Vita kati ya majangili na askari wa hifadhi za wanyama pori

Vita kati ya majangili na askari wa hifadhi za wanyama pori

Uko sahihi tuliekaa karibu na mbuga au mapori ya akiba tujua Hilo
1. Ukikutwa na Kuni wewe ni jangingiri
2. Ukikutwa na mjusi wewe ni jangingiri
3. Ukikutwa na mbao ndio usiseme
Askari wanyama pori hawafai kuliko Askari yeyote Duniani nasema tena hawafaiiii
Ila majangili wanafaa, sio
 
Ila majangili wanafaa, sio
Majangili hawafai ila ninachokizungumzia hapa Ni mambo mawili
1. Kukomaliwa wasio na sifa za ujangili na wenye sifa kuachwa.
Mi najua maana nimekulia kwenye hizo sehemu
Yaani kushipaliwa mkata Kuni na meno ya tembo yanaondoka kiulaini

2. Hawa watu hawana ubinadamu kabisa yaani wanathamini zaidi mti kuliko binadamu
Sema mimi ni mvivu kuandika ningeandika mengi ya hawa jamaa
 
Hii vita ni kali, nimewahi ishi nao hawa askari wa wanyama pori huko Selous, japo tunawalaumu ni wakatili ila nikuambie kitu ukatili wao hawaufikii wa majangili, achana na mtu anayeitwa jangili dadeki, sema hao maaskari wakiuawa au kufanyiwa vitu vya kikatili havisemwi, narudia tena achana na mtu anayeitwa jangili..
 
Nyati msikie tu, bora ukitane na pride ya simba ila sio nyati nakumbuka miaka hiyo nilipokuwa nafanya tafiti katika mbuga ya Serengeti ile wakati wa kufanya darting kuna mzungu mmoja alikoswa koswa kupigwa pembe..
Dr Titus mstaafu mlenga shabaha ......
 
Bora Ukutane na Majambazi kuliko kukutana na Jangili huyu ameshazoea kuziona damu.

Ni sawa na Bora ukutane na Muuzaji Bucha ya nyama kuliko kukutana na Mtu wa machinjioni ya mifugo hawa nao wana roho ngumu kuna jamaa angu aliwahi kuchomwa kisu mguuni kikatokea chini kwenye sori ya kiatu
 
Yani natamanigi Sana mazali kama haya yakukutana na majangili porini huko tena usiku. Huo mkono nitakaoutembeza maamaeee nitaacha historia na alama ya kudumu. Asante mleta mada Lazima sasa hivi nizame chaka niitendee haki black belt yangu.
wale wasenge wanaoga sana mitishamba. ukiwashinda kwa bunduki,ngumi na mateke, wanakushinda kwa uchawi.

niliwahi kusimuliwa story kuhusu jangili mmoja mbobevu wa meno ya tembo.

unaambiwa dawa zake zilikuwa na uwezo wa kumfanya kuwa invisible mbele ya wanyama wakali. anaingia ndani ya kundi la tembo na ku- point tembo yupi wa kumdondosha.

ni kama tu vile mmasai anavyoingia kwenye zizi la ng'ombe kukagua mifugo yake.
 
Siku nafanya zangu boat na wageni ziwa manze pale selous mgeni akaona mtu kichakani kwa mbali,alivyonitonya kuchukua binocular nikaona njema kama tano hivi zimelala na gobole zao standby asee nileguza chap boat camp.
Sikukumbuka hata kama nina radio call
Baadae tukio hili lilikuja kuniletea tatizo pale kazini
Humu kuna watu wanasema tu hawajui maisha ya porini ni vita rasmi. tulikamata mzee ana miaka kama sikosei 75+ nikakaa nae chemba kumuuliza maswali akasema yeye maisha yake ni porini hajui lolote maishani mwake ni Jangili mbobezi. Nikatoa ushauri tumuachie tukansindikiza mpaka kijijini kwake.
 
Binafsi, nawapongeza sana Askari wa wanyamapori, ni jasiri mno!
Majangiri ni watu hatari sana! Hakuna tofauti na wale wanaojiita wapigania haki wa msituni wa hit & run.
Wamekomaa mno kuliko ngozi ya mamba.
Imagine, wanaweza kukaa hata miaka 5 msituni bila kuoga?
 
Mkuu inatokea kuna majangili wako vzr shabaha alafu unakuta wameanza kuwaona nyie wakiwakurupua lazima waangushe wawili watatu mkuu
Na majangili wanako waina mbili wenye silaha za moto na silaha sizizo na moto kama mshale ect
Kuna mkasa ule wa Mkuu wa Polisi Loliondo marehemu Kong'oa. Alienda mbugani nadhani ilikuwa Ngorongoro wakafanikiwa kukamata Majangili kumbe kuna wengine wamejificha kuna mmoja alikohoa jangili akainama mzee alifumuliwa gobore la kifuani. Ikabidi JWTZ waingie msituni. Jangili yeye anachojua ni kuwa kaingia vitani maisha yake kayakabidhi Wanyama na askari pori.
 
Kama sikosei mwishoni mwa miaka 90 hiyo alikuwa OCD. Ni kweli alikohoa. Majangili wa Ngorongoro walikuwa ni balaa hawafai. Sema nao waliuwawa sana.
 
Uko sahihi tuliekaa karibu na mbuga au mapori ya akiba tujua Hilo
1. Ukikutwa na Kuni wewe ni jangingiri
2. Ukikutwa na mjusi wewe ni jangingiri
3. Ukikutwa na mbao ndio usiseme
Askari wanyama pori hawafai kuliko Askari yeyote Duniani nasema tena hawafaiiii
Umesahau
Mkaa
Asali
Mizizi ya miti.
 
Ukikutwa na nyama ya swala ni uhujumu uchumi jela miaka mingi kweli??. Yaani Afrika, Arusha nyama ya swala ni kosa. Ndio maana hayati John Pombe aliwaita mabeberu, yaani sheria zao ziwe mpaka huku.
 
Yani natamanigi Sana mazali kama haya yakukutana na majangili porini huko tena usiku. Huo mkono nitakaoutembeza maamaeee nitaacha historia na alama ya kudumu. Asante mleta mada Lazima sasa hivi nizame chaka niitendee haki black belt yangu.
Oss black belt 🥋 ya mchezo gani Mkuu
 
Back
Top Bottom