Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Compare na Ulaya na Nchi Tajiri sawa, ila Uchumi wa Syria haujawahi kuwa mbaya kama nchi za Ki Africa ama south Asia huko. Walikuwa na Uchumi wa wa kati kama Nchi za ulaya Mashariki hivi, Gdp per capita kufika $11,000 si uchumi wa kitoto.
 
Compare na Ulaya na Nchi Tajiri sawa, ila Uchumi wa Syria haujawahi kuwa mbaya kama nchi za Ki Africa ama south Asia huko. Walikuwa na Uchumi wa wa kati kama Nchi za ulaya Mashariki hivi, Gdp per capita kufika $11,000 si uchumi wa kitoto.
Hizi hapa unazofanya ni propoganda sasa, kwamba Syria ilikuwa imeikarabia GDP per capita ya Russia kwa sasa??
GDP per capita ya Syiria kabla ya vita kuanza ilikuwa inacheza kwenye $2000.
 
Uko sahihi mkuu, ila je huyo Israel na USA angewezaje kukusanya waasi kama sio watu wa ndani ambao wanampinga Assad!?
Tunarudi pale pale badala wakae watulie kujenga taifa wanafanya tofauti.
Shida inaanzia ndani kabla ya kwenda nje,na humo humo ndani ndio majamaa wametumiwa upenyo kufanikisha yao.
 
Hakuna anayefadhili makundi ya msimamo mkali(ya kigaidi) kati ya Israel au Marekani, katika hao waasi wamegawanyika wapo wenye msimamo wa kawaida pia na Wakurdi, hao ndio wanapata msaada wa Marekani. Balaa litakuja pale ambapo wale wenye msimamo mkali ndio watawapiku wenzao.
 
Waarabu huwa wanashindwa kupiga mahesabu ya kina aisee.

Badala mkubali kukaa chini ya bendera moja ya utawala mujenge taifa mnaleta utofauti unaowagawanya na kuharibu nchi na kuipasua kipande kipande.

Hili la Syria na Libya halina tofauti sana.
Hao waasi wa Syria hata sio wasyria wenyewe ama waarabu, wengi ni mercenaries toka Ulaya na mataifa mbalimbali, hawa jamaa walipotea kwa kasi Vita vya Ukraine vilipoanza, Walienda kusaidia Ukraine naona sasa wamerudi.
 
Hizi hapa unazofanya ni propoganda sasa, kwamba Syria ilikuwa imeikarabia GDP per capita ya Russia kwa sasa??
GDP per capita ya Syiria kabla ya vita kuanza ilikuwa inacheza kwenye $2000.
Ilikua $2,700 pia GDP yake haina tofauti na ya Tanzania.
Ila beyond Syria economic crambling nahisi kuna mengi sana nje ya ufisadi na uchawa uliosema mkuu.
 
Hao waasi wa Syria hata sio wasyria wenyewe ama waarabu, wengi ni mercenaries toka Ulaya na mataifa mbalimbali, hawa jamaa walipotea kwa kasi Vita vya Ukraine vilipoanza, Walienda kusaidia Ukraine naona sasa wamerudi.
Sahihi kwa namna moja kaka ila kwa namna nyingine raia wa Syria pia wapo miongoni mwa waasi.
 
Namkubali sana Assad, tatizo lake ni moja tu ambalo umeshalitaja.
Kwa maoni yangu, ingewezekana wale waasi wange stopishwa tu, sema ndiyo vile anaponzwa na marafiki
 
Boss hao waasi jina lao walikua ni Al Qaeda, Waka badili jina wakaitwa Al Nusrat na sasa hivi wamebadili tena jina.

Hii website ya Israel iki report kuwasaidia

Na hii video maarufu Bibi akiwa tembelea kuwa Julia hali hospitali

View: https://youtu.be/5doeBEyjVDg?si=ZCxGx9vqT7DOiBFb
Israel hawafichi kuwasaidia ila ni nyie tu mnaoishi kwenye Denial ndio hamtaki kuamini huu ukweli.
 
