Chama,
..asante kwa michango yako.
..tatizo la NasDaz ni kwamba amekwama na hoja zake za mwaka 72 kabla ya mkataba wa amani wa Mogadishu.
JokaKuu,
Sijakwama mkuu wangu, lakini endapo unaamini kwamba nimekwama hapo basi ni kwavile tu naamini hapo ndipo chanzo cha yote.
..kuna maelezo kwamba baada ya mkataba wa Mogadishu hali ya mpaka wa Tanzania na Uganda ilikuwa shwari mpaka miaka 8 baadaye Amini alipotuvamia.
Nanukuu: "
Beyond the Mogadishu Agreement, Nyerere and Amin met at the 1973 OAU summit in Addis Ababa and signed a pledge that Amin would stop demanding that Nyerere evict Obote from Tanzania. However, the cold war between Amin and Nyerere did not subside, for 1975 Nyerere refused to attend the OAU summit in Kampala, and waged a campaign against Amins election as the OAU Chairman."
Ukiangalia nukuu hiyo hapo juu, utagundua wazi kwamba hata baada ya Mkataba wa Amani bado hali hakuwa shwari kivile.Bila shaka hakuna ubishi kwamba hakuna vita duniani inayoanza from knowhere. Hivyo, ingawaje mpakani hali ilikuwa shwari, lakini akilini mwa Nyerere, Obote na Amin halaikuwa shwari! Ni akilini mwa mahasimu hawa ndimo mlimozaa vita ya mwaka 1978. By the way, ikiwa kweli Nyerere alikuwa na nia ya dhati ya Mkataba ule, sijui alikuwa na sababu gani za kuendelea kuwa na kinyongo na Amin!!Na kwavile umeshasema kwamba baada ya mkataba ule hali ilikuwa shwari, then bila shaka unachomaanisha ni kwamba pamoja na kwamba hali ilikuwa shwari lakini Nyerere hakutaka tu kuwa pamoja na Amin!!! Aidha, kususa kwa Nyerere kuwa pamoja na Amin kulianza chini ya wiki mbili tu tangu kusainiwa kwa makubaliano yale kwani October 21, 1972 Nyerere alisusa kuhudhuria sherehe za mapinduzi ya Somalia kwavile tu Amin angewepo kwenye sherehe hizo!! Si hivyo tu, tangu 1962, Somalia and Tanzania zilianzisha uhusiano wa kibalozi lakini uhusiano huo ukawa mbovu mara baada ya Makubaliano ya Amani kati ya Amin na Nyerere!! Haya sasa niambie wewe....kweli Nyerere alikuwa na nia ya dhati na makubaliano yale au aliamua tu kusaini kwa shingo upande ili asidhihirishe nia yake in public?!
....uthibitisho kwamba Nyerere alishaachana na mipango yake ya kumuondoa Amini ni udogo wa vikosi vya JWTZ vilivyokuwa mpakani na Uganda wakati Amini anatuvamia.
Huo hauwezi kuwa ni uthibitisho, labda ni kwavile hawakufahamu Amin angefanya wakati gani uvamizi wa kijeshi. Nukuu nyingine hii hapa: "Indicative of Nyereres restraint was his order closing Obotes training camp at Handeni.
Overt support for Ugandan exiles ended. But Nyerere privately let it be known that anti-Amin activities could go on, discreetly and quitely." Nukuu hiyo inaonesha wazi kwambaa lengo la Nyerere na Swahibu wake Obote lilikuwa palepale ila ambacho alikifanya NYerere ni kuacha kum-support Obote kwa uwazi bila shaka alichelea kuonekana anavunja makubaliano ingawaje kimsingi tayari alishayapa kisogo makubaliano hayo!! Nukuu nyingine hii hapa: "Obotes operations from 1972 to 1978 focused more on intelligence gathering and small covert operations designed to keep a very low profile." Nukuu hiyo inaonesha wazi kwamba kumbe hata baada ya makubaliano ya amani 1972, bado Obote aliendeleza "Operations" zake frm 1972to 1978 kabla ya vita. Na kwavile Obote alikuwa anahifadhiwa na kufadhiliwa Tanzania, basi sina shaka yoyote kwamba operations hizo zilikuwa na mkono wa Nyerere na hivyo kudhihirisha wazi madai yako ama si sahihi au hayana grounds!
...Pamoja na majeshi yake kuondolewa ktk ardhi ya Tanzania, Iddi Amini aliendelea kutushambulia kwa kutumia ndege na hakusitisha vitisho vyake kwamba atarudi na kuchukua ardhi ya Tanzania.
..Mazingira hayo hapo juu ndiyo yaliyopelekea Tanzania kuamua kumtoa madarakani Iddi Amini. Tangu tumuondoe Iddi Amini madarakani hakuna serikali ya Uganda ambayo imekuwa hostile to Tanzania.
Kwa hali ilivyokuwa hasa kwa kuzingatia nukuu nilizotoa, utakuta kwamba Nyerere na Amin wote walikuwa tatizo lakini endapo nitaulizwa ni nani anayepaswa kubebeshwa lawama zaidi basi sitasita kusema kwamba ni Nyerere hasa kwavile alichukua role ya Principal War Architect.
NB: Nukuu zote hizo ni kutoka kwenye andiko ambalo Mzee Mwanakijiji na Chama wanalikubali. And, as far as you're from the same boat then i've no doubt kwamba hata wewe na Jasusi mnalikubali andiko hilo: The Tanzanian Invations Of Uganda: A Just War?