Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Haukuwepo; na kama ulikuwepo labda ulikuwa wa siri sana kwa mimi askari wa cheo cha chini sana kuweza kuujua wakati huo. Wakati huo Tanzania ilikuwa upande mmoja na PLO kugombea uhuru wao kwa hiyo tulikuwa against Israel. Vita yote ile ilipiganwa na watanzania tupu akiwema Makongoro Nyerere, mtoto wa rais wakati huo. Tulikuwa na kanali mmoja pale ngome alikuwa anajua jinsi ya kupanga vita siyo mchezo. Huwa mara nyingi ninadhani ni Kanali Lupogo, lakini huenda jina lake halisi litatajwa na mtu mwingine huko mbeleni.
Hilo jina limenikumbusha kitu. Nimemuona mwenzake Madaraka Nyerere akitangaza kugombea Ubunge jimbo la Butiama. Kikubwa kilichomsukuma nadhani ni kwa sababu mwenye jimbo hayuko sawa sana ki-afya Mh. Nimrod Mkono na amekuwa hayupo jimboni kwake kwa muda. Inaonyesha kama Mkono angekuwepo katika afya yake ya kawaida, Madaraka asingegombea jimbo hilo. Yaani hawa watu hawana kabisa hata chembe, ya tamaa ya mamlka kama alivyokuwa baba yao!
 
Mayunga ameshatajwa huko nyuma ukipitia posts mbalimbali utamkuta. Yeye alikuwa ni Brigade Commander tayari na nadhani brigade yake ndiyo iliyo wasafisha askari wa Uganda kutoka pale Mutukula na Mbarara.
Kilichosababisha wamu-nickname "mti mkavu" kilikuwa ni nini?
 
Mkuu Kichuguu ahsante kwa ufafanuzi na maelezo mazuri yaloshiba.

Ila zipo habari za Msumbiji kuisaidia Tanzania kwa kutuma batalioni ya wanajeshi kama 800 hivi.

Hawa walipelekwa moja kwa moja hadi Kagera kwa ndege.

Inawezekana hawa walikwenda kuongeza nguvu kwenye operesheni Chakaza.

Jaribu kutafuta hiii madini ipo mahala.

Ila kwa hakika Tanzania ina historia ya majenerali ambao walikesha wakihakikisha nchi iko mikono salama.

Viongozi wa kijeshi wa kukumbukwa vita vya Kagera:

John Butler Walden- Black Mamba

Silas Mayunga -Mti Mkavu

David Msuguri Jenerali -Mtukula

Meja jenerali Ben Msuya,

Colonel Tumbi -Kamanda Radi

Meja jenerali Tumainieli Kiwelu na

Meja jenerali Mwita Marwa - Kambale
Tukiwa shule ya msingi, ilikuwa kila ikifika sherehe haya majina tulikuwa tunayaimba mpaka koo zinaanza kukwama,..., Marwa, Msuguli, Mti Mkavu,.....
 
Hilo jina limenikumbusha kitu. Nimemuona mwenzake Madaraka Nyerere akitangaza kugombea Ubunge jimbo la Butiama. Kikubwa kilichomsukuma nadhani ni kwa sababu mwenye jimbo hayuko sawa sana ki-afya Mh. Nimrod Mkono na amekuwa hayupo jimboni kwake kwa muda. Inaonyesha kama Mkono angekuwepo katika afya yake ya kawaida, Madaraka asingegombea jimbo hilo. Yaani hawa watu hawana kabisa hata chembe, ya tamaa ya mamlka kama alivyokuwa baba yao!

Katika viongozi wa jeshi niliokutana nao , huyu Brigadia Marwa ninamvulia kofia. Ni mtu mpole sana hana makuu, na kila mtu akimjali. Alinisaidia sana na sitomsahau. Pia akiwasaidia wengi. Alikuwepo hapa Zanzibar jeshini miaka hiyo
 
Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)

Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita... Wanajeshi walikua hawatoshi?
Kula yanga- Ni madhara ya vita hayaepukiki, Mama aweza acha kupika sababu ya kipigo cha baba usiku, akiugulia maumivu, mtashinda njaa siku hiyo ni kawaida ya ugomvi.

Huko vitani tulitumia hela, siyo maneno . uchumi lazima uyumbe bin kushuka!
lkn tumelipwa mafweza na uganda.

Nyerere hakushindwa vita hata nukta, kuhusu migambo, wananchi walijitolea wenyewe kwenda Front kama Mkoa wa Mara na wilaya zake zote uliongoza. vijana walililia kwenda jeshini. mpaka wakatungiwa wimbo ''hiyo mama hiyo mama mtoto...+2.'' na Tarime michango mingi ya ng'ombe 5 kila familia ilitoka mpaka jeshi likashindwa kubeba.
 
Wakati wa uhai wake wote Msuguri alitusaidia sana mkoa wa Mara kwa Lift za bure Dege la jeshi, kwenda Bongo na kwingineko! ukitamka tu ''Afande! mimi mtoto wa Msuguri unabebwa Faster''
bila kujali! aliheshimiwa huyo!!!!!!!
 
Faraja Kota huyu!!! huyu!! wa MATC Mtwara?? tuliye kuwa tunagombea maharage? na kuiba samaki za Wamakonde magomeni au mwingine?
Sijui unamsema nani; baba yake Faraja Kotta ni Brigadier General Kotta; alikuwa mtaalam wa mizinga (Long Range Gun Artilleries na Howitzers) jeshini, na alifariki mwaka 2008. Sasa sijui wewe uligombea naye maharage lini.
 
