Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...



Hivi unadhani kile kinachoendelea kuhusu sakata la dawa za kulevya nchini,athari zake zikoje kitaifa??
 
Vita ya madawa ya kulevya ni kubwa kuliko tunavyofikiria.

Ukisikia mumeo, mkeo, hawara'ko, kaka'ko, dada'ko, mama'ko, baba'ko, babuyo, bibiyo, boss wako, rafiki yako, jirani yako, jamaa yako, mchungaji wako, sheikh wako au wewe mwenyewe unaitwa kuhojiwa usistuke.

Ni vita kubwa sana ambayo inagusa kila mmoja wetu kwa namna moja nyingine.

Tupambane kutokomeza unga, ni safari ndefu na ngumu.

Nchi imeanza kutikisika na ndiyo mwanzo.

Wapenda mema tushirikiane kwenye hili la sivyo sisi sote tutaingia kwenye janga tukitaka tusitake.

Tukiyawachia haya, utafika wakati tutawekewa madawa ya kulevya mpaka kwenye pipi, biskuti ili mradi tuwe wateja na watu waendeleze ushetani wao.

Tuungane bila kujali nani ni nani.
 
Bro Siro, nakufamu toka ukiwa Uru seminary, K'njaro Boys, Tosamaganga, Udsm nk. Nakushauri usidhalilishe weledi wako wala taaluma yako Bro.
 
Kama wanaushahidi kwann wangoje ijumaa badala ya kuamuru polisi wawakamate? Mwenye akili timamu anaelewa mchezo unaofanywa na makonda lkn hauwezi kuwa nawisho mwema.

Kuna strategies katika kufanya hivyo.

Mojawapo ni ku instigate forceful awareness kuwa none is exempted in this war.

Mbowe ana kila sababu za kuitwa polisi kujieleza.

Biashara zake za vilabu vya usiku ni kielelezo tosha kuwa anayajuwa mengi kuhusu "underworld".

Tuungane.
 
Ahsante
 
Sawa huyo ni mbowe, na je vilabu hawavijui vilipo? Tuachane na Mbowe what about others? Kwann wasingetuma polisi ghafla wawavamie na kusachi? Hivi unapotangaza kumtuhumu mtu kufanya jambo fulani wakati hujamkamata huoni kuwa unampa nafasi kuficha au kuharibu ushahidi wote? Mbinu anayotumia makonda hawezi kufanikiwa kamwe trust me.
 
Hiyo picha haikufai...hao ni third reich ....tofauti na hulka yako
Hii picha ina maana sana kwa dunia ya leo....tunaongozwa na illiberal democracy kila kona ya dunia ukiondoa westen europe.hio picha inatukumbusha kuwa hata uwe na nguvu gani basi huwezi kuifika ya Hitler..lakini hata kaburi yake hainekani...tenda wema watu walukumbuke kwa dua...
 
kuna vitu nkifikiria sana naona kama ukimkanyaga buibui unaweza kwenda kuzalisha mayai ndani ya kiatu chako maana hivi vitu naona kama kiiini macho. Hakuna kitu kilichokua na nguvu kama FARU JOHN leo yupo api? leo tunaona ishu ya madawa nayo imepamba moto... ngoja niishie hapa
 
Wakilikalia kimya suala la madawa, serikali ipo wapi?
Wakilivalia njuga, serikali ilikuwa wapi muda wote huo?

Ni vigumu sana kuwaelewa wanasiasa kama ilivyokuwa ngumu kumuelewa mwanamke..!
 
Akomae, vita dhidi ya madawa ya kulevya ni kali sana.

Ndio maana hao akina MSUKUMA wamenyanyuka juu yake baada ya kuona maslahi yao yameguswa!
Brother pamoja sana....kuna mambo ambayo lazima yatuunganishe na tuyapinge kwa pamoja.

Vita anayopambana nayo Makonda si yake peke yake bali ya kwetu sote.
 
Wewe muunge mkono tu kama unayo nia njema...

Mkiwa vitani siku zote huwa lenu ni moja...kumshambulia adui na sio kuchukua mashambulizi ya adui dhidi ya askari mwenzenu na kuanza kumshambulia...hapo adui atakuwa amefanikiwa ktk mbinu yake ya kuwachonganisha na mkiendelea kuhitilafiana atawapiga.

Vita hii ya dawa za kulevya ni kubwa na tunapaswa kuunga mkono kwa kufumbia macho vitu vidogovidogo kwa mfano suala la masogange dhidi ya Makonda ni suala la kipuuzi na propaganda za hovyo kabisa na bahati mbaya muandishi wa habari anasimama kuuliza huo ujinga hii inaonesha kama jamii hatuko pamoja kuondoa tatizo la dawa za kulevya.

Yaani waandishi wa habari wanasimama na kuuliza propaganda bila kujua kuwa wanaziimarisha na kwa namna moja au nyingine wanamuunga mkono adui...are we serious?????
 

Si umeona wamiliki wa Casino wameitwa pia,au hujaona?

