Wazungu wanalalamika hata kwa vitu vidogo Sana. Unashangaa Uingereza Mafuta kuuzwa Tsh 5,000 huku nchi Masikini ya Tanzania yakiuzwa Nusu yake Tsh 2,700?
GDP per Capita ya UK ni zaidi ya Tsh 120,000,000/= ( $ 54,000) kwa Mwaka.
GDP per Capita ya Tz ni Tsh 2,400,000/= ( $ 1,086) kwa Mwaka
Sasa Kati ya Uingereza nchi Tajiri ambayo kipato Cha mtu ni mara 51 ya kipato Cha Mtu wa Tanzania,ni Nani anayeumia Mafuta yakiuzwa Tsh 5,000 kwa Uingereza na Tsh 2,700 kwa Tanzania?
MFANO MDOGO
Ukiambiwa chagua Kati ya vitu vifuatavyo:
A) Upewe $ 54,000 kila mwaka lakini uwe unanunua Mafuta kwa $ 2.6 kwa Lita au;
B) Upewe $ 1,089 kila mwaka lakini uwe unanunua Mafuta kwa $ 1.1 kwa Lita.
Tupe Majibu.