Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Muulize baba yako kwani yeye alikuwa kwenye saddle.Great thinkers tunazungumzia ya magamba wanavyo tumaliza.tatizo nimegundua huna mawasiliano na baba yako; hayo ndio yakuongea mkinywa kahawa. Nilitegemea utuambie meli ina nanga ngapi n.k usituvuruge

Mkuu inaonekana familia nzima ilimchukia babu baada ya yeye kuivurugia familia hiyo ndoto ya Magogoni.
 
Nyerere screwed Jumanne's plan to be a president, and if that plan would materialize... his son wouldnt be jobless and struggling to be a politician (in a jackass way)

Umenisaidia sana, mtaalam Janjaweed nakushukuru! Nilikua sijapata sababu ya kuridhisha dhidi ya upinzani wa huyu dogo kwa Nyerere. Mambo yaliyopo na yajayo yeye hayaoni kazi ni kukosoa historia tu! Ananiboa sana
 

Mkuu kwny jibu la mwisho hapo, je, Uganda ilikuwa haiwajibiki kulinda mipaka yake dhidi ya waleta chokochoko kutoka tanzania?
Haya naomba kuelimishwa,mosi, kwa wakati ule, msimamo wa OAU na UN ulikuwa unasemaje kuhusu kukabidhiana madaraka na demokrasia kwa ujumla?(maana post yako 1 pale juu umesema wali mtambua, wakati alipindua kuingia madarakani) pili, Obote aliingia madarakani kwa kupigiwa kura au naye alimpinduwa mtangulizi wake?
 

Mkuu kuwa makini.
Unachokiquote kwenye post yangu ya pili ni maoni yangu, ninasimamia maoni hayo katika namna ya kutaka kumaliza hoja hii ambayo kama nilivyoonyesha wasi wasi kwenye thread hii hii, kwamba sielewi ni kwa nini tunajadiri hii issue.

Kilinichofanya nikuulize wewe ni kitendo cha kutaka kuonyesha kwamba mwenzako anapotosha kwa makusudi wakati alikuwa anaelezea kilichotokea, alafu unareplace na ukweli ambao ni dhahiri kwamba umejikita kwenye kile unachokiamini au kukifiria, kama ulivyothibisha sasa, kwamba unachukulia maoni yangu yanafanya yakwako yawe fact. Point of correction dear Sir.
 
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.
 
William natamani uje bukoba uone makaburi ya babu zangu na ndugu zangu waliouwawa na majeshi ya Amini. Wewe uko huko mbali na mzee wako wala hukufiwa unakuja na hoja ya kibazaziiiiii............. siku ukifiwa undo utajua uchungu wa kufiwa.

Ta Muganyizi, nilitaka kukuongezea thanks juu ya ile like.
 

Kasikia JK alivo na chuki/hasira, asivompenda Mwl Nyerere so anajaribu kujipambanua humu kuwa naye hampendi Nyerere ili labda mkulu amwangalie,,kingine inaweza kuwa ile hali ya Nyerere kumdhibiti sana Baba yake,,lkn mbona still amenufaika sana na hicho alichopata mzee Malecela i.e kusomeshwa bure kwa kodi za watz nk?
 
Like I said, he is on the outside looking in. The question is: will "they" let him in?
 
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.
Jasusi, nafikiri wengi wenu mmesahau kitu kimoja...Je unakumbuka taarifa tuliyowahi kupewa na Field Marshall ES humu JF kuhusu nia ya kuandika upya historia ya Tanzania? Hiki kitabu kinatakiwa kiende sambamba na kile cha Mohamed Said cha kukosoa historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika. Hawa watu wanaamini kuwa kama wataweza kumcut down to size Mwalimu, basi watafanikiwa kuwainua watu wengine wamkaribie na ikiwezekana wamfikie na kumpita. Wakati Mohamed Said analilia wazee wake wa Gerezani, William anamlilia mzee wake wa Dodoma na kuna tetesi hiki kitabu kinaweza kutoka muda wowote kama kitakuwa hakijatoka tayari. Hizi mada anazoleta William ni katika kupima tu kina cha maji kabla ya kujitosa...na bado tutashuhudia mengi!
 