Sahihi kwa namna moja kaka ila kwa namna nyingine raia wa Syria pia wapo miongoni mwa waasi.
Wapo waasi wa Syria Makundi mbali mbali kama Waasi wa Kikurdi, Yapo makundi ya Sunni, Waasi wanaosaidiwa na Uturuki etc.

Ila Unapoongelea Isis ama Al Qaeda hao ni full mercenaries hawajawahi kuwa Nchi moja hao, wengi wazungu ndio maana wanaoenda kuvaa nguo zinazoziba mwili mzima na kuacha macho.

Vita ya Ukraine ilipo tokea wengi Wali report na magwanda yao ya Isis wakawa jeshi la Ukraine bila kubadili uniform. Nikukumbushe tu na picha

Hii picha ilipatikana live kabisa kwenye TV jamaa anahoji wanajeshi wa Ukraine mmoja akapita na magwanda yake ya Isis.

Hao ambao wame chukua Allepo ni HTS kwa jina jengine Al Nusra branch ya Al Qaeda.
 
Ilikua $2,700 pia GDP yake haina tofauti na ya Tanzania.
Ila beyond Syria economic crambling nahisi kuna mengi sana nje ya ufisadi na uchawa uliosema mkuu.
Tanzania tunaishi na GDP ya 2700 ya bila tabu nyingi sana kwa sababu chakula ni rahisi na watu wanakula mihogo, mahindi, n.k Sasa Syria wao wanaishi zaidi kwa ngano na mchele wa kununua kutoka nje, Syria haiwezi afford ufisadi mkubwa kama mataifa mengine tajiri sana ya mafuta mfano Saudia, Qatar n.k
 
Israel ni IQ kubwa, hawa Waarabu IQ zao bado sana, labda Emirates na MBS wa Kingdom of Saudi Arabia.

Waliobakia wote IQ zao ni za kunywea Kahawa tu na kufukuzana na Ngamia Jangwani.
 
Syria bila Assad ni janga kubwa Kwa dunia Kwa mara ya Kwanza naisapoti Iran na Russia kumsaidia Assad
Waasi wanajaribu kuiteka Hama tokea jana wamerudishwa nyuma na wamezungukia upande wa pili wa Mji reinforcement inapelekwa kundi kubwa la Waasi linaelekea huko.

Kiongozi wao Abu Mohamed Al Jolaani kasema baada ya Hama ni Homs,na baada ya Homs ni Damascus yenyewe, wakati huohuo maelfu ya Wanamgambo wa Kishia wanazidi kumiminika kutoka Iraq na Beyond ili kuja kuisaidia Regime ya Assad.


Al Jolaani anasema kaachana na Al Qaida lakini anataka Taliban Style Government.

Nawaonea huruma Wanawake wa Syria Arab Republic.
 
Mkuu ulikua hauna haja ya kutoa maelezo yote haya.
Maana sijakataa ila niliongeza maelezo kuwa waasi asilia ya raia wa Syria wapo.
Kiufupi waasi sio hao mercenaries peke yake.
Hii ndio point kuu mkuu.
 
Ila kuna mengi aside from ufisadi.
 
Iran ya Washia ndio wanaoiimarisha familia ya Assad madarakani Syria wasiondolewe na Wasuni, bila msaada wao ingekuwa vigumu sana kina Assad kudumu madarakani huo muda wote kwa sababu Shia na Alawites ni minorities.
Ila jeshi la Syria wengi ni Sunni
 
Naifahamu historia ya Al-Qaeda vizuri sana mkuu, Al-Qaeda ilichipukia kutoka makundi ya Mujahideen yaliyokuwa yanapambana kuuondoa uvamizi wa USSR nchini Afghanistan miaka ya 1980 na kipindi hicho yalikuwa yanapewa msaada wa silaha, pesa na intelligence kutoka US kupambana na uvamizi wa USSR, tatizo USSR na ujamaa walipong'olewa Afghanistan Al-Qaeda walienda rogue na full extremists.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…