Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
Kuna vita mbaya sana ipo lakini watu hawajui, hii vita kati ya Jangili na Askari wa kulinda na kutunza Wanjama katika hifadhi za Wanyama.
Hii ni zaidi ya vita hawa wakigumiana hakuna majadiliano ni vyuma tu vinatembea. Kwa sisi tuliokulia Selou Game reserve tunajua hii vita.
Kuna siku tupo porini hatua chache kutoka pale lilipo treini ndani ya Selou tukakatiza sehemu kuna mti upo katikati ya barabara uligoma kutolewa.
Mbele tukagumiana na mvuvi haramu jamaa alijichochea kwenye bwawa lina mamba kibao nikauliza sasa itakuwaje mzee mmoja Ranger akanijibu hao ndio maadui zetu na huyo hawezi kuliwa na hao mambo Wandenge wanauchawi sana.
Tukaenda mbele mida ya usiku mwingi tukaona moto kwa mbali unawaka tukajichochea ile tumefika tu tukakuta jamaa walikuwa wanabanika samaki. Nikajisemea hii dunia kuna mtu anaogopa kutoka ubungo mpaka mbezi kwa miguu. Wakati kuna jangili anakatika selou usiku mwingi bila hofu.
Siku hiyo tukakosa mawindo yetu nilikuwa katika mafunzo kwa vitendo. Huyu mzee akaniambia humu ni msutuni kina NguruMbili ama makucha(Simba) na Abeid Mziba(Nyati mzee wa Vichwa) na binadamu Jangili mzee akasema bora ukutane na Wanyama kuliko Jangili. Akasisitiza ni vita kali ambayo haina kelele.