Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Serikali lazima isemwe.......

Mahakama lazima isemwe .....

Rais kachaguliwa na wananchi na wabunge wamechaguliwa na wananchi hivyo bunge kumsema Rais( Serikali) ni wajibu wake.......

Msituletee porojo za kichama kimoja na Mawazo mgando ya kupiga mapambio kwa kila kitu......

Kama rais na serikali Yake hawataki kusemwa dawa ni kujiuzulu tu......
Je bunge halipaswi kukosolewa?
 
Mashambulizi yenu wana Lumumba mjiulize hii dola ni ya uchwara au yetu sote?

Maana mnayemtetea amejivika ufalme.
 
Yes huyu Papa Lowasa atajwe kabisa
amtaje, watu wanaenda na sheria hawakurupuki kama yeye, kwanza mpaka sasa nahisi anajua na imemgharimu hata kama mkuu anampa kiburi, lakini nina uhakika usingizi sidhani kama anapata
 
Hawa wabunge wakae kimya. Mbona mengi tu ya msingi wanayakanyaga hapo bungeni iweje leo waambiwe wanalala waje juu? Kwani ni uwongo huwa hawasinzii huko bungeni? Mwacheni makonda hawahusu nyie endeleeni kupiga meza huko bungeni
 
Pumba tupu!!!!
Ushahidiiiiiiiiii
Tunasema ushahidiiiiii
Ushahidi
Ushahidi

Mnawakamata wakifanya biashara husika?

Mahakamani wapika/wauza gongo hupelekwa na mapipa yao ya kupikia gongo na madum.

Sasa hawa mtawapeleka mahakamani na mivyuzi ya paka?
Hio hainuhusu..km yupo kwenye list atajwe tu..Who is he by the way!!?? Makonda amtaje tu.
 
0df96ce3c129acbdd00907b6754804cf.jpg
lazima aseme ni nani kamnunulia hili gari la milioni 470,hawezi kutengenezea wauza unga soko.
Gari gani hii m470?
 
Mngekuwa mna umoja kama huu kwenye mambo ya msingi ningewaelewa lakini kwenye vita ya madawa ya kulevya hakuna mtanzania atakaewaelewa.
 
Nashangaa mtu anapanic na hausiki ,sasa kama hausiki nenda katoe maelezo kw1bza police watakusafisha wenyewe
 
Ndugu zangu habari za asubuhi, huku tunajiandaa kulala
Tafadhali fatilia kwa makini hiki ninachokiandika hapa.. hii vita ya madawa ya kulevya ina agenda ya siri kama ingekuwa na lengo la kukomesha biashara hii haramu ingefanywa kwa kufuata kanunia na kwa weledi wa hali ya juu sana.

Kungefanywa uchungzi wa kina na baada ya uchunguzi waliobainika wangeitwa polisi kwa mahojiano zaidi kwa siri na kisha kupandishwa mahakamani.

Lakini kwa makusudi kabisa kinachofanywa leo kimesukwa kutaka kumchafua Lowassa baada ya mahakama ya kifisadi kushindwa kupata lolote la kumshitaki maana watu wengi waliamini kwamba atakuwa wa kwanza kushitakiwa kutokana na kusudio la kujenga mahakama hiyo, sasa imeshindikana na kuna hisia kuwa jama huyu asipopata mkasa wa kufikishwa mahakamani wananchi watamuunga mkono kwa wingi.

Ndio maana ikatengenezwa mbinu na kama mnakumbuka ni kijana yupi aliyejitolea kumlipua Lowassa kwenye vyombo vya habari alipokuwa ccm? ni Makonda.

Bahati mbaya jambo hili Baadhi ya viongozi wengi na mawaziri pia viongozi waandamizi hawakubaliani nalo wanaona ni siasa chafu zenye athari kwa nchi. Litakapotajwa jina la Lowassa pia litatajwa la Azim

Hayo majina kutajwa hadharani ni mkakati uliobuniwa ili siku akitajwa isemekane wengine walitajwa, lakini hakuna vita ya madawa ya kulevya inayopiganwa hivyo
Ukitumwa, jua na kuweka akili yako sawa!
 
Rc mwenyewe huyo anafukuzia ubunge na kelele zoote hizo ni za kujijengea Nyamagana !. Wabunge kukosolewa kama watu binafsi kwa matendo yao ni sawa lakini si bunge kama taasisi na mhimili itakula kwako.

By the way nyani haoni la kwake . Sbb serikali na mkuu wake ndiyo wasiotaka kukosolewa kabisa na juhudi iliyopo ni kunyamazisha nchi na wananchi.
 
Lowasa kama anahusika aswekwe lupango tumechoka na wauza madawa et kisa wapinzan
 
Vitu vingine vipo wazi kabisa sema watu wanajitoa ufaham tu!

Mwengine nimemsikia akilalama bungeni kuwa "serikali inasema ina majina ya wauza unga sasa ni ya nn Makonda aite watu wao central", sasa km unajua serikali ina majina kwann upinge analolifanya makonda kwa mkoa wa dar es salaam!!? kwanini upinge pale mtu unaempenda anapotajwa kwenye list!! yan huko kwenye vyama vingine vya siasa kumekuwa ni pango la wahalifu ndo wanajificha huko!

Ila huu ni mwanzo tu ishu bado inaendelea, nimeona gazeti la jambo leo" linaendelea na kampeni yake ya kumsafisha manji, nashangazwa sn na hawa tunaowaita waandishi!!!!
 
ulikuwa na hoja kama yangu.Umenena kweli tupu.
Naona wabunge wanalalamikia kuhusu heshima yao wengi wao wa upande upinzani lakini wanasahau kwa namna wanavyo ongea bila hata breki juu ya rais ambaye naye anastahili heshima sawa na wao wanavyostahili.
Ukitaka kuheshimiwa jiheshimu na waheshimu wengine na si kutaka heshima upande wako tu bila kujali heshima ya wengine.
Mnapoteza muda kutetea watu wasiofuata misingi ya utawala bora na sheria pia.

Kama ametoa maneno ya kejeli Kwa bunge Kwa nini asiwajibishwe?

Rais kachaguliwa na wananchi na wabunge wamechaguliwa na wananchi huyo kondakta ni mteule tu na Utendaji wake una mipaka sasa analikoromea bunge halafu wajinga wachache mnatetea
 
Back
Top Bottom