Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Yaani ndugu yangu bado huamani kuwa hata mimi nilikuwa askari tena nikiwa katikati ya mawasiliano kwa hiyo hao wengine waliokuambia ndio unawaamini tu? Pamoja na kukueleza kuwa kikosi kilichokuja kutoka msumbiji kilikuwa ni cha askari wa Tanzania ambacho kilikuwa ni sehemu ya Brigade ta Tembo; kabla ya vita kilikuwa kinafundisha jeshi jipya la msumbiji kikalazimika kurudi nyumbani kuungana na wenzao.
Elewa kuwa Tanzania tulikuwa na BM-21 launchers chache sana zisizofikia 10 na huenda zilikuwa hazizidi tano, halafu nawe unaamini kuwa tuliletewa battalion nzima kutoka msumbiji kuja kutusaidia kuoperate hizo BM-21 launchers ambazo kila moja inakuwa operated na askari watatu tu? Vile vile hata hujui kuwa Kanali Kotta alikuwa ni mtaalamu wa silaha hizo au naye utasema alikuwa wa katoka Msumbiji?
Waandishi hawakuwapo vitani; mwandishi pekee aliyekuwa vitani ni Ben Kiko ambaye naye alirudishwa nyuma baada ya vita ya Maska au Mbarara kwa sababu alianza kuwa anatangaza mambo ambayo yalikuwa yanaingiliana na tactics za jeshi. Hao wengine wote unaosoma habari zao ni za kusimuliwa na za kuhisisi tu, na hasa kama waandishi wenyewe walikuwa na wa kutoka nje ya nchi. Hata huyo uliyekwoti unasoma wazi kuwa naye hayuko definitive kwa hilo. Ni vivyo hivyo hata wewe ukiandika kitabu chako leo, nawe utasema hivyo hivyo kwa sababu ya kusikia tu. Nilikupa hint kuwa jaribu kumwuliza Gen Msuya ambaye ndiye aliyeteka jji la Kampala kwa sababu bado yuko hai umwulize swali hilo.
Ingawa ni kweli kuwa tulipata support kutoka Msumbiji na nchi nyingine za Adfrika kama Algeria, Zambia na Ethiopia kama sign ya gesture; walitusaidia silaha na fedha za kununulia silaha lakini lakini siyo wanajeshi hata kidogo. Halafu hao askari wa Uganda waliokuwa against Amin kwanza walikuwa wakimbizi wakiishi Tanzania, baada ya vita kuanza ndipo nao wakashirikishwa kama sehemu ya jitihadi za kukomboa nchi yao chini ya umbrella ya SUM (Save Uganda Movement) na tuliwaruhusu kwa lengo la kisiasa tu, siyo kwa sababu za kijeshi. Ilitakiwa ijulikane kuwa Amin aliangushwa na Waganda wenyewe, na ndiyo maana ya kuitisha mkutano wa Moshi.
Kitabu kuchapishwa Tanzania sioni kuwa ni kuhalisha kuwa kinasema ukweli; inategema na editorial oversight ya publisher. Kuna kitabu kilichowahi kuchapishwa Tanzania na mtu mmoja alikuwa akiitwa Candid Scope aliandika kitabu kikiwa kinakashifu serikali ya Nyerere wakati wa utawala wa Nyerere na kilitoka. Kuna vitabu vingi vya kama Kaptula la Marx vyote vilitoka na siyo kuwa vilikuwa vinakubaliwa na serikali. Kuchapishwa na TPH hakuna significance yoyote hapa
Duh hata hili la uwepo wa waandishi wa habari wawili waitwao Tony Avirgan na Martha Honey nalo unalikataa?
Hao ni waandishi pekee wa kimataifa ambao walipewa clearance na serikali ya mwalimu Nyerere kucover operation za Jeshi letu ndani ya Uganda.
Na hawa waandishi ndo waliandika hicho kitabu na kuelezea uwepo wa askari wa msumbiji nchini.
Hoja ya vitabu kuchapwa bado ni muhimu, Vitabu vyote vinavyozungumzia masuala ya operesheni za ulinzi na usalama vina utaratibu tofauti wa kufuata ili vipewe clearance, Scrutiny yake ni kubwa zaidi kuliko vitabu vya kawaida, kwa hiyo ni dhahiri kama hicho kitabu kilichapwa nchini basi kilipitiwa kwelikweli na watu wa vyombo vya usalama.
Lakini tukiacha kuchapwa, Vitabu vingi kama ulivyovisema kama vilikuwa na taarifa kubwa za upotoshaji vilikuwa vinafungiwa kuuzwa nchini, yaani vinapigwa ban, na hili lilifanyika sana kipindi cha mwalimu, Laiti hicho kitabu kingekuwa na information ya uongo na tena serious namna hiyo basi kingezuiwa kuuzwa nchini au wangetakiwa wabadirishe hiyo information, kwa kuwa hilo halijafanyika, au waandishi mahali popote kupata formal challenge ya kurevise hiyo information basi maana yake maelezo yao yako solid
Mzee Kichuguu, Ukiwa mwanajeshi huwezi jua yote, kubali tu kuwa hili ulikuwa hulijui, Siyo unyonge huo ni ubinadamu tu!