Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa mujibu wa televisheni ya Aljazeera ni kuwa upatanishi unaoendelea nchini Qattar uko katika hatua za mwisho kukamilika ili vita visimamishwe kwa haraka muda wowote kuanzia sasa.
Ijapokuwa mwanzoni Israel ilionekana isingeweza kabisa kusitisha vita kutokana na hasira za mashambulizi ya Hamas mnamo Okotba 7.Hata hivyo upinzani nje ya taifa hilo umezidi shinikizo la ndani la kutaka kulipiza kisasi kwa kuingia Gaza.
Marekani ambayo ilitoa kauli kali za kuiunga mkono Israel ndiyo ambayo imeanza kupata madhara zaidi nje ya Israel kuliko Israel yenyewe.
Nyundo ya mwisho kushinikiza kusitishwa kwa vita ni matamko ya leo ya viongozi wa Hamas ambao wamesema hawataendelea kuachia tena mateka wowote kabla kusitishwa kwa vita.