Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza



Asante kwa kuniwahi swali langu ni kweli hata mimi niwehi kusikia kwa 'almando mjeda' mmoja ambaye alikuwepo na yeye kwenye war zone
kuwa lile daraja walipiga wenyewe Jwtz kwamba hata wakifail huko mbele majeshi ya amini yasivuke!!
 
Dah inatia hamasa
Asante kwa kuniwahi swali langu ni kweli hata mimi niwehi kusikia kwa 'almando mjeda' mmoja ambaye alikuwepo na yeye kwenye war zone
kuwa lile daraja walipiga wenyewe Jwtz kwamba hata wakifail huko mbele majeshi ya amini yasivuke!!
 
hili la kuandaa movie sidhan mkuu actors wenyewe ndio hawa wakina hemedi...mmmhh cjui,labda tunaweza.
La kitabu ndio la msingi.
 
Eco lima safi saana,tunasubili utupie nyingine
 
Kwa hii migogoro tuliyonayo baina ya rwanda na malawi,huoni kuwa vita sio suluhisho? Kwa sababu kama tukienda pigana na rwanda lengo ni nini?kuingia na kumtoa rais wa nchi hiyo?na kwa malawi vivyo hivyo? Na athari za kiuchumi kwa nchi yetu vp?
Kwangu mimi Vita sitaki kabisa maishani mwangu maana kuna vitu vinatokea kwenye uwanja wa vita ambavyo vikitokea kijijini mwako itakuwa ni janga kubwa sana na heshima inapotea kabisa mpaka kwenye familia yako hivyo Vita si suluhisho la matatizo bali Vita ni kufungulia matatizo ya Mfululizo mfano sisi tulifunga mikanda MIEZI KUMI NA NANE Lakini haikuishia miezi 18 iliendelea 18,28,na mpaka sasa hivi mimi binafsi bado naona makovu yaliyosababishwa na Vita ile,Kimaisha watu walipoteza maisha yao vitani huku waliacha pengo ambalo halizibiki hiyo pia si nzuri kifamilia,Kiuchumi iliadhiri sana watu walivaa nguo ambazo kwetu waliziita KAUNGUZA mpaka kupata tu sabuni inabidi Mgawiwe kwenye maduka ya Ujamaa au RTC Wakati ule.
Mimi naamini Jeshi letu si la kwenda kuwatoa Marais ambao hatuelewani nao bali ni JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA(JWTZ)Hivyo Diplomasia ni lazima ichukue mkondo wake.
 
Kwangu mimi fahari sana kushiriki vita katika maisha yangu hii ni nadra sana kwa watu,nimepata uzoefu mwingi sana katika uwanja wa vita nimepata Marafiki wengi huko Uganda na si hivyo tu bali nilijua kabisa kuwa VITA si LELEMAMA vita ni kujitoa AMA ZAKO AMA ZAO na ukipoteza nafasi hiyo Umekwisha hutaacha chochote cha kukumbukwa.Kitu ambacho nakikumbuka sana ni pale nilipoingia kwenye uwanja wa vita na kupokelewa na Maiti za askari wetu watatu waliouwawa na Bomu la kutupwa kwa Mkono najua umesoma habari hiyo nimeiandika kwenye sehemu yangu ya kwanza,hiyo ilinifanya mimi nijisikie vibaya na kuwa hiyo ilikuwa kama Balaa fulani kwangu,lakini kibaya zaidi tukio hilo lilinisababishia mimi kuacha kula zile nyama za makopo na nyama zingine hasa nikifikiria miili ya askari wetu wale waliolipuliwa na Bomu la kutupwa kwa Mkono,Nilishindwa kabisa kula chakula kwa siku nzima lakini Rafiki yangu mmoja Jmanne Mwandamba yeye alipigana pia vita huko Msumbiji alinishauri nivute Bangi ili niondoe hiyo hali nami nilikubali na alinisimamamia ili nivute na akaniambia nimeze ule moshi mpaka aone umetokea puani nami kwa kuwa nilikuwa na tatizo nilifanya hivyo mara mbili moshi ukatokea puani cha ajabu nilisikia mlio mkali sana Masikioni mwangu ambao haukukoma nikasikia usingizi mzito nikaenda kulala kwenye Handaki langu lilokuwa la watu wanne cha ajabu nilipoingia ndani kulala niliona najibana sana maana kwangu limekuwa dogo sana nilitoka ndani ya handaki na kwenda kulala vihakani sikujua nimelala saa ngapi lakini nimekuja kuamka saa mbili asubuhi watu wamenitafuta kwenye ngome yetu sionekani na nilipoamka niliweza kula chakula vizuri sana niliweza kufuta kopo nne za nyama na chupa mbili za maji ya machungwa baada ya hapo niliendelea kula bila shida lakini tatizo share yangu nilikuwa sishibi mpaka nile mbili ndiyo najisikia toka siku hiyo sikujaribu tena kuvuta bangi maana ilinifanya ni-risk maisha yangu kwa kulala nje ya handaki nafikiria kama ningeamuka usiku huo na kuja kwenye ngome yangu wasingejua ni mimi wangenipiga Risasi na kufa bure kabisa,Hivyo tukio hili nalo nalikumbuka sana katika maisha yangu ya VITANI.Kuhusu kupoteza askari hiyo ni kwaida kabisa si rahisi mnabadirishana risasi wewe lisikupate hata moja lakini kikubwa ni Ushindi katika MEDANI.
Mkuu Echolima,

Unazingumziaje operation chakaza iliyoanza tarahe 25 OCT 1978 na kumalizika 25 Jul 1979.

Kitu gani ambacho unakikumbuka mpaka sasa katika operation hiyo.

