Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Vita hiyo tulipoteza sana kuliko faida tuliyopata Watanzania.
Hili lilikuwa kaburi refu la uchumi wetu hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna lolote ni sera mbovu za kiuchumi ndio kaburi refu la uchumi kwa Tanzania.
Hivi Tanzania mngepigana vita nyingi kama Misri ingekuaje!?
Kupitia 1970-2020 Misri imepigana sio chini ya vita tatu,mbona hadi sasa Misri haijayumba kiuchumi!??
Wacheni visingizio badilini sera za uongozi na uchumi.
 
Ile vita ilipangwa na matajiri wa nchi za kiarabu na Marekani.

Palikua hakuna namna ya kuvikwepa kwa sababu lengo lilikua ni kudhoofisha na kuua ujamaa.

Baadae Alhaj Iddi Amini Dada aliamua kuweka na itikadi za Kidini na kuanza kuwaua Maaskofu na viongozi wa dini ya Kikristo waliokua wanamkosoa kwa kumwambia ukweli kuwa anakosea.

Lakini pia Nyerere angechelewa Mzuka wa Mapinduzi ungehamia Nchi zote za Afrika Mashariki hasa Tanzania yenye Rasilimali nyingi zilizokua zinagombanuwa na nchi za Kibeberu.
Nyerere asingeweza kuruhusu nchi yake ivamiwe na majeshi yaliyokuwa yanamtafuta Milton Obote ,Rais wa Uganda aliyepinduliwa.

Baada ya kufanya mapinduzi Shekhe Alhaj Iddi Amin Dada alikua na agenda kuu Tatu au nne:-
(1) Kujenga himaya ya Kiislam Uganda huku akiunga mkono harakati za kulifuta Taifa Teule la Israel.
(2)Kuwasaka maadui zake na waasi waliokua wamekimbilia Tanzania .
(3)Kujenga mfumo imara wa Kujamaa kwa kutaifisha mali zote za mabeberu na mafisadi na kuzigawa kwa waganda( Hii ilikua ni agenda nzuri iliyorudisha rasilimali za Uganda kwa wazawa mpaka leo)

Hata hivyo ni wazi kuwa nchi yoyote ambayo haikupita mapinduzi ya kijeshi inakuwa na siasa za kitapeli sana . Uganda ameokolewa na Mapinduzi ya kijeshi yaliyoasisiwa na Iddi Amini .
Wanasiasa ni machawa wa matajiri wa nchi za Magharibi na Waarabu. Ndio maana kule Booroondi rais anaacha makumi ya wapiga kura wake wakiwa wanakufa kwenye kwenye kifusi na kwenda kujipendekeza kwa Mabeberu wanaotembelea ardhi ya waliofukiwa ardhini.

Nilimsikiliza Musiba nikamuelewa alikua anaongea akimaanisha kinyume chake na zlimaanisha huku akiepuka kuuawa au kurudishwa kwao Booroondi au Kanyer.
 
Sisi Walibya wa Tandale kwa Tumbo tuliumizwa sana na Ushindi ule wa Tanzania. Tulitamani Tanzania ishindwe
 
Hamna lolote ni sera mbovu za kiuchumi ndio kaburi refu la uchumi kwa Tanzania.
Hivi Tanzania mngepigana vita nyingi kama Misri ingekuaje!?
Kupitia 1970-2020 Misri imepigana sio chini ya vita tatu,mbona hadi sasa Misri haijayumba kiuchumi!??
Wacheni visingizio badilini sera za uongozi na uchumi.
Misri? Zungumzia Israel. Maana hao Misri wameshawahi chapwa mara kadhaa na Israel pia.
 
Hata hao waliokuwepo kwenye vita wamenithibitishia, na hili nimelieleza sana Je nao pia hutaki?
Aliyekusimulia aliongezea chumvi. Msumbiji walikuja Askari wetu ambao walikuwa kule na si Askari wa Msumbiji. Usisikie habari za kusimuliwa na vibaraka. Idd Amin alisaidiwa na Libya na wwo tukawachapa pia
 
Hawakukatiza mkuu, ni kwamba majeshi ya Tanzania yalitembeza kichapo kwa Idd Amin, wakaingia hadi kaskazini na magharibi mwa nchi ya Uganda, wakafika kwenye mipaka ya Uganda na Zaire(DRC), mipaka ya Uganda na Sudan. Mji wa Arua uliopo kaskazini mwa Uganda ndio kipo kijiji cha Koboko, kijiji alichozaliwa Idd Amin Dada.

