni 'sheria inafuata mkondo' na ukigeukia hili kuna wanaoambizana kuwa "hachomoki hapa"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…