Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Gaza ikiwa ni kama gereza la wazi la muda mrefu imefungiwa na kila kitu kuingia humo chini ya uangalizi wa Israel.Hata mawasiliano pia lazima yapitie Israel.
Mara Israel ilipoamua kuingiza askari wa miguu wakiongozwa na vifaru ilijua ingepata hasara kubwa ambazo wasingependa zijulikane na raia wake.Kwa hali hiyo ikaamua kuzima mawasiliano ndani ya Gaza.
Baada ya mashirika ya misaada kulalamika mawasiliano yakarudishwa lakini yakiambatana na taarifa za kivita kutoka kwa wanamgambo wa Hamas wakionesha namna walivyokuwa wakiwaua na kutia hasara jeshi la Israel.
Israel ikaamua kuzima tena mawasiliano hasa ya intanet ambayo yanazifanya akaunti za mitandao ya kijamii za Hamas kuripoti vita moja kwa moja na kuangaliwa ulimwengu mzima.
Israel ikaamua kuzima tena mawasiliano hayo na hasa kuzinyima mafuta ya kuendesha majenereta minara karibu yote ya Gaza.Hapo Ellon Musk akajitokeza kutaka kuwaunganisha watu wa Gaza na intaneneti yake ya star Link.Hata hivyo akakaripiwa na Israel na kunywea.
Hapo ilikuwa ni katikati ya vita ambapo watu wanakufa kwa mamia kwa siku moja na majengo kuporomoshwa.Kuhamanika kwa ndugu za wapalestina walio nje ya Gaza kukaongezeka sana pamoja na malalamiko ya mashirika ya misaada na vyombo vya habari.
El Helbawi ni mwandishi na mwanaharakati wa kimisri ambaye kwa kutaka kujua zaidi hali za ndugu zake walioko Gaza alitafuta mawazo kwenye akaunti zake za mitandoa ya kijamii na mara akaletewa fikra ya kununua kadi za simu za kimataifa na awatumie walioko Gaza.
Akanunua moja na kuirusha kwa mwandishi mmoja aliyekuweko Gaza ambaye aliipokea na kuiwasha.Ilipoonekana kurusha mawasiliano ndipo wanaharakati wengi duniani wakaendelea kununua kadi hizo ambazo ni ghali na kumrushia El Helbawi.
El hebrawi aliendelea kuzirusha tena Gaza na watu kugawiyana na ndipo wigo wa mawasiliano ukaongezeka ambao uliifanya Israel ishindwe kuzima mawasilaiano hayo na ishindwe kuficha kile kilichokuwa kikiendelea
Gaza na kilichokuwa kikiwapata kutoka kwa Hamas.