Waliingia huko wakiwa na mzuka wa mapambano. Amin akasalimu amri, akakimbia Uganda na kuacha majeshi ya Tanzania (Wakombozi) yakiikamata Uganda.
Amin hakukimbia alikamatwa na gen musuguri,ila nyerere alimwambia musuguri mwacheni aende
 
Hata hao waliokuwepo kwenye vita wamenithibitishia, na hili nimelieleza sana Je nao pia hutaki?
Aliyekusimulia aliongezea chumvi. Msumbiji walikuja Askari wetu ambao walikuwa kule na si Askari wa Msumbiji. Usisikie habari za kusimuliwa na vibaraka. Idd Amin alisaidiwa na Libya na wwo tukawachapa pia
 
Tulizunguka sana. Arua, Kasese, portfot na kwingine kabla ya kufika Kampala. Swali ni kwanini tulizunguka sana badala ya kukatisha tu na kufika hapo kampala na kumtimua huyu nduli?

1. Kuepuka Mashambulizi ya Moja kwa Moja na Mipango ya Utetezi wa Adui.

Idi Amin alikuwa tayari ametumia nguvu kubwa kulinda sehemu za karibu za Uganda, hasa maeneo ya kusini na kati, ambako Tanzania ingeweza kuingia moja kwa moja.

Kwa JWTZ, kufuata njia ya moja kwa moja kungewaweka wazi kwa mashambulizi makubwa kutoka kwa jeshi la Uganda, ambalo lilijua vizuri maeneo hayo na lilikuwa tayari kuyatetea.

2. Kushirikiana na Vikosi vya Waasi wa Uganda.

JWTZ ilifanya kazi kwa karibu na vikosi vya waasi wa Uganda, kama vile Front for National Salvation (FRONASA) na Uganda National Liberation Army (UNLA).

Njia ya kupitia Sudan iliruhusu ushirikiano bora kati ya JWTZ na waasi hao, ambao walikuwa na ushawishi mkubwa katika maeneo ya kaskazini ya Uganda na waliweza kuwasaidia JWTZ kushinda haraka.

3. Kijiografia na Mbinu za Vita.

Maeneo ya kusini na kati mwa Uganda yana mito mikubwa na msitu wa Maramagambo, ambayo yangeweza kuchelewesha harakati za JWTZ.

Njia kupitia Sudan ilikwepa changamoto za kijiografia na kuruhusu JWTZ kuingia kwa kasi katika maeneo yasiyokuwa na ulinzi mkali, huku ikisababisha mshangao kwa majeshi ya Idi Amin.

4. Mkakati wa Kufunika Pande Nyingi (Encirclement).

JWTZ ilitaka kuhakikisha wanamgambo wa Idi Amin hawakuwa na nafasi ya kupangua au kupangilia upya jeshi lao.

Njia kupitia Sudan iliruhusu JWTZ kushambulia kutoka pande tofauti na kufunika Kampala kwa njia ya mkakati wa mtego wa pande nyingi.

5. Umuhimu wa Uungwaji Mkono wa Kijamii.

Kupitia njia ya Sudan, JWTZ ilipata msaada wa wenyeji wa Uganda wa kaskazini na kanda za karibu, ambao walikuwa na chuki kubwa dhidi ya utawala wa Idi Amin. Hii ilirahisisha operesheni za kijeshi.

6. Sababu za Kisiasa na Kidiplomasia.

Sudan, wakati huo, ilikuwa inachukua msimamo wa kutounga mkono utawala wa Idi Amin. Kuingia kupitia Sudan kulihakikisha JWTZ kuwa haitakumbana na vikwazo vya kidiplomasia kutoka kwa nchi hiyo.

Njia kupitia Sudan pia ilipunguza uwezekano wa nchi nyingine, kama Libya (ambayo ilikuwa mshirika wa Idi Amin), kuingilia haraka.

