JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tetesi kutoka msimbazi ni kuwa kiungo wa Simba,Clatous Chotta Chama na Kocha Mkuu Pablo Franco walirushiana maneno kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Aprili 30, 2022 katika mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga.
Inaelezwa tukio ndilo lililisababisha Pablo kumtoa Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Bwalya, pia katika mchezo dhidi ya Namungo FC, jana Mei 3, 2022, Chama hakuwepo hata kwenye benchi la timu hiyo.
Kutokana na hali hiyo hapo ni wazi wawili hao hawawezi kufanya kazi pamoja na mmoja lazima aondoke, inaaminika kuwa kinachombakisha Pablo mpaka sasa ni kwa kuwa kuna uwezekano wa Simba kukutana na Yanga kwa mara nyingine katika Kombe la FA.
Kama atashindwa kuingia fainali ya FA ni wazi kuwa safari yake itauwa imewadia mapema zaidi ya inavyoelezwa, pia viongozi wa Simba wanaona ameshindwa kuinua viwango vya wachezaji wengi msimu huu.