Mkuu
Echolima
mbali na majeshi ya miguu mlitumia pia majeshi ya majini katika vita hii??
Vipi kuhusu majeshi ya anga nayo yalitumika sana au hatukua wazuri sana upande wa anga??
Mkuu,
Soma maelezo yote ndipo uulize unapohitaji. Kakuambia kwamba Mboma aliongoza vikosi vya ndege sasa unazidi kuuliza kama vile hukuelewa.
Swali lako la pili kuhusu majeshi ya majini lina mantiki kidogo na ninalijibu kama ifuatavyo.
Hatukuwa na lengo la kumpindua Idi Amin, bali kumfukuza mvamizi Idi Amin. Yeye alivamia eneo la Kagera, yaani north of Kagera river was annexed into Uganda as a new Ugandan district.
Sasa ukiangalia geography ya nchi yetu, bandari pekee kama tungetumia navy units basi tungetakiwa kutua Bukoba tu ambako ni kilomita 50 kutoka maeneo yaliyovamiwa yaani kutoka Kyaka.
Hivyo, kazi ya kwanza iliyofanyika November 1978 ilikuw akumfukuza toka ardhini mwetu na hivyo ililazimu kutumia infantry ya akina Echolima.
Echolima kafafanua vizuri, maana mimi kwa mara ya kwanza ndipo nimejua kwamba kumbe kuna majeshi yaliingilia Rwanda na hivyo geographically wavamizi wakawa wamezingirwa. Nimeielewa hili baada ya kuisoma hii story ya Echolima nikiwa na ramani ya Tanzania mbele yangu.
Kama tungekuwa tunataka tu kumpindua Idi Amin bila uchokozi wowote, basi hapo navy attacks yaani majini ingewezekana. Ingekuwa ni kiasi cha kuchukua meli kutoka Mwanza na kusogea kimyakimya hadi Entebbe na kuilipua Ikulu ya Entebbe anakopenda kukaa Rais wa Uganda.
Lakini hata hivyo, kumuua Rais wakati majeshi yake yapo bado haitoshi. Na hata hivyo angeweza kukimbilia Kampala na huko meli hazifiki.
Na mwisho ndicho kilichofanyika. Idi Amin alipinduliwa April 10, 1979 na akakimbia Uganda. Lakin majeshi ya Tanzania hayakuishia Kampala tu. Vita ilihesabika imekwisha June 03, 1979 siku Silas Mayunga na vikosi vyake vilipojikuta vimekanyaga ardhi ya Sudan huku wasudan wameshikilia bunduki wakidhani na wao wanavamiwa baada ya idi Amin.
Mayunga akasalimiana na wasudan na kisha akainua fimbo yake kwa askari wake kushangilia kwamba wameyafukuza majeshi ya Idi Amin hadi nje ya Uganda.
Nadhani kwa kifupi nimejibu swali lako.
Cc:
Jasusi,
Pasco,
Echolima,