Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 609
Hiki hujakisoma post namba moja? "Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza" - RC Makonda
sio kweli Faiza! Kama kweli anafahamu zaidi hii orodha ingekuwa na majina kamili. Utafahamu nini kwa mtu anayeitwa Trinity Mmiliki au Slipway, Deo Mchaga au Rose Mchina au Gene au Genevova. Inaonekana amekuwa akipokea simu na kukimbilia kutangaza, ona hata hakuweza kuichapisha hii orodha ili kuweka kumbukumbu vizuri. Majina mengi ni ya kubabaisha tu.
Vita hii ni yetu sote, kweli hakuna uchungu mkubwa kama kukutana na mateja- afya zao, kauli zao, vaa zao na ukifikiri hawa ndio wanatajarisha wengine wanaishi mbinguni- unawahurumia sana. Lakini pia hawawezi kufanya kazi tena na mara nyingi hudokoa. Hii vita halali kabisa, lakini nahofu, wakuu wanaiparamia na tutabaki na kesi nyingi ambazo serikali itashindwa (pengine serikali itashinda kisiasa) lakini hatutakuwa tumeshinda hii vita. Hatujajipanga. Mkuu wa Mkoa wa Dar anaharibu mikakati ya mapigano...huwezi ukarukia kutangaza kabla ya kufanya uchunguzi. Kwa mfano hana haja ya kutangaza atakutana na x au y ijumaa- angeweza kufanya kwa utaratibu kisha wale ambao wataonekana wana kesi za kujibu akatutangazia. Ningemwona yuko kisayansi, sasa hivi anavuruga vita kwa kutumia nafasi yake.