Sheria za vita haziruhusu tu kumuondoa adui kwenye ardhi yako bali kuweza pia kuondoa tishio la adui huyo na kumlazimisha kusalimu amri. Tanzania isingeweza kumuondoa Amin hadi mpakani na kuendelea kumuacha awe tishio. Katika vita - na hapa watu lazima watambue ni vita - anayeshinda ndiye anaamua terms of surrender. Tanzania haimkurudisha Obote; Obote alikuwa ni Rais wa Wauganda aliyepinduliwa na Idi Amin (kama watu wamesahau) na Obote alirudishwa kwenye nafasi yake (status quo). Sasa kama alipinduliwa tena hilo ni jingine lakini kama aliyempindua angekuwa tishio kwa Tanzania tungewajibika pia kumkung'uta.
 
William natamani uje bukoba uone makaburi ya babu zangu na ndugu zangu waliouwawa na majeshi ya Amini. Wewe uko huko mbali na mzee wako wala hukufiwa unakuja na hoja ya kibazaziiiiii............. siku ukifiwa undo utajua uchungu wa kufiwa.
Ta Muganyizi, huyu William hakuwahi kuusikia huu wimbo uliotungwa na Mayunga Ngata, naomba mwenye kuijua hii lugha atupe maana yake.

 
Last edited by a moderator:
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.

Jasusi,

..LOL!!

..jamaa ametaharuki baada kumwambia kwamba Nyerere alimtoa Iddi Amini "akampachika" Yussuf Lule.

..hiyo inavunja hoja ilee ambayo Mwalimu hasakamwa nayo.

..nimebahatika kusoma kitabu " The War in Uganda ", wanaelezea vizuri sana jinsi process nzima ya kupatikana kwa post-Amini government. Sikumbuki mahali popote pale ambapo Mwalimu alitia mkono wake.

..zaidi, kwa nguvu za kijeshi alizokuwa nazo Mwalimu, na jinsi Waganda walivyokuwa wakimtegemea, Mwalimu asingeshindwa kumuweka Obote madarakani. Ukweli ni kwamba Mwalimu hakuwa na nia hiyo.
 

NasDaz,

..baada ya Tanzania na Uganda kusaini mkataba wa amani wa Mogadishu hakukuwa na kikundi chochote kile cha Waganda kilichokuwa kikipata msaada wa kijeshi toka Tanzania.

..Yoweri Museveni anaeleza ktk kitabu chake kwamba walikuwa wamekata tamaa ya kumuondoa Iddi Amini madarakani mpaka pale Mwalimu alipotoa hotuba ya "uwezo tunao,..."
 
ndiye aliitia nchi katika janga la umasikini na madeni ambayo mpaka ulimwengu huu utakwisha hatuwezi kulipa

tutaendelea kulipa riba za deni,


sababu ni kumrudisha mkatoliki mlevi mwenzake madarakani

Mmh! Kweli udini utatumaliza, yaani udini unaweza ukamfanya mtu asifikiri kabisa. Pamoja na JK kukubali kupewa suti in exchange with our land, kamwe si haki kusema ni dini yake imemfanya ashindwe kufikiri. Madhaifu ya kiongozi hayatokani na dini au kabila lake jamani. Tukianza kufikiri hivi; kweli kwenye huu umaskini hatuwezi kuondoka.
 
Kama kuna kitu kitatusumbu sana ni hii historia mpya; tumeona hili kwa M. Said na simulizi lake ambalo sasa nina uhakika limepata mhusika mpya Vedastus Kyaruzi!
 

Umeongea vyema sana ila kuna sababu nyengine umeificha ambayo ni moja ya sababu kuu ya nyerere kumuondoa AMIN
 
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.

