Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Mbunge wa hai katajwa km mtumiaji au muuzaji?!...sijaelewa vzr hapo
 


Kumekucha!!Ni siku nyingine tena,Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ataongea leo na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.

Mkuu wa Mkoa atakuwa mubashara Azam Tv mara ifikapo saa 05:00 asubuhi leo hii.

Tetesi ni kuwa,mkutano huo unaweza kuwa ni kujibu tuhuma za kuwa anawakabili "dagaa" na wakati "mapapa" wa biashara hiyo wapo.Na majibu ya mkuu wa mkoa yatakuwa ni kuwataja hao mapapa na kuelezea hatua zitakazochukuliwa...

Tega usikie....(Stay Tuned)

=======
UPDATE:
=======

Ameanza kwa Kumshukuru Rais wa Jamuhuri.

Paul Makonda asema anataka wauzaji wa dawa za kulevya wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha.

Paul Makonda asema vita vya dawa za kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani.

'Kuna watu nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa, unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa'-RC Makonda


'Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya'-RC Makonda

'Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia'-RC Makonda

'Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi-Makonda

'Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana- Makonda

'Watu wanafanya biashara za dawa za kulevya na meli zinazokuja na mafuta'-RC Makonda

'Kuna mama kazi yake ni kusafirisha watoto wa kike ambao wanapewa dawa za kulevya, wawili wako jela China na amewatelekeza'-RC Makonda

'Tukiendelea kuvutanavutana tutapoteza lengo la kupambana na dawa za kulevya'-RC Makonda

'Tukishindwa vita hii ya dawa za kulevya, hajashindwa Makonda au Rais Magufuli tumeshindwa wote'-Rais Makonda

'Tuko na majina 65, nitahitaji kukutana nao ijumaa, wako wanaosemekana wanatumia, wako wanasemekana wanazo taarifa zitakazotusaidia-Makonda

'Nawashukuru wenyeviti wa mitaa wameanza kuleta majina ya watu ambao wanawasiwasi nao kuhusu dawa za kulevya'-RC Malone's

'Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza'- RC Makonda

'Zile nyumba mnazozitilia shaka, hamuelewi hata kinachoendelea ni wajibu wetu wananchi kutoa taarifa na taarifa zitakuwa ni siri-RC Makonda

'Kuna ambao tuliwaita wako nje ya DSM, wapo waliotoa taarifa na watafika ila wapo waliokimbia tunawafuatilia na tutawapata wote'- RC Makonda

'Nawashukuru ndugu zangu walioko nchi mbalimbali kwa kunipigia simu na kunipa taarifa mbalimbali'-RC Makonda


Wapi kawataja Mbowe, Manji, Gwajima, etc?
 
nilijiuliza hili swali tokea mwanzo na nitaendelea kujiuliza mpaka pale nitakapopata majibu halisi. sidhani kama kuna mwenye dhamira ya kweli ya kupambana na uuzaji na utumiaji Wa dawa za kulevya Bali naona mwisho Wa hili tunaweza kushuhudia viongozi wengi Wa upinzani wakiishia Kuleeeeeeeeeee! huenda hii ni mbinu Moja wapo waliyoamua kuja Nayo. Muda utasema

Nadhani ndo maana wakaamua kumficha Tundu Lissu.
 
Makonda akwende ku update list yake kwa kuongeza jina la Masogange. Wanasema wahenga kuwa lisemwalo lipo. Akamhoji na huyo binti maana amekuwa akishutumiwa na watu wengi sana. Anakuwa mkali kama mbogo maslahi yake yakiguswa. Pia anatakiwa aje aseme amepata wapi utajiri alionao. Shutuma za mbunge Msukuma zinzhitaji majibu.
 
Hawa jamaa Tundu Lisu na Mbowe nilijua tu ni lazima wanauza na wanatumia Sembe!
Halafu walitaka tuwakabidhi nchi hawa wauwaji wa Vijana wetu? Yaani Mbowe na Tundu Lisu ndiyo wangekuwa Ikulu sasa hivi, hii Nchi kweli Mungu anatupenda!
Makonda hana ajualo ni mtupu kama aliyemuweka yaani kwa kufanya hivyo andhani ndio anapata sifa ndio maana wengi wanaamini anatumiwa kisawasawa
 
Freeman Aikael Mboweeee!

Nasikitika hata huko mtamkosa.Shida yenu ni kumuumiza na kuua CDM lakini chuki,visasi na ubaguzi havitajenga.

Madrug Lords wenyewe hata mmoja hajatajwa hapo.
 
Kwanini makonda hakumtaja hadharani huyo mama aliyedai ana maduka ya nguo??
 
Kwani huko "mawingu" alienda? Au matangazo yakirushwa na clouds basi yanafanyika clouds?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
kweli kabisa maana ukicheki pale kulikuwa na mic za station nyingi tuu za tv so kama wengine waliamua kurekodi ili wakahariri kwanza isiwe sababu ya kuwaandama mawingu tv
 
Mkoroshokigoli nishampongeza,wote nawapongeza kwa hii movie tunayowachezea!
Tunawapiga kotekote!
Mkija kushtuka,2019 hii hapa!
 
Back
Top Bottom