Vita inayoendelea Syria ipo kimadhehebu zaidi kati ya Suni na Shia

Hata hivyo, vita vya Syria haviishii tu kwenye mgogoro wa madhehebu. Kuna pia migogoro ya kijamii, kisiasa, na kijeshi inayochangia.

Makundi ya kigaidi kama vile ISIS (Islamic State), ambayo ni kundi la wah radical wa Kisalafi, linashiriki vita hii kwa namna yake, likitaka kuanzisha utawala wake unaohusisha imani kali ya Kisalafi.
Pia, kuna migogoro kati ya koo, vikundi vya kabila, na maeneo ya kisiasa tofauti, ambayo inachangia mivutano zaidi.

Kabila la Alawite
Kabila la Alawite ambalo ndilo msingi wa utawala wa Bashar al-Assad. Ambalo wengi wao wanaishi maeneo ya pwani ya Syria, hasa Latakia na Tartus.

Wanaunda sehemu kubwa ya uongozi wa kijeshi na kisiasa wa serikali ya Assad. Wanapigana kubakiza utawala wa Assad madarakani, kwa hofu ya kulipiziwa kisasi.

Kabila la Suni Al Arab
Kabila hili ndilo wanalotoka Waislamu wa madhehebu ya Suni na ndio kundi kubwa zaidi la kidini na kikabila nchini Syria (takriban 74% ya watu).

Wamesambaa nchi nzima, hasa katika miji mikubwa kama Aleppo, Homs, na Daraa. Wengi wa wapinzani wa Assad wanatoka kundi hili, na wanapigania kuondoa serikali ya Assad ambayo wanahisi imewanyima haki kwa miongo mingi.

Pamoja na makabila mengine kama Wakurdi, Druze, Bedouin, Turkmen na hata Wakristo wa madhehebu tofauti kama Orthodox, Katoliki, na Assyrian, ambao wanapinga makundi ya Kiislam ya imani kali, hivyo kuunga mkono utawala wa Assad.

Ova
 
Wale sio waislam ni magaidi yasiyo na dini, Uislam ni kama njia inayotumika kutimiza matakwa yao
Sisi huku Mapadre wakilawiti tunawaita Wakristo wakristo wenye dhambi.

Ila wenzetu mkitenda dhambi sio Muislamu. Inaonekana kila muumini ni Malaika huko hakuna anayetenda dhambi.

Njia sahihi ya kutatua tatizo ni kukubali kwanza tatizo lipo.
 
Israel inalengo zaid ya iyo vita wanataka Dunia akili zao zibaki Syria ilo yeye sasa akafanye mauwaji makubwa pale Gaza raia wawaswage mpakani na Misri lkn watu wapo macho sana. Zayuni akili ana.
Muumini atanyanyua bunduki ataua muumini mwenzake lawama atapewa Marekani na Myaudi.
 
Brother unachoshindwa kuelewa ni nini?

Syria yupo US, Turkey, Iran na Russia.

Haya tusaidie kufafanua kwa kutumia muktadha wa Uzi wako!
Mkuu unaweza kutueleza pale siria kuna nini kinachoyavutia hayo mataifa makubwa
 
M
MBUMBUMBU SOYO WAISLAMU NI WAARABU... The best quote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…