Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?


mbona tuliilaani israel kuwa imemsjambulia nchi huru ya africa alipogomboa mateka wake entebe huku iddi amin akiwa adui mkubwa wetu?
 


- Kwenye hii thread ninakukubali kwamba wewe ni Great Thinker, saafi sana nice and clear bila matusi wala jazba, ndio njia pekee ya kutoa elimu kwa sisi tusioelewa na tunaouliza, kuliko wanaojifanya wanajua kumbe maneno yao wenyewe na matatizo ya taifa yanawashitaki kwamba hawajui wanallolisema! ha! ha! ha!

William.
 

William
Amin alishageuka kansa kwa watanzania ilikuwa ni lazima aondoke; kama angekuwa na vita vya maneno tu vita visingetokea; kitendo chake cha kuvamia na kuuwa watanzania wasio na hatia hicho kilikuwa si cha kufumbia macho; Mwl. Nyerere hakuwa Raisi legelege; na lazima ukumbuke Amin alijivunia wadhamini wake Ghadaf wa Libya na alishatoa kauli ataichukua Mwanza; hizo ni kauli zake, kama ambavyo haikuwa kosa kwa Dunia kumuondoa Hitler basi pia halikuwa kosa kwa wanajeshi mahiri wa Tanzania chini ya Jemedari wao Nyerere kumuondoa Idd Amin; William hizi propaganda za kumpaka Mwl. Nyerere matope hazitafua dafu; wapo wanasiasa na majemedari wetu ambao walishiriki kikamilifu kwenye vita vile waulize watakueleza visa vya Idd Amin.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 

- I mean kupiga taifa lingine na kuingilia mpaka ndani ya mipaka yake ni makosa ksiheria za kimataifa, na hadithi ya Marehemu Binaisa, kuhusu nia na madhumuni ya Mwalimu na ile vita ni tofauti kabisa na hii habari yako, betwen Lule na Binaisa, wote waliambiwa wazi kwamba nia ni kumrudisha Obote, ndio maana na wao wakamuondoa very fast kumhakikishia Mwalimu kwamba hawakubali pilcies zake kwa nchi yao.

- Kumpiga Amin mpaka ndani ya nchi yake kumetugharimu na mpaka leo bado tunalipia, ni wajibu wetu wananchi wenye uwezo wa kufikiri kuuliza kuhusu hizi failed policies!, ambazo zingine physically zinatuumiza mpaka leo, ambapo wahusika hawapo!

William.
 

Idd Amin aliwatendea waganda mambo mengi ya kiuonevu na si waganda pekee bali hata wageni kama waAsia n.k na ndiyo maana tulipata support kubwa uganda. Amin alitangaza ardhi ya tanzania kuwa sehemu ya uganda na kuweka bendera ya uganda. Kitendo cha Gadaf kumsaidia Idd Amin kilikuwa na malengo ya kuendeleza udikteta barani Afrika.
 

- Mkuu ulianza vizuri lakini mpaka hapo mwishoni ndio ukaanza kuonyesha makucha yako, naomba nikwambie hivi, mimi ninapokuwa na swali la msingi kwa taifa langu ninauliza bila kujali nani yupo upande wa pili, ninasikia vilio kila mahali na hii thread lakini bado inaendelea tu, sasa mntaka nini wote humu tuwe mabendera wa kufuata upepo wenu tu?

- Propaganda? wananchi wakiulzia wamefikishwaje hapa wewe unaita ni propaganda? Yaani mna hasira kweli mkiulizwa maswali ya kweli na ya muhimu kwa taifa, badala ya kutumia nafasi kuelimisha wanaouliza ni kwa sababu mnajua kwenye nyoyo zenu kwamba kuna makosa yalifanyika, lakini kwa vile mlishaamua kwamba makosa ni ya sasa tu, baaasi kila anayeuliza either sio mzima, au ana agenda, au propaganda, ila mkuliza nyinyi kuhusu serikali ya sasa basi mna hoja nzito sana mna akili sana, I mean tupo tulipo sasa kutokana na tulikotoka!

