Vita ya Aleppo inaanza tena

Vita ya Aleppo inaanza tena

Ukweli ni kwamba haya ni matokea ya vita ya urusi na Ukraine,na hili ni pigo kubwa kwa urusi maana Syria hasa Aleppo ilikuwa alama muhimu ya uhodari wa urusi mbele ya ulimwengu wote..,watu wengi na mataifa mengi walijua nguvu ya urusi na ushawishi wake kupitia Syria kwa Jinsi alivowachaza waasi,Nina hakika Putin hapati usingizi Kwa siku hizi hasa akiona kazi iliyompa heshima ulimwengu kote ikiaguka kirahisi namna hii, mbaya zaidi Hana msaada mkubwa wa maana kuasaidia kuokoa jahazi maana yeye mwenyewe ana fupa limemkwama kooni🏃🏃🏃
 
Vita nchini Lebanon ilipokuwa inaelekea mwisho, mzozo mwingine mkubwa umezuka Mashariki ya Kati - au labda si mpya sana. Waasi wa Syria wanaopinga serikali wameanzisha mashambulizi ya haraka dhidi ya jiji kubwa zaidi nchini, Aleppo. Tayari wanadhibiti vijiji kadhaa na wameendelea hadi barabara kuu ya Damascus-Aleppo.

Kwa mara ya kwanza tangu 2020, mapigano makali yamezuka nchini Syria. Vikosi vya serikali vinatoa upinzani dhaifu. Waasi wanasonga mbele kwa kasi, na vikosi vya Assad vimeshindwa kuwazuia, vikijiondoa vyenyewe maeneo

Wakati wa mapigano karibu na Aleppo, mshauri wa kijeshi wa Iran, Jenerali wa IRGC Kiyumars Pourhashemi, aliuawa. Shughuli mpya za waasi zimechochewa na kushindwa kwa Hezbollah na Israeli na kupelekwa tena kwa vikosi vya Urusi vilivyokuwa syria Ukraine. Dikteta wa Syria Bashar al-Assad amepanda ndege haraka kwenda Urusi kwa mashauriano na Putin.

Kulingana na ripoti ambazo hazijathibitishwa, makumi ya wanajeshi wa Urusi kutoka kwa "PMC ya Wagner" wameuawa wakati wa mashambulizi ya waasi, na baadhi , ya silaha na usafiri wa Urusi zimekamatwa. Waasi wanabomoa picha za Bashar al-Assad na alama zinazohusishwa na Urusi. Wametangaza kuwa maadui wao wakuu ni WaIrani na Warusi, wanaounga mkono utawala wa Assad.

View attachment 3165135
Ndg hapo kuna usuni na ushia, Iran ni mashia na assad ni Shia inabidi ujue hilo,na kama Syria itaanguka mikononi mwa masunni basi naiona serikali ya Iraq itakavyoangushwa muda si mrefu maana Iraq masunni nao wamechoka na kuna mapigano huko, dunia inaenda kujiform upya,
 
Unaijua vizuri siasa ya middle east? Please kabla hatujaanza midahalo em nenda kwanza kajifunze uko mitandaoni at least ujue baadhi ya key issues vinginevyo unaajenda yako please be well informed before engaging! Itakupunguzia kutokuelewa vitu vingi kama nia ni kuelewa
Jambo gan ni Bora kuliko uhai wa mtu? kama unaamin ni sahihi hao ndugu kuuana bas hizo lawama msiend zitupa Kwa Israel au Marekani au Urusi , wazibebe hao unaona wapo sahihi kuuana
 
Wananikumbusha ile 2014 hadi 2016 enzi za Khalif Dr. Abu Bakar Al-Bagdad, mtume wa mwisho Duniani enzi zile akiongoza ISIS walivyokua wanachinja watu huko Allepo na Maeneo ya Iraq.
 
Hivi nyinyi hamuwezi kujadili dini bila kuingiza kejeli na kashifa za kidini?
Hivi watz tuna matatizo gani?
Hahaha kashifa iko wapi hapo, hao ni MAGAIDI wana Twangana. Sisi tusiishie humu nikataka kufahamu tutasaidiaje, wewe usha daka dini.
 
Saa hizi yanauana wenyewe hutawasikia wazee wa mtambani wakikemea
Hahaha tunataka tuone maandamano wakipinga kuuwana, majuzi hapa waliandamana wakipinga Israel kuwatandika HAMAS=MAGAIDI, wakidai eti wanauwa wanawake na watoto. Mi niliwauliza mbona CCM wana UVCC, na UWT, mnauhakika gani kama HAMAS hawana branch kama hizo? wananitukana.
 
mtambani waendelee tu kunywa al khasus, ya syria hayawahusu
Wana double standard sana, al khasus, na shisha zao wanazipenda, kuwasaidia hawataki. Sasa sijui watasemaje, Wamarekani ndio wanawaua au Europe? hawakosi wa kumsingizia hawa.
 
Hahaha kashifa iko wapi hapo, hao ni MAGAIDI wana Twangana. Sisi tusiishie humu nikataka kufahamu tutasaidiaje, wewe usha daka dini.
Hizo chuki zako zilizo kujaa mpaka mkunduni hazitokusaidia kitu zaidi ya kukuletea maradhi ya moyo.

Na usishangae hao unao waita magaidi na wavaa kobanzi ndo watakuolea mabinti zako ili tuone kama na wajukuu wako utawaita magaidi na wavaa kobanzi.
 
Ww tangu Urusi imeanza kushambulia imesha sikia wameshambulia Shule, hospital,kambi za wakimbizi, mashirika ya UN,masoko na kama anavyo fanya Israel?
Nenda kafanye research mwenyew Kila kitu kilipostiwa humu , sio kulipia tu walikuwa wanapora na kukanya watu wakiwa kwenye magari Yao
 
Mfadhili mkubwa wa vita vya syria Qutar.. Japo kila nchi hapo zina maslai yake..
*

Russia hawez kukubali bomba la gas lipite syria liende Ulaya..
Nimesoma comments nyingi kwenye huu uzi,wengi hawajui kwanini Russia yuko pale na kwanini marekani na west wako pale,wewe umeongea point ambayo ndio sababu kubwa ya kinachoendelea .
 
Back
Top Bottom