Ninachojua mimi juu ya vita ya TZ na Uganda:
Nyerere alikuwa mpigania amani Afrika, alisaidia mataifa yote ya kusini mwa Afrika kujikomboa ndo maana Nchi kama Mozamique, Zimbabwe, Angola, Namibia Afrika ya Kusini zilikuwa na makambi yao Tanzania. Sababu ya vita ni AMIN kuudhika uamuzi wa Nyerere kumpokea Obote baada ya kupinduliwa mwaka 1971. Alikuwa anachukizwa na uamuzi wa Nyerere kumpokea OBOTE na wafuasi wake waliokimbilia TZ. Akaanza kuwatafuta tangu mwaka huo huo wa 1971, aliambiwa wamejificha kanda ya ziwa, wale wenye kumbukumbu watakumbuka Amini alipiga bomu Mwanza mwezi Mei 1971, na bomu liliangukia pale chuo cha ualimu Butimba na mabaki ya bomu hilo yapo hadi leo kwenye geti la kuingilia chuoni.
Kwa hiyo, chokochoko za kuwatafuta wabaya wake Tanzania ziliendelea mpaka pale aliposikia kuna kikosi cha ukweli maeneo ya Kagera (akina Museveni) kinajiimarisha, akaamua kwenda kuwafyeka Mwaka 1978. Weee, lilikuwa kosa hilo kwa Nyerere na kwasababu AMINI alikuwa anatoa maneno machafu kwa Nyerere, Mwalimu aliona hakuna njia ni kumfyeka.
Kwanini aliendelea mpaka kumng'oa? jibu lipo wazi, baada ya JWTZ kuyaondoa majeshi ya AMINI katika ardhi ya Tanzania, yalisimamana na kutoa taarifa kwa Nyerere (Amiri Jeshi mkuu) kwamba kazi tumeimaliza. Sasa Nyerere kwa kushauriana na makamanda waliona kumuondoa tu katika ardhi ya Tanzania isingesaidia angekuja tena na kuua watu na askari wetu pia, ndipo wakati ule makamanda wa Tanzania akina Musuguri, Mayunga na wengineo wakamwambia mzee, turuhusu tuendelee... Nyerere akasema ruksa .. kazi ikaanza mpaka Harua kule kwenye mpaka na SUDANI.
Mambo mawili ya kukumbuka:
(1)Baadada ya AMINI kung'olewa, kivita Nyerere alipasa kujitangaza yeye ndiye mtawala wa Uganda, lakini akasema hapana, uongozi wa nchi alipewa Maj.Genearal MSUYA wa Tanzania ambaye aliongoza Uganda kwa karibu wiki moja au mbili( siku mbuki vizuri) baadaye Nyerere akmwambia Obote rudi kachukue nchi yako. Msuya akaambiwa afanye maandlizi ya kukabidhi madaraka kwa OBOTE (kuapishwa) Msuya akasema yeye hajui anahitaji msaada, ndipo akapelekwa mzee Paul Sozigwa( wenye kumbukumbu wanaweza nisahihisha) mambo yaka wekwa sawa OBOTE akaapishwa
(2) Choko choko za AMIN zilifanana sana na choko choko za MAKABURU wa Afrika Kusini. Walichukizwa na kitendo cha Nyerere kuwaweka wapigania uhuru kwa nchi za Zimbabwe (Rhodesia), Namia(Western Rhodesia) na Afrika Kusini yenyewe. MAKABURU wliitafuta sana MAZIMBU pale Morogoro na kambi ya farm 17 pale Nachingwea mkoa wa Lindi. Wale waliowahi kuishi Nachingwea miaka ile ya 70's watakumbuka jinsi ndege za makaburu zilivyokuwa zinasumbua. shule zote na nyumba zote za mjini Nachingwea zilhitajika kuwa na mahandaki. Wakati hule mizinga ya kutungulia ndege ilikuwa imewekwa juu ya mlima ulipo pembeni kidogo ya mji unaitwa mlima NAMBAMBO ( sasa juu ya mlima huo pamejengwa kanisa)
Yamepita, Tugange ya jayo, tumwache mzee wetu apumzike kwa amani. Ameen