Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Israel tangu kuundwa kwake limekuwa ni taifa hatari sana kwa usalama wa wenyeji waliowakuta na usalama wa majirani zake wote na hata kwa ulimwengu mzima.
Taifa hilo linaongoza kwa kupinga maazimio ya umoja wa mataifa na hata kuvunja mikataba inayowekeana na majirani zao.
Kwa ujumla ni taifa ambalo limepata nguvu sana kwa kufanya mambo haramu.Ina silaha kali aina zote ikiwemo nyuklia na huwa haiogopi kutumia silaha yoyote iliyonayo hata ikiwa inapambana na warusha mawe na haijali iwapo silaha zake hizo zitauwa wakubwa ama wadogo.
Pamoja na silaha hizo kali na vita,Israel ina silaha nyengine za kimya kimya katika kufikia malengo yake,lengo kuu ikiwa ni kumaliza kabisa kelele za kuwepo taifa la wapalestina.
Jumla ya maazimio yanayoihusu Israel na Palestina yapo zaidi ya 200.Kati ya hayo lipo azimio namba 2334 la mwaka (2016) linalohusu kutokuyavunja majumba ya wapalestina na kujenga maeneo hayo majumba mengine kwa ajili ya mayahudi.Kinyume chake tangu kupitishwa kwa azimio hilo ndio kasi ya kuvunja na kujenga imeongezeka.
Kuna maazimio ambayo Israel huwa inayavunja tu kibabe kama hilo hapo juu lakini bado kuna mengine huwa inayavunja kwa kutumia mbinu za kimya kimya na kifisadi ikiwemo hayo maazimio yanayohusu makazi ya wapalestina.
Kwanza Israel hujifanya ni nchi ya sheria sana na kwamba kila unachokifanya ni lazima upate kibali.Lakini sheria hizi huwa zinakusudiwa ni kwa ajili ya kuwakandamiza wapalestina peke yao.Kila anachotaka kukifanya mpalestina lazima aombe kibali.Tatizo kibali huwa hakitolewe kwa mpalestina yoyote na hutolewa kwa waisrael wengine peke yao.
Mtindo wa nenda uje kesho hutumika mpaka mwisho.Mpalestina yoyote akiamua kufanya kitu kwa kuchoka kusubiri kibali, huwa ni kibali kingine kwa mamlaka za Israel cha kuvunja na kuvuruga eneo lote na kufukuzwa pale alipo.
Moja ya aina ya vibali anachotakiwa kukiomba mpalestina na anakikosa ni kujenga au kuzibua mifumo ya maji taka.Kutokana na kukosekana kwa kibali hicho maeneo ya wapalestina yanakuwa ni machafu na kusababisha matatizo ya kiafya kwa wapalestina.
Mvua inaponyesha pia wapalestina huwa wanazuiwa kukinga maji hayo na kuyatumia ikitajwa maji ya mvua ni mali ya Israel.
Wapalestina wanaoishi pembezoni mwa bahari huwa hawaruhusiwi kuvua samaki bila kibali na wakienda baharini huwa si salama kwao kwani wanauliwa muda wowote kwa shabaha za aina mbali mbali.
Vibali hivyo vya uvuvi kinyume chake hutolewa kwa wavuvi wa kiyahudi peke yao ambao huvua mbele ya macho ya wapalestina.
Kwa mujibu wa mtaalamu mmoja wa Israel amesema nchi hiyo ina ukoloni wa kiarchitecture,kwamba ramani iko tayari ya kila kitu kinachotakiwa kujengwa kwenye maeneo walipo wapalestina wakianzia na maeneo yote yenye vyanzo vya maji na ardhi nzuri ya kilimo pamoja na maeneo yenye miinuko.
Kila majengo mapya yanayojengwa huwa yanatenganishwa na kuta au seng'enge nzito kiasi kwamba wapalestina waliokuwa majirani huwa wanaonana kwa macho tu lakini hawawezi tena kutembeleana