Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

chama hakiwezi kuchafuka ila mtu na caree yake ndio anachafuka bwana. mbona mambo yanaeleweka???
Kwani huyo mtu si sehemu ya chama? Na kama ni hivyo, ni kwanini ilifikia mahala chama kubwa kikaitwa chama cha mafisadi? Si kwasababu mafisadi walikuwa ni sehemu ya watu wanaounda chama hicho? Ukweli ni kwamba hata kama utakataa kukubaliana name, bado huu ukweli hauepukiki, kuchafuka kwa chama kunatokana na kuchafuka kwa watu wake maana chama ni watu na bila watu hakuna chama. Chama si majengo, magari na vitu vingine. Unaweza ondoa vitu hivi vyote lakini chama kikaendelea kuwepo maadamu watu wake wapo. Lakini ukiondoa watu chama imeshakufa hata kama yatabaki Majengo, maofisi, magari na mali nyinginezo.
 
Natafakari kauli ya Makonda wakati akitangaza majina ya watuhumiwa wa dawa za kulevya kuwa yuko tayari "hata kupoteza Ukuu wa Mkoa". Nashindwa kung'amua. Je, inawezekana alishapata fununu za kuondolewa mapema akaamua kumtega Rais kwa kumuweka kwenye dilemma? Kwamba kama Rais angemuondoa baada ya kutaja majina angeonekana amemtosa Makonda kwa kuwagwaya wauza dawa za kulevya?
 
Rais Magufuli hawezi kumuondoa Mh Makonda ukuu wa mkoa kisa kuna kelele kwenye mitandao kuhusu vyeti.

Hilo tusilitegemee kutokea kwa utawala wa Rais Magufuli.

Sifa moja ya Rais Magufuli ni kumuamini mtu hasa anayeonesha njia kwake ni MTU muhimu sana kuliko hizo kelele.

Hizo ndiyo sifa za watu wenye personality ya Rais Magufuli.
 
Rais aongozi kwa fununu
 
Basi wasitishe na huo wanaoita ukaguzi wa vyeti na ajira feki!
 
... Hata hiki ulicholeta ni kelele pia hapa mtandaoni na yaweza kupuuzwa as well.
 
Basi wasitishe na huo wanaoita ukaguzi wa vyeti na ajira feki!
Vyeti vyake vilishakaguliwa na Utawala wa Rais mstaafu Kikwete na Rais Magufuli ndiyo maana yuko kazini mpaka sasa.

Wenye vyeti fake au vya kuazima hawako kazini Leo hii.

Mwenye ukweli na ushahidi wa taarifa hizo zinazosambaa mitandao ni si afungue kesi Mahakamani na mawakili wakujitolea wako wengi tu watasimamia kesi bila malipo maana ni wazalendo wa nchi.

Nashangaa Mch Gwajima kujitapa madhabahuni kuwa ana miliki vyeti vya watu ofisini kwake ambao hawamuhusu wala si waajiriwa wake.
 
Sasa kwanini mamlaka husika zisikanushe? Uongo ukiachwa huishia kuwa ukweli
 
kama anavyo na hakupata zero si apeleke sasa au aitishe mkutano na waandishi
 

Sawa, je na hili la kwenda kugawa ardhi aliyopewa na matapeli wanauhusishwa na kuuza dawa za kulevya imekaaje? Yeye kama mkuu wa mkoa alishindwaje kwenda kuiona wizara husika kupata uhakika wa umiliki wa ardhi? Sio mara moja au mbili anatuhuniwa kuhusu ushirikiano wake wenye mashaka na hiyo kampuni yenye mawaa. Hili unaliteteaje?
 
Sio kwa Bashite ninayemfahamu! Huyu kama angekuwa amesingiziwa angeishatoka hadharani muda mrefu na ushahidi wake mkononi kukanusha. Lakini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hata kabla ya kuona ushahidi ile namna tu ambavyo Bashite anatekeleza kazi zake ni ushahidi tosha kuwa kichwani hayuko sawa!
 

Avilete hadharani basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…