Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Vita ya kiduwanzi.
ikasababisha Kenya watupite uchumi hadi kesho! Qmamae
 
Hizi ni propaganda tu ili kufunika kombe.... Anyway wewe ni mzalendo.

Kama Mwl asingewaruhusu kina Okello, M7 kutumia ardhi ya Tz kuendesha uasi wa silaha dhidi ya Uganda, basi Iddi Amin asingepata sababu ya kuanzisha Vita na Tz.
 
Allah amlaze mahala pema peponi ndugu yetu Idi amin, bila kumsahau Ndugu yetu na kipenzi cha waafrika kwa ujumla Muammar Gaddafi, Allah amlaze mahala pema peponi!
Mh!...umewapenda sababu ya imani yao tu. ..hakuna jingine
 
akikuelewa ntashukuru sana!!!
 
Hizi ni propaganda tu ili kufunika kombe.... Anyway wewe ni mzalendo.

Kama Mwl asingewaruhusu kina Okello, M7 kutumia ardhi ya Tz kuendesha uasi wa silaha dhidi ya Uganda, basi Iddi Amin asingepata sababu ya kuanzisha Vita na Tz.
akina okelo na m7 ni wa juzijuzi tu, uhasama hasa ulianza baada ya amin kumpindua obote na mwl. kumpa hifadhi obote hapa tz. lakini amini alipoanza ku purge wafuasi wa obote kwa kuwauwa wengi walikimbilia tz kumfuata obote na walikuwemo wanajeshi pia,1972 kundi hilo lilijaribu kumpindua amin kwa kuvamia uganda kutokea tz. walishindwa vibaya. amin ali litariate akaipiga bukoba kwa mabomu na pia akadai mpaka halisi wa uganda na tz ni mto kagera pale darajani pale.
 
Hizi ni propaganda tu ili kufunika kombe.... Anyway wewe ni mzalendo.

Kama Mwl asingewaruhusu kina Okello, M7 kutumia ardhi ya Tz kuendesha uasi wa silaha dhidi ya Uganda, basi Iddi Amin asingepata sababu ya kuanzisha Vita na Tz.
Mkuu, unafahamu vitu hivi?

1. Hifadhi ya kisiasa
Sasa hao kina Okello, M7 n.k walipatiwa hifadhi ya kisiasa na inaruhusiwa kabisa. So kwa TZ kuwapa hifadhi hao viongozi lilikua ni jambo chanya tu.

2. Ukivusha majeshi ya taifa lako yakaingia kwenye nchi nyingine kushambulia, tayari unakua umefanya uvamizi dhidi ya nchi hiyo. Majeshi ya uganda yalivuka mpaka yakaingia Tanzania na kushambulia Kagera. Ulitegemea Jeshi letu litulie?

Sasa weka ushabiki pembeni vaa viatu vya Hayati Baba wa Taifa, ambae alikua ni Amiri Jeshi Mkuu wa wakati huo. Je wewe ndio ungekua Rais wa TZ wakati huo nchi imeshambuliwa Kivita, ungefanya nini? Kama Amiri Jeshi Mkuu.
 
Hifadhi ya kisiasa
Sasa hao kina Okello, M7 n.k walipatiwa hifadhi ya kisiasa na inaruhusiwa kabisa. So kwa TZ kuwapa hifadhi hao viongozi lilikua ni jambo chanya tu.
Hao jamaa walitumia ardhi ya Tz kushambulia Uganda.....hiyo huwezi kuiita ni hifadhi ya kisiasa labda uite ni kuunga mkono uasi.

Ukivusha majeshi ya taifa lako yakaingia kwenye nchi nyingine kushambulia, tayari unakua umefanya uvamizi dhidi ya nchi hiyo. Majeshi ya uganda yalivuka mpaka yakaingia Tanzania na kushambulia Kagera. Ulitegemea Jeshi letu litulie?
Sababu ya uvamizi ilikuwa ni nini?
 
