Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 4,107
- 9,671
- Thread starter
- #61
Wale wanadai walikuwa Wasomali jeshi liliingilia kati walitembezewa kibano sana. Majangili hatari usije kuombea kukutana nayo ni hawa Wasomali na Warundi na Wanyarwanda ndugu wale ni vita. Kuna pori la katavi na kuna sehemu ya pori la Inyonga kwenye Mpung'o jangili anakatiza. Wameteka sana mabasi.Kama sikosei mwishoni mwa miaka 90 hiyo alikuwa OCD. Ni kweli alikohoa. Majangili wa Ngorongoro walikuwa ni balaa hawafai. Sema nao waliuwawa sana.
Kuna wakati serikali walikuwa wanalia na wizi wa nyaya za simu zote zilikuwa zinaishia porini mikononi mwa jangili. Niliamua kuachana na maisha ya msituni yana raha na kero ni kubwa. Kuna siku tulikuta tent la Watalii mzee Tembo kalichakaza vibaya kumbe ndani walibeba Maepo.