Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Mkuu, kwani wewe ungekua Rais wa wakati huo wa TZ ungefanya maamuzi gani? Nchi yako imevamiwa ardhi ya kagera inatangazwa ni sehemu ya Uganda na mpaka mpya unatangazwa kinyume na sheria. Wewe ungefanyaje?
Kwanini in the first place ufuge majambazi wa jirani yako sebuleni kwako?

Kwanini usiwatimue (kina M7, Okello) na kuwaambia jamani nawafukuza ondokeni sitaki shari na majirani zangu
 
Na Mseveni alikua Mwl chuo cha Ushirika Moshi

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Vita ya kiduwanzi.
ikasababisha Kenya watupite uchumi hadi kesho! Qmamae
Tangu 1967,Nchi ya Kenya ilikuwa mbele kiuchumi zaidi ya Tanzania.
Kwa hiyo sio kweli kwamba vita ya kagera ndiyo chanzo cha Kenya kuwa mbele kiuchumi.
 
Hizi ni propaganda tu ili kufunika kombe.... Anyway wewe ni mzalendo.

Kama Mwl asingewaruhusu kina Okello, M7 kutumia ardhi ya Tz kuendesha uasi wa silaha dhidi ya Uganda, basi Iddi Amin asingepata sababu ya kuanzisha Vita na Tz.
Ukikumbuka ushiriki wa Tanzania kuzikomboa baadhi ya nchi ( Mozambique, Zimbabwe, Angola, Namibia na vyama vya ukombozi vya Africa kusini)
Nchi ya Malawi chini ya Banda Kamuzu iliandaliwa kuwa chokochoko maeneo ya kusini mwa Tanzania.
Kilichofuatia ni kumshawishi Amin aanze vurugu.
Kwa hiyo nchi ikawa ina ukosefu wa Amani kusini na Kaskazini.
Vita ya kagera ndivyo ilivyo anza.
 
Mojawapo ya upungufu mkubwa wa nchi yetu ni kutowaruhusu watu walioshuhudia matukio muhimu ya kihistoria kuandika vitabu. Watu wengi walioshuhudia matukio muhimu wamefariki bila kacha taarifa muhimu. PhD yangu ni ya mambo ya vita na nilishawwishika sana kuandika kuhusu vita ya Kagera (mtazamo wa Tanzania) lakini Mwalimu wangu akanionya kuwa ningepata shida kupata taarifa. Ombi langu kwako ni kuhakikisha unaandika kitabu, kinafungiwa sehemu na watoto wako wakichapishe baada ya kifo chako.
 
Kwanini in the first place ufuge majambazi wa jirani yako sebuleni kwako?

Kwanini usiwatimue (kina M7, Okello) na kuwaambia jamani nawafukuza ondokeni sitaki shari na majirani zangu
Haujanijibu swali Mkuu
 
Kwanini asingedeal na hao watu? Yeye akaishambulia TZ mkoa wa kagera na kuutawala kimabavu kwa muda na kusema ni sehemu ya uganda. Je ni nchi gani duniani ingekubali sehemu ya ardhi yake kutekwa kimabavu?
Si alideal nao kwa kutuma jeshi lake nchini. Alifanya retaliation ya aggression tuliyokuwa nayo. Na retaliation mara nyingi haiwi na sababu halisi.

UN General Assembly Resolution 2624 ya mwaka 1970 inazuia kuwapa silaha au kuwasadia waasi wa nchi nyingine, hata magaidi. Tanzania tulikuwa na kiherehere na kisebusebu bila faida, ni upuuzi kuingilia maswala ya wenzako hasa kama uchumi wako ni wa kutembeza mabakuli. Hata Marekani iliingilia suala la Afghanistan na imetumia gharama kubwa sana.

Mwanzo tu tulikuwa wajinga, eti Obote amekuja kupewa hifadhi Tanzania nchi jirani na kwake. Hiyo diplomasia ya wapi? Zine Al-Abidine ben Ali wa Tunisia alikimbilia Saudi Arabia wala hakwenda Libya au Misri kwa majirani, hiyo ndio political asylum ya top leader inatakiwa kuwa. Leo hii Tanzania tumpe hifadhi mkuu wa inteligence service ya Rwanda unadhani inaleta picha gani.
 
Mkuu, Jeshi la Uganda lilivuka mpaka wa Tanzania na kushambulia kagera, kutangaza mpaka mpya kinyume na sheria na kutangaza kuwa sehemu hiyo ya kagera ni ardhi ya Uganda. Je wewe kama ungekua Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania wa wakati huo ungefanya maamuzi gani?
 
Mimi kama amiri jeshi ningeshambulia Uganda na kuirudisha kwao kisha na kufanya assesment kama Uganda inaweza leta tafrani tena, kama ndio ningeingia mpaka kumtoa Amini na kama sio ningeishia kuwarudisha kwao.