- JF sio chombo cha kuongelea mazuri isipokuwa ni chombo cha kukosoa ili kusaidia kila anayekosolewa, sasa hizi elimu zenu mlizofundishwa kukosoa tu bila kukosolewa ni elimu gani hizo? Kama hoja ni za propaganda na hazina mashiko kwa nini zinafilia kurasa zote hizi? Na kwa nini zinawavuta sana maana mimi thread ambazo naona hazina mashiko huwezi kuniona huko, sasa nyie mnaolalama kila wakati na bado mnazidi kuja kutoa maoni ya vitisho, ni nini hasa kinawasumbua?

- Mnaonekana mmezoea kuiskia nyimbo za upande mmoja tu, please tuacheni watu tukate ishus hapa, swali lipo very clear kwamba kulikuwa na ulazima gani wa kuingia mpaka ndani ya nchi na kuliacha taifa likiwa na madeni yasiyolipika? Kama ni swali la propaganda then kwa nini unakuja kujibu propaganda great thinker?

William.

William.
 

William
Kinachotugharimu leo hii si gharama ya vita vya Uganda ni ufisadi wa viongozi wetu msikwepe ukweli; silaha nyingi zilizotumika kwenye vita vilikuwa ni mkopo kutoka Russia na madeni hayo yalishasamehewa; kama unataka kujua ukweli tafuta gharama halisi ya vita na gharama ya ufisadi utaona ukweli wa maneno; gharama za ufisadi ni kubwa zaidi ya mara 10 ya vita vya Uganda.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
dah! Kupitia huu Uzi nimejifunza mengi saaaana! Sasa naanza kumwamini mwalimu wangu aw History A level mwaka 2000-2002 Ambaye kila siku akiingia class alikuwa anasema Nyerere was selfish, incompetent na asiyeambilika. Wadau endeleeni kumwaga data na Kama kuna watu wataelezea vizuri habari za villagelization ntafurahi sana kuliko kumpa Mtu sifa ambazo alikuwa hastahili mwaka 1999 tulizuiwa hata kufanya graduation za kuhitimu o level eti tukio kwenye maombolezo ya Baba aw Taifa kumbe baba mwenyewe mbinafsi
 

- kama unataka kuongelea ufisadi then fungua thread yake, lakini kujaribu kuingiza hoja za propaganda hapa ndio ufisadi wenyewe, siamini kwamba Russia ilitusamehe madeni ya ile Vita, ambayo wao walikuwa wanauza silaha kwetu na kwa adui at the same time, tunaambiwa tulikuwa na Viongozi genius enzi hizo, lakini walikubali tukadanganywa na Russia wao wakiuza silaha huku na kule,

- Sasa leo tunawauliza was it fair kujiiingiza kwenye ile vita mpaka kufikia madeni yote tunayolipa mpaka leo? Mnasema ni propaganda, oooh maswali ya chuki za binafsi, REALLY?

William.
 
Kwanini nchi za kiislam zilimsaidia IDDI AMINI? ukipata jawabu hapo utajuwa kwa nini Nyerere alianzisha vita na AMINI, kisha watanzania wakafanywa "wapumbavu" kutungiwa nyimbo za ajabu ajabu.

Orodhesha hapa nchi za kiislam zaidi ya Libya zilizomsaidia Amin.
 

- Nimewahi kukaa chini na Binaisa na Lule, story zao ninaziamini sana maana zinakaribiana sana na za viongozi wetu ambazo huwa wanzitoa kwa siri sana, kwa kuogopa kuonekana wana tatizo na Mwalimu.

- Binaisa anasema aliambiwa wazi kwamba yeye ni RC tu wa Uganda sio rais, yaani Mkuu wa mkoa wa Tanzania wakati ule, Lule alipojaribu kuwa objective anasema aliwekwa under house arrest, halafu mnakuja watu wazima hapa mnataka kutudanganya na kututisha na maneno mengi uongo uongo as if wote hapa ni watoto wadogo, kama mmezidiwa hoja ni kukaa pembeni tu! Mnatutisha na mavitabu yaliyoandikwa na ma-compromise, mtu unasoma kitabu ukurasa wa kwanza tu umeshaelewa kila kitu kitabu gani hicho?