Kwa ujumla, maamuzi ya JWTZ ya kutumia njia kupitia Sudan yalilenga kufanikisha ushindi wa haraka kwa gharama ndogo, huku yakiwalinda wanajeshi wake na kuhakikisha mafanikio ya operesheni ya kijeshi dhidi ya utawala wa Idi Amin.

Ova
 
Sa
Ile vita ilipangwa na matajiri wa nchi za kiarabu na Marekani.

Palikua hakuna namna ya kuvikwepa kwa sababu lengo lilikua ni kudhoofisha na kuua ujamaa.

Baadae Alhaj Iddi Amini Dada aliamua kuweka na itikadi za Kidini na kuanza kuwaua Maaskofu na viongozi wa dini ya Kikristo waliokua wanamkosoa kwa kumwambia ukweli kuwa anakosea.

Lakini pia Nyerere angechelewa Mzuka wa Mapinduzi ungehamia Nchi zote za Afrika Mashariki hasa Tanzania yenye Rasilimali nyingi zilizokua zinagombanuwa na nchi za Kibeberu.
Nyerere asingeweza kuruhusu nchi yake ivamiwe na majeshi yaliyokuwa yanamtafuta Milton Obote ,Rais wa Uganda aliyepinduliwa.

Baada ya kufanya mapinduzi Shekhe Alhaj Iddi Amin Dada alikua na agenda kuu Tatu au nne:-
(1) Kujenga himaya ya Kiislam Uganda huku akiunga mkono harakati za kulifuta Taifa Teule la Israel.
(2)Kuwasaka maadui zake na waasi waliokua wamekimbilia Tanzania .
(3)Kujenga mfumo imara wa Kujamaa kwa kutaifisha mali zote za mabeberu na mafisadi na kuzigawa kwa waganda( Hii ilikua ni agenda nzuri iliyorudisha rasilimali za Uganda kwa wazawa mpaka leo)

Hata hivyo ni wazi kuwa nchi yoyote ambayo haikupita mapinduzi ya kijeshi inakuwa na siasa za kitapeli sana . Uganda ameokolewa na Mapinduzi ya kijeshi yaliyoasisiwa na Iddi Amini .
Wanasiasa ni machawa wa matajiri wa nchi za Magharibi na Waarabu. Ndio maana kule Booroondi rais anaacha makumi ya wapiga kura wake wakiwa wanakufa kwenye kwenye kifusi na kwenda kujipendekeza kwa Mabeberu wanaotembelea ardhi ya waliofukiwa ardhini.

Nilimsikiliza Musiba nikamuelewa alikua anaongea akimaanisha kinyume chake na zlimaanisha huku akiepuka kuuawa au kurudishwa kwao Booroondi au Kanyer.

1. Kuepuka Mashambulizi ya Moja kwa Moja na Mipango ya Utetezi wa Adui.

Idi Amin alikuwa tayari ametumia nguvu kubwa kulinda sehemu za karibu za Uganda, hasa maeneo ya kusini na kati, ambako Tanzania ingeweza kuingia moja kwa moja.

Kwa JWTZ, kufuata njia ya moja kwa moja kungewaweka wazi kwa mashambulizi makubwa kutoka kwa jeshi la Uganda, ambalo lilijua vizuri maeneo hayo na lilikuwa tayari kuyatetea.

2. Kushirikiana na Vikosi vya Waasi wa Uganda.

JWTZ ilifanya kazi kwa karibu na vikosi vya waasi wa Uganda, kama vile Front for National Salvation (FRONASA) na Uganda National Liberation Army (UNLA).

Njia ya kupitia Sudan iliruhusu ushirikiano bora kati ya JWTZ na waasi hao, ambao walikuwa na ushawishi mkubwa katika maeneo ya kaskazini ya Uganda na waliweza kuwasaidia JWTZ kushinda haraka.

3. Kijiografia na Mbinu za Vita.

Maeneo ya kusini na kati mwa Uganda yana mito mikubwa na msitu wa Maramagambo, ambayo yangeweza kuchelewesha harakati za JWTZ.

