Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Shida sio kuita au kuitwa, tatizo ni je ukishaita hao wahusika nini kinafuata?? tumeona wale wakina tid na Wema nini kimetokea, kweli muuza Unga anapewa dhamana?

Mbona wale akina Shikuba, Chonji, mama Leila hawakupewa dhamana? na mpaka leo wako jela??

Huweza kusema unapambana na wahalifu kwa kuwaita na kuwahoji then ukawaacha waende zao then unatuambia uko kwenye vita ya madawa, ni aibu, dharau na utoto uliopitiliza...
 
Sikia Jef Kirhiku, siku zote ukiona mtu anajihami basi juwa kuna anachokificha. Hawa jamaa wameguswa, walifikiri hivi ni zama za Kikwete, rais asiyefuatilia kauli zake mpaka akaja kudharauliwa na viongozi wake.
 
Mimi Sioni kamaliza kuna tatizo mtu akituhumiwa kwa kosa fulani, kumbukeni Ni tuhuma tu, na tuko kwny mchakato wa kuzithibitisha, wasiwasi na mihemko kwa watuhumiwa inatia mashaka zaidi!
 
Mbona tuliwasema juzi hapo baada ya kuhongwa mil 10? Kwani walifanyaje?....
Alisema Mbowe bungeni alitakiwa aripoti PCCB lakini uliamini, Je nini kinakufanya unakuwa mgumu kuamini Mbowe anauza madawa ya kulevya? nini kinakufanya huamini kuwa wabunge wanasinzia? au kusinzia ni Wasirra na marehemu Komba tu
 
Ukwel ukisemwa watu huinuka kuupinga.siasa za utaifa ziko wapi nchi hii? Kila kona siasa za uchama, itakuwa gumu sana kufikia hiyo demokrasia
 
Toa porojo zako hapa,wabunge wanawatumikia wananchi na wana haki ya kuhoji sehemu yoyote ile. Na makonda ni lazima ang'oke,akatumikie wauza unga wake GSM.
 
Siyo wakazi wa Dar es Salaam
 
Ndugu zangu habari za asubuhi, huku tunajiandaa kulala
Tafadhali fuatilia kwa makini hiki ninachokiandika hapa.. hii vita ya madawa ya kulevya ina agenda ya siri kama ingekuwa na lengo la kukomesha biashara hii haramu ingefanywa kwa kufuata kanunia na kwa weledi wa hali ya juu sana.

Kungefanywa uchungzi wa kina na baada ya uchunguzi waliobainika wangeitwa polisi kwa mahojiano zaidi kwa siri na kisha kupandishwa mahakamani.

Lakini kwa makusudi kabisa kinachofanywa leo kimesukwa kutaka kumchafua Lowassa baada ya mahakama ya kifisadi kushindwa kupata lolote la kumshitaki maana watu wengi waliamini kwamba atakuwa wa kwanza kushitakiwa kutokana na kusudio la uanzishwaji wa mahakama hiyo, sasa imeshindikana na kuna hisia kuwa jama huyu asipopata mkasa wa kufikishwa mahakamani wananchi watamuunga mkono kwa wingi.

Ndio maana ikatengenezwa mbinu na kama mnakumbuka ni kijana yupi aliyejitolea kumlipua Lowassa kwenye vyombo vya habari alipokuwa CCM ni Makonda.

Bahati mbaya jambo hili Baadhi ya viongozi wengi na mawaziri pia viongozi waandamizi hawakubaliani nalo wanaona ni siasa chafu zenye athari kwa nchi. Litakapotajwa jina la Lowassa pia litatajwa la Azim

Hayo majina kutajwa hadharani ni mkakati uliobuniwa ili siku akitajwa isemekane wengine walitajwa, lakini hakuna vita ya madawa ya kulevya inayopiganwa hivyo
 
Acha uongo wewe, usiandike kwa ajili ya kufurahisha au kuhadaa umma. Kama wanshindwa kukamilisha upelelezi wa mtu. Mmoja tu, kweli unataka kutaminisha kwa tuhuma hizi wana uhakika wa kuthibitisha mahakamani? Angalia mahaba yasikutie uchizi.
 
Usiweke siasa kwenye masuala kama haya CCM ndio inauza unga au? embu ushindani usiwepo bwana hauwezi jua? hapa tuangalie nani kahusika na sio chama bwana
Chama ni watu, bila watu hakuna chama. Iwe ni Cuf, Chadema au CCM au chama chochote kile, ikumbukwe watu ndio wanaounda chama. Na unaposikia chama ni kichafu maana yake watu wake wanaokiunda ni wachafu. Hivyo basi hata katika suala hili la madawa ya kulevya, Kama wanaCCM watabainika ndio wahusika wakubwa, basi ni dhahiri kuwa chama kimechafuka na kimeumbuka. Hii ni fact na si siasa.
 
Ficha uwezo wako wa kufikiria!

Kumkubali Rais Maghufuli, na uongozi wa Makonda, unahitaji hekima. Ni kweli tunahitaji viongozi hawa. Mwenyezi Mungu anajua zaidi, na analolitaka halipingiki. Mwenyezi Mungu awaongoze na awalinde. Tunahitaji kusaidiana nao katika uongozi wao, hakuna aliyekamilika isipokuwa ni Mola peke yake. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…