- Waliotyaka kuandika vitabu vya ukweli si walufukuzwa au hujui? I mean wakuu wacheni tujadili taifa letu kama kawa!


William.
 
Fikra zangu zilikuwa Kama za w malecela wakati niko form .2 ila baada ya kusoma sana na kutafakari kwa kina nikagundua Nyerere alikuws sahihi katika jambo hili.tumvumilie huyu malecela kwani akili zake bado ni za form 2
O

- REALLY? Umekuja kwenye thread iliyoandikwa na mtu mwenye akili za darasa la 10? ha! ha! ha!

William.
 
Naomba kuuliza. Hivi ni watanganyika tu wanaowajibika na PAN-AFRICANISM?
 

Hizo zilikuwa propaganda za amin ili ku justify uvamizi wake kwa TZ na alifanikiwa kumuingiza mkenge gadaffi ambaye alimuunga mkono lakini gadaffi alikuja kugundua badae kuwa amin was a liar na ndo maana gadaffi alimtaka radhi nyerere vilevile nyerere alimrudishia gadaffi mateka wote wa kilibya na gadaffi alifarijika kwa kuipa TZ mafuta mengi buree!
 

William
Wewe ni msomi kila uandishi una agenda na kila agenda utumika kama propaganda machine; kama uliwahi kuongea na Binaisa na Lule hilo hatuwezi kulithibitisha wote ni marehemu (R.I.P) ukweli wa hilo unalijua wewe binafsi; labda nikuulize tu mbona umelitoa leo hii na si jana; "halafu mnakuja watu wazima hapa mnataka kutudanganya na kututisha na maneno mengi uongo uongo as if wote hapa ni watoto wadogo, kama mmezidiwa hoja ni kukaa pembeni tu"! Hapa hatutishani tunadebate kutafuta ukweli wa hoja; katika mada yako unadai vita vimetugharimu hadi leo ninachotaka kukwambia tu kabla Mwl. Nyerere hajaachia madaraka alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha madeni yetu na Urusi na China yanasamehewa kitu ambacho alifamikiwa kwa kiasi kikubwa; nimegusia ufisadi ili ujue nini kinachotugharimu watanzania umejaribu kuhusisha gharama vita ndio inayotugharimu umejaribu kukwepa ukweli watanzania wanajua nini kinachowagharimu; Mkuu unapo debate ni wigo mkubwa yataingia yaliyomo na yasiyokuwamo umesoma hilo kwenye humanities; nimesema hizo ni propaganda za wazi najua unaelewa vyema siasa na propaganda vinamix bila matatizo. HIZI NI PROPAGANDA KWANI ULIANZA NA BIAFRA NA SASA VITA NA IDD AMIN HIVI WEWE KAMA MTANZANIA HUNA HATA MOJA ZURI LA KUMJADILI NYERERE? NAAMINI YAPO MENGI SANA ALIYOYAFANYA NYERERE AMBAYO YALIKUNUFAISHA NA YANAENDELEA KUKUNUFAISHA HADI LEO HII. Tuendelee na hoja

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
mbona tuliilaani israel kuwa imemsjambulia nchi huru ya africa alipogomboa mateka wake entebe huku iddi amin akiwa adui mkubwa wetu?
ninalokumbuka ni kuwa Nyerere alilaan Islael kwa kuiteka na kuikalia palestina.
 

Mkuu William,

Sijakaa na Binaisa au Lule. Lakini nachofahamu kuwa vita vya kukomboa Kagera na kumuondoa Idd Amin vilichukua kama miezi sita (October 1978 - April 1979). Vilikuwa ni vita fupi.

Baada ya vita Tanzania ilichukua jukumu la kukaa Uganda kwa miaka miwili. Na miongoni mwa majukumu ya miaka miwili hiyo ilikuwa ni mikakati ya kurudisha Obote.