Hao jamaa walitumia ardhi ya Tz kushambulia Uganda.....hiyo huwezi kuiita ni hifadhi ya kisiasa labda uite ni kuunga mkono uasi.
Hao jamaa walikua Jeshi la TZ? Kwanini amini avushe Jeshi la Uganda kuja kuishambulia TZ mkoa wa Kagera na kusema Kagera ni ardhi ya Uganda na kuunda mpaka mpya ambao si halali?

Sababu ya uvamizi ilikuwa ni nini?
Kwa mujibu wa Amini alisema mwenyewe Kagera ni sehemu ya Uganda baada ya kuvamia. Hivyo kwa Quote hiyo bila shaka alivamia ili kuitawala Kagera kama sehemu ya Uganda.
 
Hao jamaa walikua Jeshi la TZ? Kwanini amini avushe Jeshi la Uganda kuja kuishambulia TZ mkoa wa Kagera na kusema Kagera ni ardhi ya Uganda na kuunda mpaka mpya ambao si halali?
Kwanini muwafuge watu wanaotumia ardhi yenu kushambulia nchi nyingine?
 
Utadeal nao vipi? Wakati wapo nchi nyingine wamefichwa huko?

Marekani alideal vipi na Alqaeda (Osama na wenzake) waliokuwa wamefichwa Afghanistan?
Deal kwa njia za diplomasia, ikibid piga ambush kwenye camp yao tu kama alivyofanya USA alivyodeal na Alqaida. Je ulisikia USA kasema sehemu ya nchi nyingine ni yake kimabavu?.

Lakini sio kama Amin alivyofanya, kwa kuvusha Jeshi kuvamia nchi yetu na kuteka sehemu ya ardhi ya kagera na kusema hadharani kuwa hiyo sehemu ya ardhi ni ya Uganda.
 
Unaandika mavi tu!

Mshikaji anakupiga na point za maana wewe unajibu UHARO
 
Unaandika mavi tu!

Mshikaji anakupiga na point za maana wewe unajibu UHARO
Mkuu, kwani wewe ungekua Rais wa wakati huo wa TZ ungefanya maamuzi gani? Nchi yako imevamiwa ardhi ya kagera inatangazwa ni sehemu ya Uganda na mpaka mpya unatangazwa kinyume na sheria. Wewe ungefanyaje?
 
Baada ya diplomasia kufeli, USA alideal na Alqaeda kwa kuivamia Afghanistan na kuwaondoa Taleban au umesahau.

Hayo ya kuvamia Kagera ni kweli....ila naomba soma kuhusu jamaa anaitwa 'Juma Butabika'....huyu alikuwa Luteni Kanali wa jeshi la Amin......huyu jamaa ndiye aliyeamuru Tz ivamiwe kwa kuanzisha chokochoko mpakani bila Amin kujua na hatimaye kupelekea vita.....jaribu kusoma habari zake kwenye mtandao
 
Baada ya diplomasia kufeli, USA alideal na Alqaeda kwa kuivamia Afghanistan na kuwaondoa Taleban au umesahau
Ndio hii njia niliosema, ikibidi fanya Ambush kwenye camps zao tu. Ndio alichokifanya USA. USA hakuivamia Afghanistan na kutangaza sehemu ya ardhi ya Afghanistan kuwa ni ardhi ya USA kimabavu. Bali alifanya Ambush kwenye camps za Alqaida na Taleban. Au uliwahi kusikia USA katangaza sehemu ya ardhi ya Afghanistani ya kwake?

Hayo ya kuvamia Kagera ni kweli....ila naomba soma kuhusu jamaa anaitwa 'Juma Butabika'....huyu alikuwa Luteni Kanali wa jeshi la Amin......huyu jamaa ndiye aliyeamuru Tz ivamiwe na hatimaye kupelekea vita.....jaribu kusoma habari zake kwenye mtandao
Kiutaratibu hakuna Luteni anayeweza kuamuru Jeshi kuvuka mpaka kuingia nchi nyingine kufanya uvamizi bila ya kuwa na Approval ya wakuu wake. Ndio maana baada ya uvamizi wa kagera Rais Amin alizuru kagera na kutangaza rasmi eneo hilo kuwa ni la Uganda, hiyo inamaanisha hiyo Operation kivita aliitambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…