Njia kupitia Sudan ilikwepa changamoto za kijiografia na kuruhusu JWTZ kuingia kwa kasi katika maeneo yasiyokuwa na ulinzi mkali, huku ikisababisha mshangao kwa majeshi ya Idi Amin.

4. Mkakati wa Kufunika Pande Nyingi (Encirclement).

JWTZ ilitaka kuhakikisha wanamgambo wa Idi Amin hawakuwa na nafasi ya kupangua au kupangilia upya jeshi lao.

Njia kupitia Sudan iliruhusu JWTZ kushambulia kutoka pande tofauti na kufunika Kampala kwa njia ya mkakati wa mtego wa pande nyingi.

5. Umuhimu wa Uungwaji Mkono wa Kijamii.

Kupitia njia ya Sudan, JWTZ ilipata msaada wa wenyeji wa Uganda wa kaskazini na kanda za karibu, ambao walikuwa na chuki kubwa dhidi ya utawala wa Idi Amin. Hii ilirahisisha operesheni za kijeshi.

6. Sababu za Kisiasa na Kidiplomasia.

Sudan, wakati huo, ilikuwa inachukua msimamo wa kutounga mkono utawala wa Idi Amin. Kuingia kupitia Sudan kulihakikisha JWTZ kuwa haitakumbana na vikwazo vya kidiplomasia kutoka kwa nchi hiyo.

Njia kupitia Sudan pia ilipunguza uwezekano wa nchi nyingine, kama Libya (ambayo ilikuwa mshirika wa Idi Amin), kuingilia haraka.

Kwa ujumla, maamuzi ya JWTZ ya kutumia njia kupitia Sudan yalilenga kufanikisha ushindi wa haraka kwa gharama ndogo, huku yakiwalinda wanajeshi wake na kuhakikisha mafanikio ya operesheni ya kijeshi dhidi ya utawala wa Idi Amin.

Ova
mzee wangu Kichuguu ameeleza vizuri sana kwenye huu uzi. Pia kuna uzi wa Echolima1 nao una mengi ya kujifunza. Ahsante kwa mchango wako.
 
Ile vita ilipangwa na matajiri wa nchi za kiarabu na Marekani.

Palikua hakuna namna ya kuvikwepa kwa sababu lengo lilikua ni kudhoofisha na kuua ujamaa.

Baadae Alhaj Iddi Amini Dada aliamua kuweka na itikadi za Kidini na kuanza kuwaua Maaskofu na viongozi wa dini ya Kikristo waliokua wanamkosoa kwa kumwambia ukweli kuwa anakosea.

Lakini pia Nyerere angechelewa Mzuka wa Mapinduzi ungehamia Nchi zote za Afrika Mashariki hasa Tanzania yenye Rasilimali nyingi zilizokua zinagombanuwa na nchi za Kibeberu.
Nyerere asingeweza kuruhusu nchi yake ivamiwe na majeshi yaliyokuwa yanamtafuta Milton Obote ,Rais wa Uganda aliyepinduliwa.

Baada ya kufanya mapinduzi Shekhe Alhaj Iddi Amin Dada alikua na agenda kuu Tatu au nne:-
(1) Kujenga himaya ya Kiislam Uganda huku akiunga mkono harakati za kulifuta Taifa Teule la Israel.
(2)Kuwasaka maadui zake na waasi waliokua wamekimbilia Tanzania .
(3)Kujenga mfumo imara wa Kujamaa kwa kutaifisha mali zote za mabeberu na mafisadi na kuzigawa kwa waganda( Hii ilikua ni agenda nzuri iliyorudisha rasilimali za Uganda kwa wazawa mpaka leo)

Hata hivyo ni wazi kuwa nchi yoyote ambayo haikupita mapinduzi ya kijeshi inakuwa na siasa za kitapeli sana . Uganda ameokolewa na Mapinduzi ya kijeshi yaliyoasisiwa na Iddi Amini .
Wanasiasa ni machawa wa matajiri wa nchi za Magharibi na Waarabu. Ndio maana kule Booroondi rais anaacha makumi ya wapiga kura wake wakiwa wanakufa kwenye kwenye kifusi na kwenda kujipendekeza kwa Mabeberu wanaotembelea ardhi ya waliofukiwa ardhini.

