Vita ya Haji Manara dhidi ya wachambuzi wa mchongo

Yule jamaa anaongea kweli seme nyinyi mashabiki mnataka msikie kila siku taarifa nzuri hata kama timu yako imefanya kosa unataka asifie ndio maana timu zetu miaka yote ziko pale pale hakuna timu ambayo imewahi kuchukua kombe kimataifa
 
Sisi wenzenu wakati huo tunasikiliza mipira na wachambuzi redioni, tulizoea kusikia maneno ya kiswahili kama...

Kumimina majimaji au kumimina majalo
KUpiga kombora
Kulala yombo
Kupelekwa markiti
Kupigwa/piga darizi
Kupigwa telo
Kugawa vyumba
"banana chopu".
 
Miaka ya RTD tulikuwa na watangazi mpira ambao kwa leo hii tunaweza kuwaweka kwenye kundi la wachambuzi japokuwa hawakuwa wakichambua sana zaidi ya kutangaza mpira na kuelezea nini kimefanyika au nini kilitakiwa kifanyike "in real time".

Leo hii tuna "the so called wachambuzi" ambao utawakuta mitaa fulani wakiangalia "post-match analysis" ya BBC Sport, Sky Sport, na "clubs' TV" na kuandika vitu vya kwenda kutudanganya wasikilizaji/watazamaji wa vipindi vya "spoti" .

Nawakumbuka wakina Ahmed/Omar Jongo, Charles Hillary, Halima Mchuka na wengineo.

Namkumbuka Ben Kiko niliwahi mtania kule kwake Miyuji kuwa hawezi tangaza mpira, akanitangazia mpira kwa dakika 5, ilikuwa balaa.
 
umesahau kutandika reli
 
umesahau kutandika reli

Naam, ipo misemo mingine mingi nimeiacha wadau muongezee...

Kuinua daluga
Mkwaju wa penati
Mpira unapelekwa mahali kuku anatagia
Anapiga pasi mkaa
Anaanua mpira
Anaunawa mpira
 
Watanzania... Aliye waloga ni nani?
Kutwa mampira tu... Kujadili mampira tu.... Tunapo elekea tuta zalisha kizazi cha mampira tu kisicho weza kufanya ufumbuzi wa vitu vyenye tija KWa taifa kijamii na kiuchumi.....

Eti,,, ni nani aliye waloga?
 
Mchambuzi alikua mzee Kashasha .
 
YULE ASINGEKUWA NA KILEMA KILE ANGETUSUMBUA SANA, ASANTE MUNGU KWA KUMKANDIKA KOVU LA WAZI WAZI.
 
Reactions: Tui
Kuna hili la "Kukabia juu"[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…