Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Hata hivyo, vita vya Syria haviishii tu kwenye mgogoro wa madhehebu. Kuna pia migogoro ya kijamii, kisiasa, na kijeshi inayochangia.Wanaukumbi hizi Imani za kumpigania Mungu zinaitesa Dunia, vita nyingi zinazohusisha vikundi vya kigaidi kama Hayat Tahrir al-sham inayoshusha kipondo kwa mashia ya Irani na Syria ni ya kidhehebu zaidi.
Hao wote ukiwauliza wanasema wanampigania Allah kwa kuwafuta makafiri.
Swali ninalojiuliza kwanini wampiganie Allah wakati yeye ndo muweza yote? Naamini kama muweza yote anaweza kujitetea mwenyewe pasi msaada wa wanadamu.
Sasa kwanini tuwe wasemaji na wahukumu kwa niaba yake? Yeye mwenyewe amekaa kimya hao uliwaita makafiri anawapa mvua,jua, chakula na mavazi na neema zingine tele wewe kiherehere chanini?
Nasemaje wote wanaoinua upanga kwa jina la Allah ni watu wenye Imani potofu hawana tofauti na wale wanao uwa walemavu wa ngozi kwa kisingizio cha kutaka utajiri.
Makundi ya kigaidi kama vile ISIS (Islamic State), ambayo ni kundi la wah radical wa Kisalafi, linashiriki vita hii kwa namna yake, likitaka kuanzisha utawala wake unaohusisha imani kali ya Kisalafi.
Pia, kuna migogoro kati ya koo, vikundi vya kabila, na maeneo ya kisiasa tofauti, ambayo inachangia mivutano zaidi.
Kabila la Alawite
Kabila la Alawite ambalo ndilo msingi wa utawala wa Bashar al-Assad. Ambalo wengi wao wanaishi maeneo ya pwani ya Syria, hasa Latakia na Tartus.
Wanaunda sehemu kubwa ya uongozi wa kijeshi na kisiasa wa serikali ya Assad. Wanapigana kubakiza utawala wa Assad madarakani, kwa hofu ya kulipiziwa kisasi.
Kabila la Suni Al Arab
Kabila hili ndilo wanalotoka Waislamu wa madhehebu ya Suni na ndio kundi kubwa zaidi la kidini na kikabila nchini Syria (takriban 74% ya watu).
Wamesambaa nchi nzima, hasa katika miji mikubwa kama Aleppo, Homs, na Daraa. Wengi wa wapinzani wa Assad wanatoka kundi hili, na wanapigania kuondoa serikali ya Assad ambayo wanahisi imewanyima haki kwa miongo mingi.
Pamoja na makabila mengine kama Wakurdi, Druze, Bedouin, Turkmen na hata Wakristo wa madhehebu tofauti kama Orthodox, Katoliki, na Assyrian, ambao wanapinga makundi ya Kiislam ya imani kali, hivyo kuunga mkono utawala wa Assad.
Ova