Nilimsikiliza Musiba nikamuelewa alikua anaongea akimaanisha kinyume chake na zlimaanisha huku akiepuka kuuawa au kurudishwa kwao Booroondi au Kanyer.
Nationalist
 
Mkuu Kunguni kwanza kabisa Pole na stress za corona,

Tangu inchi ipate uhuru ni miaka takribani 17 pekee ilikuwa imepita, ndio tukakutana na janga la vita nchii ilikuwa haijakomaa na sidhani hata kama ilikuwa na akiba hata ya asilimia 40% ya kifedha.
Vita inahitaji fedha,

Na nchi yetu haikuwa na uchumi ya vyema ilikuwa ni nchi changa.

Na kwa wakati huo mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akihitaji watu wajitolee na ndio maana kuna watu walikuwa wanatoa ng'ombe, fedha, kusafirisha watu walio jitolea kwenda vitani, magari, na vitu vingine vingi.

Russia pia na Cuba zina mchango kwetu wakati wa hii vita,
Hivyo ilikuwa ni kweli uchumi ulishuka sababu tulitumia chakula kingi wakati wa vita na kama ujuvyo uzalishaji ulipungua,

sasa wewe kichwa maji unakuja hapa jukwaani kama kumtuhumu mwl, Utadhani yeye ndie aliesababisha hiyo vita.
Niongezee kidogo kuku support Tulisaidiwa na Umoja wa kuikomboa Uganda,Kagame akiwa upande wa Uganda,Ethiopia,Msumbiji na Nigeraia na ndio walituma mzinga wa BM21.Ila kusaidiwa sio lazima askari
 
Haukuwepo; na kama ulikuwepo labda ulikuwa wa siri sana kwa mimi askari wa cheo cha chini sana kuweza kuujua wakati huo. Wakati huo Tanzania ilikuwa upande mmoja na PLO kugombea uhuru wao kwa hiyo tulikuwa against Israel. Vita yote ile ilipiganwa na watanzania tupu akiwema Makongoro Nyerere, mtoto wa rais wakati huo. Tulikuwa na kanali mmoja pale ngome alikuwa anajua jinsi ya kupanga vita siyo mchezo. Huwa mara nyingi ninadhani ni Kanali Lupogo, lakini huenda jina lake halisi litatajwa na mtu mwingine huko mbeleni.
Kuelewesha watoto vichwa ngumu ni shida sana na nashukuru sana unajitahidi kuelewesha hawa wanao na tena tuseme wajukuu bila kukasirika wewe unaelezea ulichofanyia kazi wao wanaelezea walivyosoma.
Huyo uliyemtaja na mimi sina uhakika ila ngoja nikupe majina ya makamanda waliomtoa Iddi Amin kamasi na majina yao ya kimapigano.
Brig David Musuguri(Mutukula)
Brig Lupogo(Amphibia) sasa kikosi chake kilishawahi kaa ndani ya maji siku mbili
Brig John Butler Walden huyu alikuwa na asili ya Scotland kwa baba yake ila mama yake alikuwa wa Iringa
Kanal Tumbi---(radi) huyu alikuwa mkuu wa askari wa mizinga ndio maana akaitwa Radi.Huyu ndio mizinga yake ilinguruma huku daraja linajengwa kuvuka mbele wakaona askari wa amini wamekufa lukuki kwa hesabu zake kali.
Kanal Kitete-----(supersonic) huyu aliitwa hivyo sababu kikosi chake kilikikuwa kinasonga mbele kwa speed ya supersonic
Brg Yusuf Himid hayu alikuwa mzanzibari
Maj gen Abdala Twalipo ndio alikuwa mkuu wa majeshi
Conel Bayeke----huyu alikuwa natumia tarumbeta wakiingia mji flani akipiga adui anachanganyikiwa bado yuko hai.
Conel Laurian Makunda(Torpedo) huyu alikuwa mkuu wa jeshi la majini ndio maana akaitwa Torpedo
Conel-Nshimanyi
Brgi Mayunga(Mti Mkavu) huyu alipata sifa ya kuitwa mti mkavu sababu alikuwa hatembeI Na silaha kulikuwa na dhana kuwa sayansi ya kiafrica ya kisukuma alikuwa anatumia aliingia mjinI Kampala huku anatembea.
Brig Mike Marwa..
Brig Imran Kombe(Kamanda Ngono) sio ngono ya matusi ila kikosi chake ndio kilivuka mto ngono
Colonel Muhidin Kimario.....Huyu alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa vita aliacha ofisi akavaa magwanda na kuacha ujumbe kumuomba Raisi amsamehe amekwenda kupigania nchi yake
Major gen Ernest Mwita Kiaro.
Major Robert Mboma----Huyu ndio alikuwa mkuu wa ndege za kivita.Ndiye aliyekwenda kupiga bank ya Libya Entebe hadi Amini akasema walikuwa wachina maana hakuamini usahihi wa shabaha.Na ndege zetu zilikuwa hazitumiki hivyo hadi wakaziita ma fanicha ila sisi tulikuwa tunajua kutungua ndege za adui Amini alikuwa mjinga sana alikuwa na ndege lakini alikuwa hawajui kuzitumia ziliangushwa 22.
Kapten Msuya---- Huyu ndio aliyeweka funga kazi kumalizia vita baada ya kikosi chake kukutana na upinzani mpakani na Uganda na Sudan na kuwateketeza wote.
Kwa ujumla wapo wengi ambao hamuwezi amini walishiriki
Mfano Lowasa,Mzee Makamba,Makongoro Nyerere,Andrew Nyerere n.k
Vyeo nilivyoandika hapa wengine walikuwa hawajafikia lakini baada ya vita walipandishwa na wengine walipandishwa wakati wakiwa mstari wa mbele
VIJANA NI VIZURI MUULIZE MWASWALI MTAJIBIWA TU ILA MSI MKEJELI AU KU KEJELI WATU AMBAO WAMEPIGANA LIVE KAMA KINA KICHUGUU MAANA WENGINE MLIKUWA HAMJAZALIWA MTU ANAKUPA NONDO HALAFU UNAULIZA UMRI WAKE
 