Jasusi,
Sina shaka yoyote kwamba miongoni mwa watu makini humu jamvini wewe ni mmoja wao. Mtu aliye makini hawezi kukurupuka na kusema kitu kisicho na ushahidi hata kidogo.....kwahiyo je, unaweza kunionesha post yangu angalau moja ambayo nimesema kwamba mimi ni anti-Nyerere?! Niwekee hiyo post, iwe ya leo au siku za nyuma ambayo nimetamka kwamba mimi ni anti-Nyerere!! Am very confidence kwamba hamna hiyo post na kama nimepitiwa basi ibandike hapa!! Nakiri wazi kwamba mara nyingi nimekuwa nikikosoa na baadhi ya mambo yaliyofanywa na Nyerere, mathalani hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/199759-nyerere-hakuwa-na-mapungufu-alikuwa-kiongozi-mbovu.html . Na sio Nyerere tu, hata Kikwete nimewahi kukosoa baadhi ya yale ninayoona amekosea, mathalani hapa: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/223514-happy-valentine-h-e-jakaya-mrisho-kikwete.html .

Haya nielimishe mkuu wangu, je kumkosoa mtu ni kuwa anti-him/her?! Ina maana unataka tuwe tunakubali na kushangilia kila tunaloambiwa kama inavyotokea tunavyoambiwa na vitabu vyetu vya kidini kwa kuhofu kwamba kupinga ni kukufuru?!

Niwekee hiyo post niliyotamka kwa maneno yangu kwamba mimi ni anti-Nyerere!!!!!
 

Mkuu Pan Africanism ni jambo jema sana, only shortsighted atapinga! Mtu yeyote mwenye hisia za Umoja hapendwi na Wazungu, watafanya chochote aonekane mbaya! Mifano: Gadaffi, Mugabe, Nyerere, nk! Only Waafrika hatujui kuwa mchawi wetu ni sisi wenyewe.
Back to topic kuhusu Vita ya Uganda, Idi Amin alianza chokochoko tangu mwaka 1972, mwaka mmoja baada ya kuchukua madaraka! Hizi chokochoko ziliendelea hadi alipivamia nchi yetu na kuimega mwaka 1978! Mimi nionavyo ilikuwa ni sahihi kumtoa huyu nduli kwa kuwa alikuwa ni threat kwa amani ya nchi yetu!
 

JokaKuu, mwalimu hakuwa mpumbavu na mjinga. Ni rais mpumbavu tu ndie angechukua uamuzi wa kumsimika Obote moja kwa moja. Bado Mwalimu alitaka kuushawishi umma kwamba aliingia Uganda kwa ajili ya kuitetea Tanzania kwahiyo endapo Obote angesimikwa moja kwa moja basi tuhuma dhidi yake kwamba alijiingiza Uganda kwa ajili ya kumtetea Obote zisingekuwa na ubishi kama ilivyo sasa. Pamoja na Yusuf Lule kupachikwa urais wa Uganda(kwa msaada wa Tanzania); Nyerere alifahamu kwamba itabidi uchaguzi ufanyike Uganda na alikuwa na uhakika kwamba swahibu wake Obote atashinda tu!!

By the way, nini kitakachonifanya nitaharuki baada ya kuambiwa kwamba baada ya Amin kuondolewa ni Lule ndie alipachikwa Urais?! Yaani ulitarajia hiyo kwangu iwe ni habari ngeni? Usinichekeshe wakati sijisikii kucheka hivi sasa! Also, kwanini mnakwepa kujibu hoja ya msingi.....kwamba, je wakati Obote allies wanavuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganda na kufanya jaribio la mapinduzi; serikali ya Tanzania ilifahamu au haikufahamu?! Ingewezekana vipi Waganda wafanye maandalizi ya mapinduzi ndani ya Tanzania na Tanzania isifahamu! Na kwanini hata baada ya Tanzanaia kufahamu kwamba Obote na watu wake walikiuka miiko ya ukimbizi bado watu hao waliendelea kubaki Tanzania?! Acheni mawazo mgando, binafsi simchukii Nyerere lakini sioni taabu hata kidogo kuyaelezea mafyongo aliyoyafanya! Hata kama mtaona ni chuki dhidi ya Mwalimu, hayo ni yenu lakini ukweli bado utabaki pale pale.....katu siwezi kuisoma historia sawa na ninavyosoma maandiko ya dini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…