Ni kweli tulipoteza wanajeshi wengi katika mapambano.
 
Last edited by a moderator:
Historia ya pili lini? Na JWTZ walisaidiwa na nchi zipi ktk hii Vita japo kwa silaha na hata mafunzo, najua hazikosekani mkuu
Ni nchi nyingi ambazo walitupatia Vifaa kama vile USSR,CHINA na zingine ambazo zilikuwa Rafiki Nashukuru MUNGU sana pamoja na kuwa tulikuwa na tecknolojia ya hali ya chini Tuliweza kushinda vita fikiria kwenda-Ku-REC wanatumwa watu waende wakati mwingine watu waliweza kwenda zaidi ya kilometer moja wanapotoka huku wengine mnakuwa Roho juu juu mpaka warudi salama ndiyo mnashangilia lakini kwa Tecnolojia ya leo hakuna haja ya watu kupanda miti kufanya OP.
 
Hio usiite vita!
Hio ilikuwa ni fujo tu!
Na ghasia za watu wenye magobole!

Sasa hii ukiita vita na vietnam uite nini!?

Hebu wacha kufira maneno wewe!unajua nini kuhusu vietnam? au kwa sababu umeona movie za vita vya vietnam basi akili yako ndipo ilipo ishia sio? nadhani hata vita vya majimaji jipole wewe utaita ghasia eh?subiri tukianza kuwachapa wanyarwanda nakukamata nakurushia upande wa rwanda halafu nakupa madochi ya maana tu!
 
Mkuu wengi wetu tumefarijika sana mpaka leo bado nazikumbuka katuni za nduli kwenye magazeti na jinsi gani tulivyokuwa tunamchukia na kumhofu Alhaji Amin miaka hiyo!Pia natupa imani kuwa Bwana Kagame akileta upuuzi wake na atapata zisizoonekana!
 
"Kitu ambacho nakikumbuka sana ni pale nilipoingia kwenye uwanja wa vita na kupokelewa na Maiti za askari wetu watatu waliouwawa na Bomu la kutupwa kwa Mkono najua umesoma habari hiyo nimeiandika kwenye sehemu yangu ya kwanza,hiyo ilinifanya mimi nijisikie vibaya na kuwa hiyo ilikuwa kama Balaa fulani kwangu,lakini kibaya zaidi tukio hilo lilinisababishia mimi kuacha kula zile nyama za makopo na nyama zingine hasa nikifikiria miili ya askari wetu wale waliolipuliwa na Bomu la kutupwa kwa Mkono,Nilishindwa kabisa kula chakula kwa siku nzima lakini Rafiki yangu mmoja Jmanne Mwandamba yeye alipigana pia vita huko Msumbiji alinishauri nivute Bangi ili niondoe hiyo hali nami nilikubali na alinisimamamia ili nivute na akaniambia nimeze ule moshi mpaka aone umetokea puani nami kwa kuwa nilikuwa na tatizo nilifanya hivyo mara mbili"
-----------------------------------------------------------------------------------------
Komredi Echolima. Hongera sana. Viva ! Ila mengine ni siri za vitani. Si vizuri kuyaanika yote yanayotendeka uwanjani hadharani. Vita mara nyingi ni kipimo cha ustahimilivu na ukatili wa mwanadamu. Unajikuta ukifanya, kutenda au kushuhudia mambo ambayo huwezi kuthubutu katika hali ya kawaida. Hi ndiyo sababu mtu anapojitolea kujiunga na jeshi -hususan jeshi la ulinzi au kwenda vitani kuipigania nchi yake: huwa hiyo ndiyo biggest sacrifice ambayo mzalendo yoyote anaweza kufanya kwa ajili ya nchi yake. Somo kutokana na vita nyingi duniani ni kwamba "Msukumo wa kwanza wa kujiunga na jeshi la taifa unatakiwa kuwa uzalendo, na kwenda vitani ndicho kipimo cha uzalendo huo".
 
Echolima
Ahsante sana kwa huduma yako kwa taifa wewe na wenzako walio hai na waliotangulia mbele ya haki

Mimi sina shaka na habari yako. Nakumbuka alieleza kuhusu Capt Alexander Kaleya Mshana ndege yake iliyoangushwa musoma na JWTZ. Nakumbuka tukio hilo vema sana pale Musoma. Kulikuwa na connections kati ya wakazi waliotoka nyumbani kwao Alex Usangi ambao walijua ndugu yao kafariki next day pale Musoma.

Echolima, Brig Msuya ni mtu muhimu sana katika masimulizi ya vita kwasababu vitabu na habari nyingi za vitabu ni lazima anatajwa kwa namna moja au nyingine. Nadhani ni muhimu sana unapofikiri kuandika kitu kumuona au kumtumia yeye, yupo ni mstaafu

Ukimsikia Brig Walden(RIP) halafu ukakutana naye utashangaa sana. Ni mtu 'simple' friendly na huwezi kujua ndiye yule wa vita.

Echolima, nakumbuka bandari ya zamani ya musoma (tukiita old custom) pale kisiwani tuliona boti za kivita zikifanya mazoezi sana. Sijui kama zilishiriki kwa namna gani katika vita au zilikuwa kwa ajili ya kulinda ziwa?

Kitu kinachinishangaza ni kuwa sasa hivi ni karibu 33 tangu vita imalizike, kwa maana kuwa habari za jeshi ni declassified kwamba zinaweza kuwekwa hadharani au kuongelewa bila kuathiri usalama.
Sijui kwanini watu kama akina Kiwelu, Msuya ,Maneno na wengine hawajitokezi kueleza experience zao kama documentary au vita.
Pasco hamuoni opportunity ya habari hapo?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…