VIJANA NI VIZURI MUULIZE MWASWALI MTAJIBIWA TU ILA MSI MKEJELI AU KU KEJELI WATU AMBAO WAMEPIGANA LIVE KAMA KINA KICHUGUU MAANA WENGINE MLIKUWA HAMJAZALIWA MTU ANAKUPA NDONO HALAFU UNAULIZA UMRI WAKE
Kwakweli mnafanya vizuri sana kuuelezea ukweli wa vita ya Kagera. Kinachosikitisha sana ni kwamba wanaomtetea Idd Amin wanaongozwa na vitu viwili tu Imani na Ujinga.

Wa ujinga huenda watabadilika lkn wa imani wataendelea ndiyo hulka yao dunia nzima kubadilibadili historia na kueneza propaganda ili hicho wanachobadili kionekane cha kweli...

Kwa bahati mzuri/mbaya hatutakuwepo lkn amini usiamini baada ya miaka 300 hao wa kusukumwa na imani watasema rais wa kwanza wa Tanzania alikuwa ni Mwinyi na ndiye anastahili kuitwa baba wa taifa na historia imebadilishwa kwa kuficha historia ya kweli kwa msaada wa Marekani!!!

Ndivyo walivyo ni mabingwa wa kufuta historia za watu kwa uzushi na propaganda, maeneo mengi sana wamefanikiwa na hatimaye kuzifuta kabisa jamii na historia zingine.

Ni taifa moja/jamii moja tu ndiyo imegoma kabisa kufutwa na hawa jamaa wanaoongozwa na imani yao kwa kila kitu. Lkn hiyo jamii cha moto inakiona japo na yenyewe ndiyo hasa kiboko yao, haikubali kufutwa!
 
