Vita ya Akili Unde (AI) ni kubwa kati ya matajiri

SaintErick

Member
Joined
Aug 7, 2013
Posts
95
Reaction score
61
VITA YA AKILI UNDE (AI) NI KUBWA KATI YA MATAJIRI
Kwa sasa bidhaa adhimu katika sekta ya teknolojia ni Akili Unde (AI) ambayo ukiitazama kwa umakini utaona kua dunia ijayo ni dunia itakayoendeshwa kwa Akili Unde karibu kila nyanja ya maisha ya binadamu. Hii ni fursa na ni changamoto mpya miongoni mwa wanaotaka kutawala dunia ya baadae.

Hili limeibua ushindani usio na usawa na kuleta vita za chini kwa chini kati ya wahusika wakuu. Kisa cha Elon Musk kujitoa Open AI na baadae kutaka kuinunua kwa njia isiyokubalika kulichochea mzozo mkubwa kati ya Elon Musk (xAI) na Sam Altiman (Open AI). Open AI walimburuta Musk mahakamani na hilo likawa limemleta Mark Zuckerberg wa Meta katika vita ya Akili Unde. Na hii inaonesha kuna watu wana nia ovu na AI. Kwanini Elon Musk amekua katika msururu wa kesi hivi karibuni?

 
Huyu kijana Sam Altiman (Open AI), yupo speed ya Ngiri mkia juu,

Nimeona Chatgpt/Open AI, unaweza kuipa password na username za mfumo wako(website fulani) na ikakufanyia majukumu yako ndani ya website safi kabisa. Huyu kijana anatisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…