Tulizunguka sana. Arua, Kasese, portfot na kwingine kabla ya kufika Kampala. Swali ni kwanini tulizunguka sana badala ya kukatisha tu na kufika hapo kampala na kumtimua huyu nduli?
View attachment 1418087
Swali lako zuri,ni kweli kuna kikosi kilipitia huko sudan ila haimaanishi vyote vilipita huko,ni kamandi moja tuu ndio ilipita huko kwa dhumuni la kuivamia Uganda kwa kupitia Nimule(boarder ya ug&Sudan) na aliyewezesha vikosi kufika hapa ni either Kamanda Lupogo au Kimario(mmoja wao ndiye alianza advancement ila baada ya kushindwa aliludishwa makao na mwengine ndiye akaongoza kwa mafanikio sana kwa kupitia katika mwa uganda)
 
Kwan msuguri kashatangulia mbele za haki? Sijasikia mimi
Wakati wa uhai wake wote Msuguri alitusaidia sana mkoa wa Mara kwa Lift za bure Dege la jeshi, kwenda Bongo na kwingineko! ukitamka tu ''Afande! mimi mtoto wa Msuguri unabebwa Faster''
bila kujali! aliheshimiwa huyo!!!!!!!
 
Ila wahaya ni wakuwaonea huruma sana, Ukimwi ulipoingia uliwafyeka sana wao na Vita ya Kagera iliwamaliza sana.... haiyumkini leo hii hili ndio lingekuwa kabila kubwa na lenye nguvu nchini hasa kwa idadi ya watu.... pia Mji wa Bukoba ungekuwa Jiji pengine.... Mungu awape nguvu wahaya na makabila yote wazawa wa Bukoba
Kitu cha ajabu ni kuwa Ukimwi uliingia Tanzania kutokea Uganda mwaka 1984 ukiwa unaitwa "Juliana" kutokana na mashati ya beach ya aina ya Hawaii na Bahama ambayo yalikuwa yameandikwa "Juliana." Mashati haya yalikuwa yanaingizwa nchini na wafanya biashara ya mageado kutokea Uganda baada ya vita na ndio wanaoaminika kuwa carriers wa kwanza wa Ukimwi kuingia nchini. Kwa hiyo Kagera kuwa victim wakubwa kama Uganda ni obvious; ila Dar es Salaama watu walipukutika sana kwa ukimwi. Nilikuwa ninaishi Sinza, kila siku mtaa ulikuwa na kifo hasa kwa vijana. Generation ya 1985-1992 ilipungua sana kutokana na janga hilo.
 
Kichuguu wewe una elimu na pia umri wa kutosha acha kubishana na hawa akina kichwa nazi Gavana hawa huwa hawana hoja washakuwa brain washed. Wewe tupe madini sisi wenye akili. Hawa ambao.... Achana nao watakupotezea muda tu

Sisi unatuona ni vichwa maji kwa sababu mzigo wa mwenzako kwako unaona ni ganda la usufi. Athari ya uvamizi tunayo sisi Wazanzibari tunamwelewa Laanatullahi Nyerere vizuri
 
Ni ujinga wenu tu na laana baada ya kumkataa mwana mapinduzi John Okello. Mpaka leo hiu mnamlaumu Nyerere na ninyi wenyewe ndo mabwege. Nyie ndo laanatullahi maana hamjitambui hamjielewi.

Mnashindwa nini kujikwamua? Ndo ukichwa nazi wenyewe huo. Hata rais wenu mnapangiwa ....hapo nyerere anahusikaje? Huo ni Ubwege. Pambaneni na hali zenu.

Sisi unatuona ni vichwa maji kwa sababu mzigo wa mwenzako kwako unaona ni ganda la usufi. Athari ya ivamizi tunayo sisi Wazanzibari tunamwelewa Laanatullahi Nyerere vizuri
 
Ni ujinga wenu tu na laana baada ya kumkataa mwana mapinduzi John Okello. Mpaka leo hiu mnamlaumu Nyerere na ninyi wenyewe ndo mabwege. Nyie ndo laanatullahi maana hamjitambui hamjielewi.

Mnashindwa nini kujikwamua? Ndo ukichwa nazi wenyewe huo. Hata rais wenu mnapangiwa ....hapo nyerere anahusikaje? Huo ni Ubwege. Pambaneni na hali zenu.

Haki ya kukasirika na kuandika povu lako unayo endelea tu kuharisha
 
Heeeeeh....😳😳😳 Mimi tena ndo wa kukasirika? Kwa lipi? Wakati sisi ndo tunawatawala nyie😂😂😂 na wewe ndo unalalamika kila uchwao na kumlaani nyerere. Mi sina hasira. Wewe ndo una hasira katika kila comment yako. Inaonekana you cant breath 😂😂😂

Haki ya kukasirika na kuandika povu lako unayo endelea tu kuharisha
 
Kwa taarifa yako majeshi ya Uganda yalikuwa vizuri sana kabla ya uasi.

Vita ilipoanza tulipoteza wanajeshi wengi mno japo taarifa zilifichwa, binamu yangu amepigana na amesimulia mengi mno ambayo serikali haikuweka na haitaweka wazi.

Hivyo unaposema kwani tulizunguka, unafikiri hao jamaa walikuwa dhaifu kiasi hicho?

Vita ina mbinu nyingi, moja wapo ni kumzunguka adui wakati yeye anapambana na wale waliom face... ghafla snashangaa anashambuliwa eneo ambalo asikutegemea.


Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna ukweli hapo, ila mibongo itakupinga kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom