Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

(1)Kwenye ishu ya kufa kuna majibu yote matatu, ama kuna waliokufa, au hawakufa yote yanawezekana, Mathalani Tulikuwa na Wanajeshi zaidi ya 40000 kwenye uwanja wa mapambano askari tuliopoteza hawakufika hata 1000, which means survival rate ilikuwa ni kubwa!.

(2) Haukuwa peke yako vitani, tena wewe ulikuwa askari wa akiba kama ulivyosema huko awali, hauna uhakika wa nini haswa kilitokea msitari wabele. Waliokuwa na hao wasumbiji kwenye units zao Wanakiri kushirikana nao, nashangaa ushuhuda huu huutaki!, Kila saa unaukwepa ushuhuda huu

(3) Ishu ya askari wa Msumbiji toka mwanzo ilikuwa clouded na secrecy, hii ni kwa sababu Nyerere hakutaka hii vita ionekane as if ni ya Afrika nzima, hakupenda Afrika idhani Tanzania inatumia position yake ya frontline state kujisaidia kwenye vita zake yenyewe dhidi ya member mwingine wa OAU, Hata hivyo hakuna siri duniani!.
Huyu jamaa ana ubishi wa kiboya

Kichuguu hakuwa uwanja wa vita lakini ana access ya taarifa zote hata za siri sababu alikuwa kitengo cha mawasiliano
 
Vita ilikuwa 1978, ni miaka 42 sasa. Wapiganaji wengi waliokwenda vitani mstari wa mbele by the time walikuwa na age ya 25 - 40. Kwa sasa kundi hili lina miaka 67 - 82.

Wengi watakuwa wameshatangulia mbele ya haki na waliopo wapo hoi bin taabani ki maisha. Je tuna utaratibu wa kuwakumbuka mashujaa hawa hata kwa Bima ya afya tu na viposho kidogo vya kuwawezesha kumudu maisha ya uzeeni?

Huyu hapa - Zahir Ally Zoro, aliyekuwa mmoja wa askari mstari wa mbele kumtandika Nduli Idd Amini.

Kuna habari zilisambaa kuhusu vita - sasa mtoa mada unaweza kusema ni ya kweli ama urongo...

- Kikosi cha Mizinga chini ya MAYUNGA ( mti mkavu) ndicho kilifanya kazi kubwa mno kumsambaratisha nduli Amin, wanasema mzee alikuwa anatumia na uwezo mwingine wa kiasili..bila kikosi hiki mambo yalikuwa yashaanza kuharibika.
 
Walipotea wapi; si ajabu unasikia hadithi tu; ni kweli tulipoteza wanajeshi karibu 500 ( siyo 2000 ingawa sina namba kamili) ambayo ni karibu batallion moja, na nimekuambia kuwa katika hatua za kwanza za vita kuna karibu Batallion nzima iliyopotea kwa sababu ya uamuzi mbovu wa kamanda mmoja.

Vile vile vita ya Lukaya iliua waganda na walibya wengi sana lakini pia watanzania walikufa. Mimi nilikuwa karibu sana na taarifa za mapambano yale kuanzia mwezi Octoba mwaka 1978 (siyo 1979) kabla hata Rais hajatangaza vita yenyewe kwa vile nilikuwa kwenye Brigedi ya Magharibi ambayo ndiyo iliingia vitani kwanza.

Vita iliendelea kwa miezi saba katika mazingira magumu kama niliyosema hapo, hivyo ni kweli watu walikufa. Huwezi kupigana vita ya ardhini bila askari wako kufa. Jeshi la Uganda halikuasi bali lilielemewa nguvu na jeshi la Tanzania licha ya kuwa walikuwa wanasaidiwa na askari wengi sana kutoka Libya.

Unaposema kuwa watu wetu walielemewa sana ila baada ya hapo jeshi la Uganda likaasi ndipo tukapata unafuu- ni wazi hujui vita nini- ile siyo ngoma ya mdundiko ndugu yangu, ni kazi ya kurushiana risasi za moto, sema pia ni askari wangapi wa Uganda waliokufa kama hutapatwa na ugonjwa wa moyo iwapo unaliangalia jeshi la Tanzania wakati huo katika negative lens;

Jeshi la Uganda lilikuwa kubwa sana, Amini alikuwa anawekeza sana katika jeshi kuliko sehemu nyingine yoyote, ila sasa JWTZ ilikuwa inawafuta kama sisimizi ndipo wakafikia kukata tamaa ya kuendelea na vita ile.
Mkuu wape somo, siye wengine tulikoswa koswa kwa futi moja tu ili tuingie jeshi wakati ule maana ndio kwanza tumemaliza JKT, 1977.
 
Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)

Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita... Wanajeshi walikua hawatoshi?
Siye tulikuwapo miaka hiyo.
Nyerere alikuwa na akili sana.
Jeshi kama la JKT , mgambo, Polisi na Magereza wote ni reserve army.
Hao walitayarishwa KABLA hata ya vita.
Mimi nilikuwa JKT 1977, zoezi tulilopiga la kijeshi lilikuwa si la kawaida na tulijua kuwa lazima kunaweza tokea jambo.

Uhusiano na Ugada wakati huo ulikuwa si mzuri.
Ni uongo kusema kwamba hao reserve army walikusanywa ati baada ya JWTZ kushindwa.
Vita huendi kama unaenda ngomani, unjitayarisha kwa idadi ya wanajeshi na vifaa.

Tulisikia kutoka BBC kuwa Iddi Amin ameshabmulia na ameteka kule Kagera.
Vijana tulikuwa na moto wa kwenda kuitetea nchi, na si wote walifaninikiwa kwenda.

Vijana wengi wa sasa hamjui ule uzalendo uliokuwepo miaka hiyo, na wengi walikuwa wakisema tukimpata Amin tutamla nyama.
Pili, una hadithi za kudanganywa , unga wa Yanga toka Marekani likuja mwaka 1974 baada ya njaa iliyoikumba nchi.
Mashuleni tulikula sana unga huo na haukuwahi kuja tena baada ya 1974.
 
Siye tulikuwapo miaka hiyo.
Nyerere alikuwa na akili sana.
Jeshi kama la JKT , mgambo, Polisi na Magereza wote ni reserve army.
Hao walitayarishwa KABLA hata ya vita.
Mimi nilikuwa JKT 1977, zoezi yulilopiga la kijeshi lilikuwa si la kawaida na tulijua kuwa kazima kunaweza tokea jambo.

Uhusiano na Ugada wakati huo ulikuwa si mzuri.
Ni ungo kusema kwamba hao reserve army walikusanywa ati baada ya JWTZ kushindwa.
Vita huendi kama unaenda ngomani, unjitayarisha kwa idadi ya wanajeshi na vifaa.

Tulisikia kutoka BBC kuwa Iddi Amin ameshabmulia na ameteka kule Kagera.
Vijana tulikuwa na moto wa kwenda kuitetea nchi, na si wote waifanimikwa kwenda.

Vijana wengi wa sasa hamjui ule uzalendo uliokuwepo miaka hiyo, na wengi walikuwa wakisema tukimpata Amin tutamla nyama.
Pili, una hadithi za kudanganywa , unga wa Yanga toka Marekani likuja mwaka 1974 baada ya njaa iliyoikumba nchi.
Mashuleni tulikula sana unga huo na haukuwahi kuja tena baada ya 1974.
Mkuu inasemekana mwaka 1984 kutokana na njaa kali Wananchi waliponea unga wa Yanga toka Marekani
 
Mkuu inasemekana mwaka 1984 kutokana na njaa kali Wananchi waliponea unga wa Yanga toka Marekani
Uwongo mkubwa sana sana huu; in fact mwaka 1984 Tanzania tulikuwa na chakula kingi sana kuliko uwezo wa kukitumia, kingi kikapelekwa maghala ya National Milling Corporation. Njaa iliyoleta mahindi ya Yanga ilikuwa ni matokeo ya el-nino ya mwaka 1974; na mbaya zaidi ikawa ni muda mfupi baada ya operatetion vijiji, ambapo mashamba mengi ya asili yalikuwa hayakulimwa mwaka 1973. Baada ya Njaa hiyo Nyerere alikuja na mwito wa "Siasa ni Kilimo"- yaani Azimio la Iringa, na kusababisha nchi iwe inazalaisha chakula kingi sana kuliko mahitaji yake hadi mwaka mwaka 1987 ndiyo siasa ni kilimo ilipotoweka. Anayekuwambia kulikuwa na mahindi ya yanga mwaka 1984 anakudanganya, na hakutendei haki kwa kufanya hivyo kwani anatumia udogo wako kutokuheshimu akili yako.
 
Mheshimiwa hata mimi nilikuwepo mwaka wa 1984, nilikuwa mwanafunzi wa form 3. Mwaka huo tulikula ugali wa 'yanga' shuleni, na unga huo ulikuwa unaletwa kama msaada kwa sababu ya njaa iliyokuwepo kipindi hicho.
Kwa hiyo njaa ya 1984 ni jambo halisi, lilitokea na sisi wengine tulishuhudia.
 
Huo ni uwongo blatant; form 3 Ulikuwa unasoma shule gani, na Headmaster wako alikuwa anatoa wapi ungo huo wa yanga kwani kuanzia mwaka 1977 National Milling Corporation (NMC) ilikuwa na chakula cha kutosha sana; usingeweza kula unga wa yanga ulioletwa mwaka 1974 baada ya miaka kumi kwani ungekuwa umeoza wote. Ule unga wa yanga ulikuja Tanzania kwa kuidhinishwa na rais Jimmy Carter mwaka huo wa 1974 na mwaka 1984 rais wa Marekani alikuwa Reagan ambaye hakuwa na uhusino kabisa na nchi zilizokukuwa zina mlengo wa kijamaa kama Tanzania na hakuwahi kutoa msaada wowote Tanzania. Acha kusema uwongo mbele ya wazee tunaojua mambo hayo kwa kina; hata sisi tuliokula unga ule tunajua kuwa mkwishoni mwa mwaka 1974 ulikuwa umeharibika. Tuliltetewa meli moja tu ya unga wa yanga, siyo kuwa tulikuwa tunaletewa kila siku; kwa hiyo baada ya muda unga ule ulianza kuharibika.
 
Ni kweli inawezekana sana kwani sina mahesabu kamili haraka haraka kichwani, ila wakati ule batalian moja ilikuwa na kombania saba pamoja na hedikwota COY, na kila kombania ilikuwa na platuni tatu pamoja na ile ya hedikwota zote kwa pamoja zikiwa na kama askari kama 120 mpaka 130 hivi-sitaki kwenda kwa kina zaidi juu ya Organization ya wakati huo. Sasa ukipiga hseabu hiyo mara saba kwenye Battalion moja ni kama askari 910 ambao ukijumulisha na na HQ COY unapata kamaaskari kama 1260. Ila sasa Batallion za kivita wakati huo zilikuwa ni kubwa zaidi ya orgaization hiyo kwa sababu ya Mgambo, magereza, JKT na Polis waliunganishwa katika Batallions hizo.

Jamaa wa Wikipedia wanatoa namba za vifo kama ifuatavyo kwa hiyo hawakufika 2000 wala Batallion moja ya kawaida. Ila majeruhi walikuwa wengi zaidi.

View attachment 1471680
Hao 435 ni wale waliozikwa Kaboya, lakini wengine walizikwa nyumbani kwao. Sisi ndugu yetu aliyefia vitani aliletwa nyumbani akazikwa kijeshi. Nilikuwa darasa la tano nakumbuka lile tukio vizuri kabisa.
 
Huo ni uwongo blatant; form 3 Ulikuwa unasoma shule gani, na Headmaster wako alikuwa anatoa wapi ungo huo wa yanga kwani kuanzia mwaka 1977 National Milling Corporation (NMC) ilikuwa na chakula cha kutosha sana; usingeweza kula unga wa yanga ulioletwa mwaka 1974 baada ya miaka kumi kwani ungekuwa umeoza wote. Ule unga wa yanga ulikuja Tanzania kwa kuidhinishwa na rais Jimmy Carter mwaka huo wa 1974 na mwaka 1984 rais wa Marekani alikuwa Reagan ambaye hakuwa na uhusino kabisa na nchi zilizokukuwa zina mlengo wa kijamaa kama Tanzania na hakuwahi kutoa msaada wowote Tanzania. Acha kusema uwongo mbele ya wazee tunaojua mambo hayo kwa kina; hata sisi tuliokula unga ule tunajua kuwa mkwishoni mwa mwaka 1974 ulikuwa umeharibika. Tuliltetewa meli moja tu ya unga wa yanga, siyo kuwa tulikuwa tunaletewa kila siku; kwa hiyo baada ya muda unga ule ulianza kuharibika.
Wewe hapo 1984 ulishakuwa bosi unakula bata batani, hukujua kinachoendelea kwa wengine wa hali ya chini, sisi wengine tulikuwa shule. Nimesoma Umbwe secondary school iko Kibosho Moshi. Wenzangu kama wako humu watashuhudia.
 
Ukweli ni kwamba hakukuwa na unga wa Yanga Tanzania mwaka 1984; unaweza kuwa ulikula dona lakini siyo yanga. Tanzania hatukuwahi kilima mahindi ya yanga, tuliletewa unga ule kwenye mifuko ya USAID kutoka marekani na ilikuja meli moja tu. Tulipoanza kuula ulikuwa mzuri tu, rangi ya yanga haikuwa tatizo. Ni kwamba baada ya muda ndipo ukawa unaharibika na kuanza kukosa radha. Mpaka leo ninaishi marekani nikitaka ugali wakati mwingine huwa nanunua unga wa Goya wa Yanga na hauna tatizo kabisa. Wote wanaolalamikia unga wa yanga ni kwa historia kuwa baadaye mwishoni mwa mwaka 1974 na hadi mwishoni mwa 1976 unga ule ulianza kuharibika na kuwa mchungu. Haukuendelea kwenye mzunguko baada baada ya 1976; kwa hiyo wakati tunasheherekea kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977 tulishasahau kabisa unga wa Yanga.

Wewe huko Umbwe unaweza kuwa ulikula dona la kawaida tu ambalo halikukobolewa vizuri au lilitokana na mahindi ambayo hayakukuka vizuri, ukaaminishwa kuwa huo ni unga wa yanga lakini siyo kweli! Kubaliana na mimi mzee wangu; wengine tumepitia historia ya nchi hii kwa njia za ajabu sana na tunaijua vizuri sana.
 
Huo ni uwongo blatant; form 3 Ulikuwa unasoma shule gani, na Headmaster wako alikuwa anatoa wapi ungo huo wa yanga kwani kuanzia mwaka 1977 National Milling Corporation (NMC) ilikuwa na chakula cha kutosha sana; usingeweza kula unga wa yanga ulioletwa mwaka 1974 baada ya miaka kumi kwani ungekuwa umeoza wote. Ule unga wa yanga ulikuja Tanzania kwa kuidhinishwa na rais Jimmy Carter mwaka huo wa 1974 na mwaka 1984 rais wa Marekani alikuwa Reagan ambaye hakuwa na uhusino kabisa na nchi zilizokukuwa zina mlengo wa kijamaa kama Tanzania na hakuwahi kutoa msaada wowote Tanzania. Acha kusema uwongo mbele ya wazee tunaojua mambo hayo kwa kina; hata sisi tuliokula unga ule tunajua kuwa mkwishoni mwa mwaka 1974 ulikuwa umeharibika. Tuliltetewa meli moja tu ya unga wa yanga, siyo kuwa tulikuwa tunaletewa kila siku; kwa hiyo baada ya muda unga ule ulianza kuharibika.
Mkuu hao wamehadithiwa stori na wakubwa wao kinusu nusu.
Mwaka 1984, actually kuanzia mwisho wa vita ya Kagera hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana.
Vitu vilikuwa mwendo wa kuruka, lakini unga wa Yanga haukuwa msimu huo.
Nakumbuka baada ya vita Mwalimu alilitangazia Taifa kuwa tutakuwa na "miezi kumi na nane" ya msuko suko wa kiuchumi kutokana na vita ya Kagera.
Hiyo " miezi kumi nane " ikageuka kuwa miaka, na wananchi wakaanza kuwa disillusioned.
Huko Mtwara watu walivaa magunia-si uongo, hilo lilishuhudiwa na Waziri Mkuu wakati huo Salim Ahmed Salim.
Na huo ulikuwa mwanzo wa kurasimisha mitumba ya nguo.
Kwa kuona mbali, Mwalimu alisema muda huu, kipindi chake kikiisha 1985 , ni lazima ang'atuke na kumpisha Rais mwingine.
 
Uwongo mkubwa sana sana huu; in fact mwaka 1984 Tanzania tulikuwa na chakula kingi sana kuliko uwezo wa kukitumia, kingi kikapelekwa maghala ya National Milling Corporation. Njaa iliyoleta mahindi ya Yanga ilikuwa ni matokeo ya el-nino ya mwaka 1974; na mbaya zaidi ikawa ni muda mfupi baada ya operatetion vijiji, ambapo mashamba mengi ya asili yalikuwa hayakulimwa mwaka 1973. Baada ya Njaa hiyo Nyerere alikuja na mwito wa "Siasa ni Kilimo"- yaani Azimio la Iringa, na kusababisha nchi iwe inazalaisha chakula kingi sana kuliko mahitaji yake hadi mwaka mwaka 1987 ndiyo siasa ni kilimo ilipotoweka. Anayekuwambia kulikuwa na mahindi ya yanga mwaka 1984 anakudanganya, na hakutendei haki kwa kufanya hivyo kwani anatumia udogo wako kutokuheshimu akili yako.
mzee wangu Kichuguu ni kweli 1984 kulikuwepo na huo unga wa yanga. Sikimbuki kama ni njaa au ni nini maana nilikuwa mdogo na nilikuwa nakula tu bila kujua kwamba ilikuwa ni njaa. Nakumbuka kabisa nilikuwa darasa la nne.

Pia kulikuwa na yale mahindi ya yanga tulikuwa tunakwenda kusaga na kupata unga kwa ajili ya ugali.

Yote kwa yote Kichuguu wewe ni mzito sana. Una busara unajua kuelimisha, kufundisha, kueleza japo unakutana na wabishi wao ndio wanafanya wewe uzidi kufunguka na kutoa elimu kwetu.

Kuna mdau hapo juu kaweka mziki wa jkt Mafinga ya Zairi Ally Zohoro Tumerudi kishujaa. Huo mziki ndio chanzo haswa cha mimi kuweka huu uzi hapa.
Nikushukuru sana mzee wangu kwa elimu uliyotoa hapa. Barikiwa sana.
 
Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)

Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita... Wanajeshi walikua hawatoshi?

Ahsante. 1979 ulikua una umri gani kaka?

Hivi kuna mtu kamili anayehitaji kufundishwa uhusiano wa maendeleo ya uchumi na vita au instability yoyote?
 
Vita hiyo tulipoteza sana kuliko faida tuliyopata Watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakunaga vita yenye faida ( kwa maana kuongeza pesa ), issue ni kwamba, kwanini tulikwenda kupigana na Amini ndio muhimu, ukilijua hilo wala haikupi shida sana. Amini alianza uchokozi since 1972, yaani alivyo pindua tu akaanza uchokozi dhidi yetu, Nyerere ni mvumilivu sana otherwise tulitakiwa kupigana na Amini even before huo mwaka 78
 
Back
Top Bottom