Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Hiki hujakisoma post namba moja? "Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza" - RC Makonda

sio kweli Faiza! Kama kweli anafahamu zaidi hii orodha ingekuwa na majina kamili. Utafahamu nini kwa mtu anayeitwa Trinity Mmiliki au Slipway, Deo Mchaga au Rose Mchina au Gene au Genevova. Inaonekana amekuwa akipokea simu na kukimbilia kutangaza, ona hata hakuweza kuichapisha hii orodha ili kuweka kumbukumbu vizuri. Majina mengi ni ya kubabaisha tu.

Vita hii ni yetu sote, kweli hakuna uchungu mkubwa kama kukutana na mateja- afya zao, kauli zao, vaa zao na ukifikiri hawa ndio wanatajarisha wengine wanaishi mbinguni- unawahurumia sana. Lakini pia hawawezi kufanya kazi tena na mara nyingi hudokoa. Hii vita halali kabisa, lakini nahofu, wakuu wanaiparamia na tutabaki na kesi nyingi ambazo serikali itashindwa (pengine serikali itashinda kisiasa) lakini hatutakuwa tumeshinda hii vita. Hatujajipanga. Mkuu wa Mkoa wa Dar anaharibu mikakati ya mapigano...huwezi ukarukia kutangaza kabla ya kufanya uchunguzi. Kwa mfano hana haja ya kutangaza atakutana na x au y ijumaa- angeweza kufanya kwa utaratibu kisha wale ambao wataonekana wana kesi za kujibu akatutangazia. Ningemwona yuko kisayansi, sasa hivi anavuruga vita kwa kutumia nafasi yake.
 
Nimeshangazwa na majina yaliotajwa baada ya kuona jina langu,haiwezekani mtu uuze bangi na mirungi na gundi alafu utajwe......😉😉😉😉😉😉😉😉😉😉
 
Nani kakwambia kuwa na mahusiano ya kimapenzi offence
 
Rafiki yako akiwa mwizi.na wewe ni mwizi?
 
kama
Wewe ndio wakujiongeza.. hauhitaji kutumia akili nyingi kutambua kuwa kunatofauti kati ya Philemon na Freeman.. wala haihitaji akili yakufundishwa.. hata mahakamani hawa ni watu wawili tofauti
Kama ulijua hilo kwa nini ulikuwa unatupotezea muda wetu humu ndani. umeshaona middle na last name yake alafu bado unauliza maswali kama tuko kwenye pombe za kienyeji.
 
Naomba mwenyekiti wa chadema taifa na wengineo mlioitwa polisi ijumaa wekeni ulinzi mkali wa kutosha kwenye nyumba zenu wasije wakawawekea madawa kama vidhibitisho maana tunakoelekea hatupajui .
 
Ndio maana ulishaambiwa hawakurupuki kama wewe unavyotaka, wanajua nini wanafanya yote yatafahamka muda si mrefu
Hizo Siasa utaona kama utakuja kuyasikia majina yao mbona wengine amewataja,kama hajakurupuka si angesubiri mpaka pale atakapowajua majina yao huo ni uhuni
 
Hi ni vita ya matajiri waliosaidai upinzani na wapinzani,kamakuna mtu alitakiwa namba moja kuhojiwa Tanzania ni Ridhiwani.Ametajwa sana miaka ya nyuma hadi kuna watu wanasema alishikwa China akakombolewa na gesi ya mtwara.Mbowe anatajwa ili kudhoofisha upinzani au kuuwa kabisa kampuni ya mafuta ya GBP wao wanaukumiwa kwa kutoa mafuta ya bodaboda wakati wa kampeni za lowassa,Manji uyanga na kusaidia kampeni za lowassa.Mmiliki wa Efm anaisiwa lowassa yupo nyuma yake ,wamiliki wa clouds wanaisiwa miaka mingi niwauzaji na waagizaji lakini wameachwa redio yao ndio inatumika kutaja wauzaji madawa.Lengo lao wakamsachi mbowe kwa kisingizio cha madawa lakini wanayao.
 
Kwambaliiiiiiii kiona mbali changu kinanionyesha tukimpoteza mkuu wa mkoa wetu pendwa,Nakiona kilichomkuta yule Dada yetu miaka ileeeeeeee aliyekuwa na majina ya wauza madawa ya kulevya tukaishia kuambulia machozi akiwa amerest in peace.
Hakika anapotea.
 
kama

Kama ulijua hilo kwa nini ulikuwa unatupotezea muda wetu humu ndani. umeshaona middle na last name yake alafu bado unauliza maswali kama tuko kwenye pombe za kienyeji.
nina mashaka na uelewa wako.. siwezi kuendelea kubishana na wewe, nikupoteza muda wangu.. mkuu wa mkoa mwenyewe ameulizwa imebidi arekebishe
 
Kwan makonda anatangazia chini ya ardhi? Tuwe watulivu anaehusika na asiyehusika itafamika tu vizur
 
Magazeti ya kesho utasikia ....Gwajima kitazini" chadema yapatwa kwa jua"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…