Halafu ndiyo kwanza awamu (phase) ya pili. Usiwe na hofu, wengi wataitwa.

Niliandika hivi:

Vita ya madawa ya kulevya ni kubwa kuliko tunavyofikiria.
Ukisikia mumeo, mkeo, hawara'ko, kaka'ko, dada'ko, mama'ko, baba'ko, babuyo, bibiyo, boss wako, rafiki yako, jirani yako, jamaa yako, mchungaji wako, sheikh wako au wewe mwenyewe unaitwa kuhojiwa usistuke.

Ni vita kubwa sana ambayo inagusa kila mmoja wetu kwa namna moja nyingine.

Tupambane kutokomeza unga, ni safari ndefu na ngumu.

Nchi imeanza kutikisika na ndiyo mwanzo.

Wapenda mema tushirikiane kwenye hili la sivyo sisi sote tutaingia kwenye janga tukitaka tusitake.

Tukiyawachia haya, utafika wakati tutawekewa madawa ya kulevya mpaka kwenye pipi, biskuti ili mradi tuwe wateja na watu waendeleze ushetani wao.

Tuungane bila kujali nani ni nani.
 
Jamani mlioko mjini huko sasa hivi hakuna mateja tena? Ulevi umeisha huko?
 
Ok nilitaka watanjwe wale waliopo kwenye list ya kitwanga aliosema imeshafanyiwa uchunguzi wa kutosha na ipo verified kuwa waliopo wameshakuwa proven kuwa ni wauzaji na kilichobaki ni kuburuzwa mahakamani tu........ile ndio itumike ila hii ya kusema mtu aje tumuhoji wakati kumbe ushahidi hamna huoni ni kuchafuana tu after kutaja jina lake kwenye public....akikutwa hana hatia je utaita press kumsafisha??

Siku wasema tunasaka mashoga afu waseme mido luly njoo kwa ajili ya mahojiano wwe unafkiri watu watahisi nni kma sio kukuchafua tayari hta kma itajulikana hujihusishi na tabia hiyo??

WATUMIE LIST YA KITWANGA ILIYOKUWA VERIFIED ENOUGH OF THS POROJO
 
Jamani watu walilalamika kuwa Makonda kataja vidagaa Sasa na hawa je walio tajwa tena sio vidagaa????
 
Kwa majivuno na kiburi cha viongozi wetu, hali inayopelekea kuona watu katika jamii wasio na madaraka sio kitu. Kwani mimi nina jeshi linanizunguka, police na ninaweza kufanya ninachotaka. Hata kuingilia kazi ya chombo husika cha madawa ya kulevya kwani wao hawafai mimi nafaa zaidi. Hii ndio tuliokuwa tunaambiwa Tanzania mpya inakuja. Wasaniii wanajitahidi katika umaskini wao,hadi kuipaza Tanzania bila kusaidiwa, hata wanasaidia mnafikia uongozi mlipo. Kisha sasa hivi ni takataka. Mnawatumia kama toilet paper. Hata kama mtu amekosa,media dunia nzima aonekane kakosa, wakati bado ni tuhuma (tuhuma zinamfanya anakuwa guilt hata kabla ya investigation ).Wanasheria wetu kimya katika hilo sababu ya viongozi wa nature ya majivuno. Mungu sio Athumani. Usione umesimama usije ukaanguka.
 
Tofautisha wale wameitwa wamiliki kma wamiliki sio individual....... ina maana shareholders wa zile casino wanaweza tuma mwakilishi tu ila kwa mbowe kaitwa yeye kma yeye sasa kma issue ni hoteli zake mbona hajaitwa wamiliki au management rather kaitwa mbowe pekee??? Je hakuna shareholders wengine???

Hivi kwanini basi mutaje watu kuwahoji na kuwaachia wakati tayari kuna list ipo verified ya kitwanga na wanadai inaushahidi wa kutosha wakufungua kesi?? Why not use the verified list nyie mnatumia ya makonda ambayo inataka kuhoji tu hamuoni wastage of time and resources?
 
Jamani watu walilalamika kuwa Makonda kataja vidagaa Sasa na hawa je walio tajwa tena sio vidagaa????
Sawa tulitaka ataje vigogo ila njia aliotumia sio sahihi...... list bado haijafanyiwa uchunguzi unaitaja ya nni???

Bulaya na mdee na kambi ya upinzani inataka ile list ya kikwete na kitwanga ndio itumike yenye vigogo mwanzo mwisho maana hata lukuvi alisema ile ya kitwanga ikitajwa nchi itatikisika sasa kwanni wasiitaje ile tunakimbilia list isiyo na chembe ya ushahidi??!!
 


Kwa hiyo wewe ukienda TANESCO kutoa taarifa ya tatizo la umeme na ukamkuta mtu aliyekuibia jogoo lako naye kaja kuripoti tatizo hilohilo basi utamwachia? Kwamba kwa kumwachia basi tatizo la umeme litaisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…