Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Point of correction Bunazi wala kyaka hakuna makaburi kaburi lipo moja Kwabwoba!kabla ya kufika mtukula.
 
Siyo tanzania sema duniani kote Usishindane na nchi ndani ya nchi vatican inanguvu sana inabalozi ulimwenguni kote hivyo siyo jambo lakushangaza hadi ndani saudia kuna ubalozi wa vatikan sasa wewe utapoteza muda kupinga ukatoliki
 
Vita ilikuwa ya ulazima kwani Amin alijua Tanzania awamuwezi kwakuwa alikuwa na vifaa vya kivita kuliko sisi!nakwakuwa alidhamilia kuchukua kagera yote vita ilikuwa aihepukiki!
Wanajeshi wote na Wananchi wa Uganda walikuwa upande wa Watanzania, hawakumtaka kabisa Idd Amin, walikuwa tayari kumuoverthrown na walishaanza huko kwao.

Idd Amin hakuwa na silaha za kutisha, baada ya vita kuanza ndio akapata support ya Ghadaffi kutoka Libya.
 
Mkuu nakufatilia kuanzia mwanzo kijografia inawezekana kagera iliyokuwa imetekwa uifahamu vizuri tukianzia kwakyaka hadi mtukura hakuna mlima eneo la nsunga kuna kamuinuko kidogo hivyo wakati wa vita kuikomboa kagera tanzania ilikuwa ikituma mashambulizi kutokea kashaba katika muinoka ya hapo pale ilikuwepo brigedi yatembo kutoka songea brigedi iliyofanya kazi kumuondoa Iddi Amin kyaka ni brigedi ya mbuni.......tuendelee
 
 
Amin alikuwa mshenzi sana ujui unatetea uislamu lakini hata wewe unayemtetea ungengia anga zake na pensi yako angekufyekelea mbali sioni unachotetea kwa Iddi amin Dada
 
Amin alionekana ni threaten kwa tanzania hivyoa lazima umtoe kwa maslahi mapana ya taifa kama ujui hilo.
 
Vita hiyo tulipoteza sana kuliko faida tuliyopata Watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili mbovu za chadema eti tipoteza zaidi kuliko faida kama siyo hiyo vita tz tungekuwa kama DRC maana hata vinchi vidogo kama Rwanda na Burundi na malawi vilikuwa vinaleta chokochoko pamoja na Kenya ndiyo ilikuwa inatumiwa kabisa na mabeberu ila baada ya kuona kile jwtz imemfanyia idiamini wakagundua tz siyo nchi ya kuichokonoa wakakoma kabisa hiyo ni faida kubwa sana wewe unadhani DRC ina sumbuliwa na vinchi hadi vidogo kwa sababu gani ?
 

Mzee Kichuguu anakataa sources zote juu ya hili suala utadhani yeye alikuwa na taarifa zote za mapambano kitu ambacho si kweli

Sources zangu juu ya uwepo wa askari wa Msumbiji ni

1. Afande waliopigana nao msitari wa mbele bega kwa bega kumpiga Amin

2.Kitabu cha Waandishi wa habari wawili, waandishi pekee kutoka nje waliopewa press clearance kusonga na majeshi yetu kucover operesheni za jeshi letu huko msitari wa mbele, na kitabu chao kilichapwa nchini na kilipata ridhaa za uchapaji na serikali yetu, laiti hilo suala wangekuwa wamedanganya, wangeambiwa walifute

3. Kuna secondary sources, nimeweka hadi gazeti la New York Times la mwaka 1982

Mzee Kichuguu hizi sources zoooote hazitaki, anataka za kwake tu, mtu ambaye kwanza hakuwa msitari wa mbele.

Hata kama alikuwa COMM, hii haimaanishi alikuwa anajua kila kitu cha msitari wa mbele!
 
Nikiwa eneo la vita vita ilianza siku ya jumanne tarehe 4 october 1978 tukiwashule tuliona TPDF Wakifanya mobilization tukawa atuelewi siku ya Alhamis tukatangaziwa kusitisha masomo siku hiyo hiyo ndege za kivita zikaja kushambulia zikafukuzwa moja ikapigwa ikaenda inawaka moto!! siku iliyofuata ijumaa kama saa kumi ilikuja ndege kuangusha mabomu zilikuwa ndege nne kufika maeneo ya bunazi zikatunguliwa moja ikaanguka pale bunazi nyingine inaenda inafuka moshi kwenye pori la minziro mbili zikarudi!Uganda siku ya jumamosi sasa ikajulikana kuwa tumevamiwa kama nchi ila sasa jumapili tuliambiwa sasa tuondoke majumbani ili kuokoa maisha yetu!
 