Nyerere alikuwa ana deni kubwa na Obote. Mwaka 1971 kulikuwa na harakati za kupindua serikali ya Obote. Hivyo Obote hakutaka kwenda kwenye mkutano wa jumuia za madola uliofanyika Singapore. Nyerere akamshawishi kwenda na matokeo yake Obote kupinduliwa. Tanzania ilimpokea na kumwifadhi kama rais. Na juhudi zilifanyika kumrudisha.

Uwezekano mkubwa kama tulivyoona vita vya Iraq, gharama kubwa zilikuja katika juhudi za kumrudisha Obote madarakani na sio kwenye vita vya kukomboa eneo la Kagera au Kumuondoa Iddi Amini.

Kumrudisha Obote ilikuwa ni kazi kubwa. Kwanza alikuwa hakubaliki na waganda wenyewe. Na kwenye uchaguzi hakufanya vizuri.
 

Jipu haliwezi kupona bila kutolewa ile mbegu iliyo kwa ndani...
 
Asolutely wrong Bill. Baada ya Amin alifuata Lule ambaye aliondolewa na kurithiwa na Binaisa.
Binaisa alikuwa 'arrested' na akina Tito Okello.
Ndani ya serikali ya Binaisa Museveni alikuwa waziri wa Ulinzi na kisha kuhamishwa wizara hiyo.
Kabla ya Obote kushinda uchaguzi, uganda ilikuwa inaongozwa na kamati ya muda.

Aliyemondoa Obote ni Majeshi yake. Hadi hapo Lule na Binaisa walikuwa hawana uwezo dhidi ya Obote.
Kusema ya kuwa Binaisa na Lule walimuondoa Obote ili kumkomoa mwalimu na siasa zake si kweli na nadiriki kusema ni upotoshaji wa 'short cut' ili hukumu ipatikane hata kwa mashitaka ya kuunga unga.

Obote aliporudi mara ya pili alifanya mauaji ya raia wengi hasa jimbo la kati. Hata alipotorka na kufika mpakani mwa Kenya, Nyerere hakukubali arudi Tanzania.

Sababu kubwa ya Amin kuvamia Kagera kwa mujibu wake ni madai kuwa Kagera ni sehemu ya Uganda. Alipofanikiwa kupora mali, kuvuruga maisha ya watu wa Kagera, Amin alipandisha bendera ya Uganda na kumteua mkuu mpya wa Wilaya ya Kagera.

Vita ya Kagera inaweza kuwa ni 'failed policy' kama unavyodai. Ni vema basi utueleze ingekuwa wewe upo katika nafasi ya kutoa maamuzi unadhani nini ungefanya wananchi wako wakiwa wameuawa na kufukuzwa katika eneo lao na kipande cha nchi kuchukulia?
 

Chama,

Vita viliingiza gharama kubwa sana kiuchumi. Katika Hotuba ya mwisho wa mwaka 1979, Nyerere alisema kuwa itachukua miezi 18. Baada ya mwaka akasema miaka 18.

Kuhusu madeni ya Urusi na China sina uhakika nayo. Lakini sehemu kubwa matumizi ya jeshi haipo kwenye zana za kivita. Warusi na wachina walitudai kwenye zana za kijeshi.

Lakini wakati wa vita vya Kagera na Uganda, serikali ilibidi iongeze idadi ya wanajeshi. Na vita vilipokwisha wote walipewa nafasi katika majeshi ya ulinzi na usalama. Hivyo kulipa mishahara pekee yake ilikuwa ni kazi kubwa.

Vilevile majeshi ya Tanzania yalikaa Uganda kwa miaka miwili. Gharama za kukaa kule zilikuwa za kwetu. Vilevile zana zingine za kivita zilitoka katika nchi nyingine kama Yugoslavia. Hivyo hoja ya kuwa tulisamehewa haina mpango.

Vilevile manunuzi mengine ya zana na mahitaji ya kivita yalitumia reserve na mikopo ambayo ilitakiwa kutumika kwenye shughuli za maendeleo. Hivyo misamaha ya warusi na wachina haikutoa unafuu wowote hule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…