Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ukiangalia kwa undani makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya utawala wa dikteta Bashir Al-Assad nchini Syria hayatoi matumaini mema kwamba endapo yatafanikiwa kumng'oa Assad siku za usoni za Syria zitakuwa njema chini ya utawala wao mpya, makundi yanayompinga Assad ukiondoa Wakurdi nusu yake ni makundi ya kijihadi yenye msimamo mkali. Haya makundi yakishika madaraka ina maana Syria itageuzwa taifa la kidini rasmi na inaweza kugeuka changamoto nyingine kubwa si kwa raia wa ndani tu bali hata nchi majirani ikiwemo Israel.
Familia ya Assad ambayo ni alawites , tawi la Washia lenye msimamo tofauti na sehemu kubwa ya Waislamu ikiwemo kuruhusu matumizi ya pombe na kutoamini kabisa wanawake kuvaa hijabu ni takwa la lazima la dini wameiendesha Syria kama taifa jumuishi la imani zote kwa muda mrefu japo chini ya utawala wa chama kimoja cha Baath, hakuna uhakika kama waasi watakoingia kumrithi Assad watadumisha taifa jumuishi la Syria lisilo la kidini au lenye mrengo wa upande mmoja zaidi wa kidini na hapo ndipo migogoro itapozidi na kuharibu mambo kabisa.
Ni kweli kihistoria Syria chini ya utawala wa familia ya Assad haujawahi kuwa rafiki sana wa Israel lakini pia haijawahi kuwa utawala wa uadui wa kiwendawazimu sana kuipasua kichwa Israel, mara nyingi imejizuia au imejiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Israel. Mtihani mkubwa ni kwamba Syria ya Assad imekuwa kibaraka wa Iran wakati wote ambaye ni adui mkubwa wa Marekani na Israel.