Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Wazaaaaziiii
Wazazi wetu eeee
Wazaaaaziiii
Wazazi wetu eeee
Mashujaa waliokufa, wamekufa kishujaa
Mashuajaa waliorudi, wamerudi kishujaa
Lengo na nia yetu wazazi, ilikuwa moja
Kuilinda ardhi yetu eeee
Kuilinda ardhi yetu eeee
 

Attachments

Kiuhalisia ile vita haikuwa na Ulazima

Watanzania walikufa wengi sana kuliko Waganda.

Ukikutana na wanaoijua ile vita vizuri watakueleza.
Naomba unipatie majibu ya maswali yangu haya ma4, ili kuthibitisha kauli zako hizo mbili.

"Ile vita haikuwa na ulazima"
1) Je unaijua sababu ya vita ile kupiganwa?

"WaTz walikufa wengi sana kuliko waGanda"
2)Je unayatambua malengo ya vita ile kwa waTz yalikuwa ni yapi?
3)Je malengo yalifikiwa au hayakufikiwa?
4)Kuna vita inayopiganwa bila kupoteza askali?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nyie madogo wa 2000s hata akili hamna kabisa. Yaani unaandika vitu kama hivi bila hata kufikiria
 
Niliwahi ambiwa na Mzee mmoja kuwa mdogo wake alipigana Ile vita

Ni kwamba wanajeshi wa jwtz walizingilwa na kuwekwa Kati halafu amri ikatolewa na na jeshi la Uganda kuwa walale kifudifudi halafu kifaru kikapita kina wakanyaga na kuwaua kabisa. Basi waliofanikiwa kukimbikia wakarudi na kusema yaliyo tokea yote. Wale waliokuwa wanaambiwa kilichotokea wakaadhibiwa Kwa kupigwa viboko 10 Kila mwana jeshi halafu wanaambiwa wasonge mbele.

Wale walio nusurika kufa wakaambiwa ninyi pandeni kwenye gari hili mrudi uraiani.

Kweli wakapanda lkn mmoja wao akawaambiwa wenzeke jamani kama tulio wasimulia kilichotokea wamepigwa vibokona kuambiwa wasonge mbele je sisi tunaenda kufanywaje? Akasema Mimi naenda vitani huko tunaenda kunyongwa kabisa!!

Ikabidi washuke na kwenda kujiunga na wenzao.

Je hili Lina ukweli wowote au ilikuwa chai yenye kwamba ndani yake?
 
Uwongo !!
 
Asante kwa elimu wengine tunapita kujifunza.
 
Vita hiyo tulipoteza sana kuliko faida tuliyopata Watanzania.
Hili lilikuwa kaburi refu la uchumi wetu hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe bado hujui lolote kuhusu vita. Vita sio nzuri lakini nia na kusudi la vita linakusukuma kupigana. Kauli mbiu ya vita popote ni kupigana hadi tone la mwisho la damu hasahasa linapokuja suala la hadui kukuvamia na kuchukua nchi yako. Mvamizi akifanikiwa kukuteka na kutwaa ardhi yako kinachofuatia ni kukufanya mtumwa wewe na wanao na wazazi wako na wake zako? Sasa wewe usiyejielewa je huko tayari kufanywa mtumwa? Idd Amini aliweka wazi kuwa mkoa wa Kagera ni mali yake na akishautwaa atatwaa tena Mwanza na eneo looote la ziwa Victoria upande wa Tanzania mali yake. Na akasema 'by saa nne kesho chai atainywea Dar es Salaam' na kweli ndege za Amini zilifika hadi Dar kabla ya kulazimishwa kutua na kutekwa na jeshi letu. "The is nothing good in war except it is ending". Wee unaongelea hasara kwa upande wa Tanzania, ulishawahi kuwaza hasara ya Uganda? Kwanza kile kitendo cha kupigwa, na kiongozi wako wa nchi kukimbia, na nchi ngeni ikakukalia kwa muda kadhaa, ni kitendo cha AIBU MPAKA KESHO. Tanzania tulishawahi kuitawala Uganda! Na kuanzia hapo tukamuweka Rais tunayemtaka na anatawala mpaka sasa!
 
Tulizunguka sana. Arua, Kasese, portfot na kwingine kabla ya kufika Kampala. Swali ni kwanini tulizunguka sana badala ya kukatisha tu na kufika hapo kampala na kumtimua huyu nduli?

Kwenye vita kuna kitu kinaitwa tactical manuvers, hizi ni muhimu sana,, adui huwa anajipanga sana kwenye njia rahisi. hivyo utapoteza watu wengi hapo, lakin inakuwa ngumu kwa adui kujua njia zako na ni rahis kumpiga.
Kwa wale waliopitia mafunzo zaid wanaelewa hii, inafundishwa
 
Hiyo ni kweli kuna story azisemwi hadi leo mzee wangu alikuwa rubani wa kuvulumisha mabomu enzi hizo
 
Kichuguu,

Tulipoteza wanajeshi wengi, acha kutetea
Kupoteza askari katika vita ni jambo la kawaida! Hiyo ni vita sio harusi! Lakini kinachoangaliwa mwisho wa vita nani kashinda? Kama Tanzania tungehamua kuwaua askari mateka wa Uganda na Sudani ingejuwa "massacre". Tanzania ilipokuwa inakamata askari ilikuwa inawaweka mateka (ilikuwa haiwahui)
 
Wee mwehu nini? Nyerere vita ilimshinda kivipi? Idd Amini alipigwa na kukimbia! Tukaweka uongozi tunaoutaka mpaka leo na kesho!
 
Kwa hiyo gazeti likiandikwa unaamini Tu! Afadhali ingekuwa kitabu
 
Kwa nini wewe ushindwe kumuandikia na kumpigia simu akupe hiyo context uliyoitaja ???au huna context unafoka na kumwaga povu tu ??
Sheikh wangu umevuliwa nguo.jisitiri.acha hili lipite. Tutafute hoja nyingine.hii jamaa ameshinda kwa busara na uelewa. Wala usihamaki na kughadhibika. Kichuguu anaonekana ni msomi.
 
Kiufupi hii vita ilikuwa ya kijinga na kiwendawazimu iliyotugharimu Hadi leo.nyerere alimchokiza idd amini Kwa lengo la kumrudisha Obote Kwa kuwa alipinduliwa na iddi amini baada ya uchumi kuwa hoi.Nyerere alimfadhili Obote na baadhi ya waganda wakafany uvamizi Uganda na kuishia kupigwa vibaya sana na majeshi ya amini(hapo ilikuwa ni kabla ya kutangazwa vita)Alipoona Hivyo iddi amini ndiyo akaamua na yeye kuiteka kagera na ndiyo ikawa mwanzo wa vita rasmi.kiufupi Nyerere alikuwa mchokozi na tungekuwa na mkuu wa majeshi mwenye kujitambua asingemkubalia Nyerere.
 
Kasome vizuri historia yako kama sivyo nwalimu wako alikudanganya
 
Watoto wa 2000 wanapojaribu kuzaliwa 1960

Mdogo wangu vita haikuwa ya ulazima wakati Nduli Iddi Amini Dada alivamia Mkoa wa Kagera kwa madai ya kwamba ile ni sehemu ya uganda lazima aichukue.

Kwa hiyo mwl. JKN angewaachia..!?
Hawa vijana sijui wamedanganywa na walimu wao wa history huko shuleni !? Maana kama kweli aliifatilia ile vita vizuri hawezi kusema haikuwa na ulazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…