chama,
Mkuu wangu umeonyesha mengi sana mabaya ya Idd Amin ambayo bado hayajengi hoja ya kwamba Idd Amin hakupendwa sana na wananchi wake maana hawa wote ulowaweka ni watu waliokuwa wakimpinga Idd Amin. Sijasema Idd Amin alikuwa mtu mzuri, tena basi kwa mifano yotye hii uloitoa inaonyesha jinsi jamaa huyu alivyokuwa mnyama lakini mnakataa sii yeye aliyeivamia Tanzania pamoja na unyama wake wote ila Nyerere ndiye alitaka kumrudisha Obote. Nikawauliza, sasa kama Nyerere alitaka kumrudisha Obote ilikuwaje baada ya kumwondoa Idd Amin walipewa Yussuph Lule na kisha akaingia Binaisa badala ya Obote?.. Na hata Obote aliporudi Uganda aliingia kupitia uchaguzi wa kura ndipo alipochaguliwa kuridi madarakani na yeye akaanza mauaji kama Idd Amin na pengine zaidi lakini hutasikia watu hawa hawa waandishi wakimsema sana kama Idd Amin tena basi wanamchukia Museveni zaidi japokuwa naye aliwaokoa toka makucha ya Obote. Jiulize!
Kifupi kwa mtu makini kama mimi sipendi kusoma habari zinazoandikwa na watu wa west hasa pale wanaposisitiza kwa mfano picha ya juu wanasema Idd Amin alikuwa akiua watu and I quote - The Bodies of most of Amin's victims were clandestinely sdisposed of or mutilated beyond recognition - halafu tunaonyeshwa picha za maiti za watu ambao wanaonekana vizuri tu, mara ati Archbishop aliuawa mara tu baada ya makutano hayo tukionyeshwa bastola kiunoni mwa Idd Amin, lakini tena mwandishi anadai mchungaji huyo aliteswa sana kabla ya kuuawa. karibu kila unaposoma unakuta habari zinagongana zenyewe ingawa kweli Idd Amin alikuwa mnyama lakini kuongeza chunvi mara nyingi huharibu habari nzima.
Nitasema hivi Idd Amin alikuwa mshenzi sana tena wa kuchosha lakini bado itabakia ukweli kwamba alipendwa sana na wananchi wake labda nikupe mfano wa Hitler. hakuna kiongozi aliyependwa na wajarumani kama Hitler japokuwa hakuna kiongozi tunayemchukia dunia nzima kama Hitler. Kupendwa kwake na Wajarumani hakuwezi kuondoka kwa kutazama picha ama hisia zetu sisi kwa kuweka mtiririko wa maovu yake bado ukweli utabakia Hitler alipendwa sana na Wajarumani.