Vita vya ukraine huenda vikamfanya putin kufuata nyanyo michael gobachev 1991

Neno "Huenda" limekinajisi kichwa chote cha uzi wako.

Impossible future tense.
 
... umoja na utangamano ndani ya Urusi unaenda kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya vita; kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa na kijamii yanaenda kutokea ikiwamo utawala wa mkono wa chuma kufikia mwisho.

Naiona Urusi ya kidemokrasia mbeleni huko; Urusi isiyotawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja au kakikundi ka wachache bali matakwa ya wananchi; Urusi isiyokuwa na "rais wa maisha" bali Urusi yenye viongozi waliowekwa na watu kwa ajili ya watu na sio madikteta yaliyojitawaza kuwa marais wa maisha.

Huyu fashisti amejigeuza waziri mkuu na rais mara kadhaa kabla ya kuona huo ni usumbufu hatimaye akabadili katiba atawale milele kwa raha zake. Hili chaka aliloingia hatoki salama.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
FOsn5ExVEAc8G0o.jpg
 
Uchumi wa Urusi unamilikiwa na familia ya Putin.

Nimepata kuwafahamu hawa kina Putin kwenye familia yake kuna Generali wa jeshi tajili sana huwa anakuja kila mwaka kuwinda Tanzania, lile group huwa likija unaweza kuipata taswira halisi ya ukwasi walionao, na huwa wanasafiri na cash ya hatari, sijui hata hizi sheria za kiwango cha pesa za kusafiri nazo zinawalenga baadhi tu ya watu?
Dah!!!
Duma na Orgachies ni sauti ya 3 ndani ya Urusi ndiyo maana Ma- Orgachi wengine hawaelewi Merode ya wimbo unaochezwa,😀
 
... umoja na utangamano ndani ya Urusi unaenda kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya vita; kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa na kijamii yanaenda kutokea ikiwamo utawala wa mkono wa chuma kufikia mwisho.

Naiona Urusi ya kidemokrasia mbeleni huko; Urusi isiyotawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja au kakikundi ka wachache bali matakwa ya wananchi; Urusi isiyokuwa na "rais wa maisha" bali Urusi yenye viongozi waliowekwa na watu kwa ajili ya watu na sio madikteta yaliyojitawaza kuwa marais wa maisha.

Huyu fashisti amejigeuza waziri mkuu na rais mara kadhaa kabla ya kuona huo ni usumbufu hatimaye akabadili katiba atawale milele kwa raha zake. Hili chaka aliloingia hatoki salama.
Toka Lin marekani wanachi ndyo wanamuweka madarakani raisi pale refer uchaguzi WA 2017 ivi nyie watu mmesomea kweli au mnapelekwa pelekewa Tu labda nikwambie Tu Putin hajiuzulu wala hakuna kitakacho ibafikisha RUSSIA
 
Hakuna kitu kinafirisi kama vita, Warussia watuulize Tanzania hadi mawaziri wa Nyerere walikuwa na Kaunda Suit tatu tatu tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] yani unatoa reference ya vita yenu ambayo hata hamkujiandaa mliendaa kama vichaaa unaisi urusi ni Tanzania
 
Wewe jamaa umevunja mbavu zangu hadi Waziri makuu soko nne alikuwa na oair tatu za viatu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] yani unatoa reference ya vita yenu ambayo hata hamkujiandaa mliendaa kama vichaaa unaisi urusi ni Tanzania
Unajifanya unaijua sana urusi as if umezaliwa Moscow, urusi ana historia chafu ya kushindwa vita, ww1 mjapani alimchakaza, 1939 Finland alimchakaza kishenzi, hata ww2 asingemuweza Hitler sema mgermani alikuwa anapigina maeneo mengi
 
... umoja na utangamano ndani ya Urusi unaenda kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya vita; kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa na kijamii yanaenda kutokea ikiwamo utawala wa mkono wa chuma kufikia mwisho.

Naiona Urusi ya kidemokrasia mbeleni huko; Urusi isiyotawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja au kakikundi ka wachache bali matakwa ya wananchi; Urusi isiyokuwa na "rais wa maisha" bali Urusi yenye viongozi waliowekwa na watu kwa ajili ya watu na sio madikteta yaliyojitawaza kuwa marais wa maisha.

Huyu fashisti amejigeuza waziri mkuu na rais mara kadhaa kabla ya kuona huo ni usumbufu hatimaye akabadili katiba atawale milele kwa raha zake. Hili chaka aliloingia hatoki salama.
Endelea kusubiri embe chini ya mpapai
 
Gorbachev aliamini ndani Urusi nzima kuna mbadala wake, Putin aamini ikiwa kuna mbadala wake ndani ya Urusi.
moja ya Ma- Orgachi ambaye mali zake zimetaifishwa alinukuliwa akisema:, mataifa ya magharibi yanatuonea bure hawaijui nguvu inayoendesha Kremlin.
hii inatoa picha kwamba putin ndiye konda na ndiye dereva.
Ma- orgachi ndio watakaomtoa Putin madarakani maana hawatakubali wawekewe vikwazo na ulaya vinavyopelekea wao kufilisika.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] yani unatoa reference ya vita yenu ambayo hata hamkujiandaa mliendaa kama vichaaa unaisi urusi ni Tanzania
Swala sio kujiandaa, swala ni gharama na Urusi kwa uchumi wake hawezi kupigana muda mrefu na vikwazo juu ndio maana anaomba msaada China.
 
Kinachoenda kuimaliza Russia kuliko kitu kingine chochote ni uchumi wake ambao unaenda kusambaratika wote.

Export capability yake inaenda kushuka vibaya hadi chini ya 10% na hawataweza kutumia akiba kubwa waliyonayo ya dola bilioni 640 (Foreign Exchange Reserve) pia kuna mabilioni yao mengine yamekuwa frozen na Marekani na mwisho wa siku Moscow Stock Exchange nayo itafungwa kwa sababu hata sasa tayari inasuasua.

Kuna kitu watu hawawezi kuelewa labda kwa sababu ya uelewa mdogo au ushabik tu hakuna kitu kibaya kama vikwazo vya kiuchumi na afadhali mpigane vita mambo yaishe lkn usiwe umewekewa vikwazo na mataifa yenye nguvu kiuchumi duniani.

Angalia leo hii jinsi Iran anavyohaha ili ule mkutano wa 6 + 1 uweze kufanyika kwani kufaulu kwake matokeo yake ni wao kuondolewa vikwazo walivyowekewa na Marekani ambavyo vinanyonga uchumi wao vibaya.

Iran amejaribu kukwepa makali ya vikwazo kwa kutumia the third party arrangement lkn imekuwa na changamoto kibao kiasi kwamba huyo mtu wa kati anataka kunufaika karibu kuishinda Iran yenyewe ambaye ndiye mwenye mali kiasi kwamba Iran anaona afadhali akae mezani na Marekani wayamalize ili awatue hawa watu wa kati.
 
Muda utazungumza, ila huo uwezekano ni mkubwa sana
 
Back
Top Bottom