Kuelewesha watoto vichwa ngumu ni shida sana na nashukuru sana unajitahidi kuelewesha hawa wanao na tena tuseme wajukuu bila kukasirika wewe unaelezea ulichofanyia kazi wao wanaelezea walivyosoma.
Huyo uliyemtaja na mimi sina uhakika ila ngoja nikupe majina ya makamanda waliomtoa Iddi Amin kamasi na majina yao ya kimapigano.
Brig David Musuguri(Mutukula)
Brig Lupogo(Amphibia) sasa kikosi chake kilishawahi kaa ndani ya maji siku mbili
Brig John Butler Walden huyu alikuwa na asili ya Scotland kwa baba yake ila mama yake alikuwa wa Iringa
Kanal Tumbi---(radi) huyu alikuwa mkuu wa askari wa mizinga ndio maana akaitwa Radi.Huyu ndio mizinga yake ilinguruma huku daraja linajengwa kuvuka mbele wakaona askari wa amini wamekufa lukuki kwa hesabu zake kali.
Kanal Kitete-----(supersonic) huyu aliitwa hivyo sababu kikosi chake kilikikuwa kinasonga mbele kwa speed ya supersonic
Brg Yusuf Himid hayu alikuwa mzanzibari
Maj gen Abdala Twalipo ndio alikuwa mkuu wa majeshi
Conel Bayeke----huyu alikuwa natumia tarumbeta wakiingia mji flani akipiga adui anachanganyikiwa bado yuko hai.
Conel Laurian Makunda(Torpedo) huyu alikuwa mkuu wa jeshi la majini ndio maana akaitwa Torpedo
Conel-Nshimanyi
Brgi Mayunga(Mti Mkavu) huyu alipata sifa ya kuitwa mti mkavu sababu alikuwa hatembeI Na silaha kulikuwa na dhana kuwa sayansi ya kiafrica ya kisukuma alikuwa anatumia aliingia mjinI Kampala huku anatembea.
Brig Mike Marwa..
Brig Imran Kombe(Kamanda Ngono) sio ngono ya matusi ila kikosi chake ndio kilivuka mto ngono
Colonel Muhidin Kimario.....Huyu alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa vita aliacha ofisi akavaa magwanda na kuacha ujumbe kumuomba Raisi amsamehe amekwenda kupigania nchi yake
Major gen Ernest Mwita Kiaro.
Major Robert Mboma----Huyu ndio alikuwa mkuu wa ndege za kivita.Ndiye aliyekwenda kupiga bank ya Libya Entebe hadi Amini akasema walikuwa wachina maana hakuamini usahihi wa shabaha.Na ndege zetu zilikuwa hazitumiki hivyo hadi wakaziita ma fanicha ila sisi tulikuwa tunajua kutungua ndege za adui Amini alikuwa mjinga sana alikuwa na ndege lakini alikuwa hawajui kuzitumia ziliangushwa 22.
Kapten Msuya---- Huyu ndio aliyeweka funga kazi kumalizia vita baada ya kikosi chake kukutana na upinzani mpakani na Uganda na Sudan na kuwateketeza wote.
Kwa ujumla wapo wengi ambao hamuwezi amini walishiriki
Mfano Lowasa,Mzee Makamba,Makongoro Nyerere,Andrew Nyerere n.k
Vyeo nilivyoandika hapa wengine walikuwa hawajafikia lakini baada ya vita walipandishwa na wengine walipandishwa wakati wakiwa mstari wa mbele
VIJANA NI VIZURI MUULIZE MWASWALI MTAJIBIWA TU ILA MSI MKEJELI AU KU KEJELI WATU AMBAO WAMEPIGANA LIVE KAMA KINA KICHUGUU MAANA WENGINE MLIKUWA HAMJAZALIWA MTU ANAKUPA NDONO HALAFU UNAULIZA UMRI WAKE
Asante sana kwa kuleta kumbukumbu zaidi. Wakati Kimario akiwa mkuu wa mkoa wa Mwanza alikuwa tayari ni Brigadier (siyo kanali); Chief Tactician wa kwanza pale ngome alikuwa Col Kitete kabla hajapewa command yake huko frontline.
 
Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)

Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita. Wanajeshi walikua hawatoshi?

Ahsante. 1979 ulikua una umri gani kaka?
wengine hii vita ilituachia majonzi uchungu na kumbukumbu za huzuni
 
Back
Top Bottom