Labda tuache kabisa habaria za maisha yake ya binafsi; ila ni kuwa alikuwa Anglican. Ili kuthibitisha dini yake ongea na binti yake Lilliane; haongei kiingereza vizuri lakini mawasiliano yanakwenda tu.
Kingine nilichojifunza kutoka kwako mzee wetu ni kwamba pamoja na mtu kuwa anakujibu kwa kukutest na kebehi, lakini wewe umekuwa ukimjibu kwa hekima na kumpa elimu juu yake tena bure kabisa. Ubarikwe sana.
 
brooh izo mnazosema eti ilkua siri tena siri ya kijeshi nyie mmeijulia wapi?

baada ya ku mobilise jesh almost tulimzidi ug ×3
askari walitoka majeshi yoye magereza polisi jkt jwtz hadi uamiaji walitoa askari bado mgambo na bado wangine wakujitolea walipokea mafunzo ya muda mfupi

bado sioni kwa nini tuombe msaada wa askari nje!
kama ni wataalam tulkua nao
wakutosha jeshi letu lilelewa na canada na uk kabla ya mchina!! walikuapo wataalam wengi tu walopata mafunzo kwe vyuo vikubwa vya nje!!
ilo la msumbiji kutoa askari ni NO!
vita ni propaganda na hatukutaka kujali propaganda kama amini wakati ule maana propaganda hazina msaada sana kwe uwanja wa medani..

hizo source zako zinawalakini..maana waliandika kwa kusikiliza pande zote ug na tz sasa jiongeze nani ni sahihi? pia sio kila askari anajua kilichokua sahihi...sometyms hapakosi uvumi mnapokua kwe kazi kama hiyo!
kama unataka taarifa za kukusatisfy nenda mmj pale utasaidiwa lakini kwakutegemea tuu vyanzo vyako utapagawa zaidi

tz ni nchi ya kijamaa lakini pia
ktk mambo ya security kuna ka msemo "jifanye weak kumshinda adui yako sasa unajifanyaje kua weak? usiri ni kitu cha muhimu sana
unadhani serkali haijui historia ya vita hii imechezewa?
je unafkiri covd19 tuliishinda kwa nguvu za mwenyezi?
mambo mangine ni= unapoteza tuu muda maana hutakaa uyajue kamwe.
 

Jeshi si wingi wa Askari tu bali kuna aina fulani fulani za askari unaweza kuwahitaji, kwa mfano kama wewe jeshi lako limezoea kupigana Msituni, unaweza kuhitaji askari wenye uzoefu wa kupigana Jangwani. Unaweza kuhitaji aina fulani ya makomando, unaweza kuhitaji aina fulani ya askari wa kuoperate vifaa fulanifulani

Hata Marekani pamoja na ukubwa wa Jeshi lake huwa anapenda kufanya alliances na washirika wake kwenye vita zake.
Sisi ya kwetu pamoja na mambo mengine, ilikuwa pia ni Shukrani ya Samora Machel kwetu baada ya sisi kuwa ni wenye kumsaidia kwenye vita yao ya uhuru.

Wasumbiji walikuwa na uzoefu mkubwa sana wa mapambano ya msituni kwa sababu walipigana muda mrefu dhidi ya wareno.

Na kwa taarifa nilizonazo walifanya kazi nzuri kuunguurumisha zile BM
 
auwezi ukawa upo serious we jamaa ila poa!!

rudia tena kusoma nilicho kiandika

nakumbuka baada ya kichapo kumzidia dada amini aliitangazia dunia tumeingiza
mamluki kutoka ussr mara mozambiq izo zote zilkua story tuu
sie tunakapenda kale ka msemo cha jifanye weak ili kumshinda adui yako
in shot amini alitudharau yani alitomba moto bila kujua
 
Najua wewe unasisisistiza kuwa watanzania hatukuwa na uwezo wa kupigana mpaka tuliposaidwa na msumbiji ambao ni sisi ndio tuliokuwa tunawafundisha. Una psychological effect fulani inayoitwa "confirmation bias" yaani tayari unaamini kuwa Tanzania hatuna uwezo, na unachohitaji ni habari yoyote itakoingia kwenye bias yako na kufanya kuwa ndio ukweli wote badala ya kukubali ukweli kamili ambao hauingii kwene bias yako. Sasa hivi unaamini ya kusimuliwa na watu waliosimuliwa na watu waliodhani kuwa tulisaidiwa na msumbiji; sisi tuliokuwa ndani ya jeshi one-to-one tunapokuambia ukweli unaukataa kwa madai ilikuwa ni siri ambayo hawa wanajeshi tusingejua.
 
mkuu naona kama umeenda mbali, hata mimi nnachojua marafiki walituunha mkono, msumbiji walitoa watu hiyo haina maana kwamba jeshi letu halikuweza kusimama lenyewe

Sent from my BLL-L21 using JamiiForums mobile app
 
mkuu naona kama umeenda mbali, hata mimi nnachojua marafiki walituunha mkono, msumbiji walitoa watu hiyo haina maana kwamba jeshi letu halikuweza kusimama lenyewe

Sent from my BLL-L21 using JamiiForums mobile app
Na wewe unaamini kuwa tulipata askari wa Msumbiji wote wakarudi kwao wote wazima bila kufa au kujeruhiwa. Kama walikuja kusaidia kazi nyingine za ulinzi wa ndani na logistics, hiyo inawezekana lakini siyo kuja kwa ajili ya frontline combat kwa sababu nilizosema. Jeshi ilikuwa na commands ambazo zilikuwa established kivita na uongozi majenerali hadi maluteni kanali. Kila aneyetetea hakusaidiwa na msumbiji vitani haji na ushahidi kuwa waliongozwa na kamanda gani; ndiyo maana inakuwa ni hearsay tupu. Katika vita unaposema jeshi unaanza na kamanda; huwezi kusema idadi ya watu tu.
 
Amin alikuwa mshenzi sana ujui unatetea uislamu lakini hata wewe unayemtetea ungengia anga zake na pensi yako angekufyekelea mbali sioni unachotetea kwa Iddi amin Dada

Mshenzi kuliko Nyerere?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…