Je kama wewe ni mwanausalama wa Uganda na jeshi la Tanzania linawapa silaha, makazi na mafunzo waasi wanaokuja kumshambulia rais wako ungefanyaje? Unajua mediation iliyofanywa na Siad Bare Rais wa Somalia na katibu mkuu wa UN, Ngo Ekangaki ilivyotukuta na hatia. Upuuzi na kiherehere tulikuwa nao
 
Mimi kama amiri jeshi ningeshambulia Uganda na kuirudisha kwao kisha na kufanya assesment kama Uganda inaweza leta tafrani tena, kama ndio ningeingia mpaka kumtoa Amini na kama sio ningeishia kuwarudisha kwao.
Sasa hii ndio Kitu kilochofanyika majeshi ya Uganda yaliondoshwa Kagera, ikafanyika assesment na kuona kuna ulazima wa kuendelea kupigana vita na kumtoa kabisa Amini.


Moja, Kumbuka wale hawakua waasi kama unavyosema bali ni jeshi la Uganda lililokua na utii kwa Rais aliyepinduliwa na Amini. Ukisema wale walikua waasi nakushangaa sana. Wale walikua ni wanajeshi kamili waliokataa kuwa vibaraka.

Pili, una uthibitisho gani kwamba Jeshi la TZ liliwapa silaha?

Jeshi la Tanzania linawezaje kuwapa mafunzo Jeshi ambalo ni kamili la Uganda? Au unafikiri hao walikua mgambo?

Kuhusu makazi hao wote walikua wamepatiwa hifadhi ya kisiasa jambo ambalo linaruhusiwa kabisa. Hao walikua ukimbizini Tanzania.
 
Sasa unabishana na Yoweri Museveni aliyesema mwenyewe kwamba walipewa silaha na mafunzo?

Na hicho kiherehere cha kusema walikuwa jeshi halali nani kakupa. Nchi yako haina uwezo wa kujenga vyoo, mnakunya kwa msaada wa wazungu alafu bado unashobokea masuala ya nje. Yaani mtu mkeo na wanao wanakushinda kutunza na kuongoza, tena unaleta na wa jirani yako
 
Walipewa silaha wakati gani? Wakati wa vita vilipoanza rasmi ni kweli baadhi ya wanajeshi wa Uganda waliokua watiifu kwa Obote walijoin ili nao wapambane kumtoa Amini.

Kuhusu mafunzo ni kweli baadhi ya makamanda wengi wamewahi kupata mafunzo hapa TZ, kama Museven n.k kabla hata ya vita ya kagera.

Hao wakimbizi wa vita kutoka uganda baada ya mapinduzi ya Amin unafikiri walipenda wawe hivyo?

Ukweli utabaki ya kwamba ile vita ilikua ni lazima Tanzania ipigane ili kulinda heshima na ardhi ya nchi yetu, kutokana na uvamizi uliofanywa na majeshi ya Amin mkoani kagera.
 
Shusha madini mkuu
 
Tatizo halikuanza kwenye ile vita hapa tunatafuta justification for war. Huwezi mchukua mtu aliyehasi au aliyeondolewa pale Rwanda au Uganda leo ukampa hifadhi Tanzania alafu ukapanga watu wake wakamshambulie Rais wa nchi yake wakati huo no matter yuko kikatiba au vinginevyo.

Unahisi walioasi Rwanda wakaenda South Africa ni wapumbavu, au unahisi Wakenya wenye makosa ya uhaini waliorudishwa kwao tulikosea? Hakuna nchi inafanya upumbavu kama huo, sisi eti kisa Nyerere na Obote walikuwa marafiki
 
Mpe mfano mdogo kwenye familia yake,mwanaume mmoja wa kawaida anaingia ndani kwako anampiga mke wake na watoto wake ,angefanyaje
 
Mkuu, nakukumbusha tena wale hawakuhasi bali walipinduliwa na kukimbilia ukimbizini sehemu mbalimbali ikiwemo TZ, na si kosa nchi yoyote duniani kutoa hifadhi ya kisiasa au ya ukimbizi. Kama una ushahidi kwamba wale wanajeshi watiifu wa Uganda kwa rais Obote wakati huo walipangwa ili wakamshambulie Amini uweke huo ushahidi, vinginevyo itakua ni maneno ya propaganda tu.



Unahisi walioasi Rwanda wakaenda South Africa ni wapumbavu, au unahisi Wakenya wenye makosa ya uhaini waliorudishwa kwao tulikosea? Hakuna nchi inafanya upumbavu kama huo, sisi eti kisa Nyerere na Obote walikuwa marafiki
Nchi yoyote duniani inaruhusiwa kisheria kutoa hifadhi ya kisiasa au ukimbizi kwa wahanga wowote. Pia nchi inaweza kuamua kuwarudisha au kuendelea kuwapa hifadhi wahanga kutokana na mazingira itakayoona inafaa. Sasa nakuuliza swali Je kama Amini asingevusha Jeshi lake na kuvamia Tanzania na kuteka sehemu ya ardhi ya Kagera na kusema ni sehemu ya Uganda, unafikiri (Kagera War) ingetokea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…