Vita ya Intaneti Tanzania: Faiba vs Ruta za mchongo

Vita ya Intaneti Tanzania: Faiba vs Ruta za mchongo

Ukitembea kwenye mitaa ya makazi Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha au Dodoma, utaona picha inayochanganya kidogo. Kwenye nguzo kama za umeme, kuna nyaya za mtandao zimetandazwa hadi mitaani ambako familia nyingi bado zinategemea bando za kawaida za simu. Wakati huo huo, TTCL wanaomiliki Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wameweka nguvu zao kwenye majengo ya serikali na mitaa ya kitajiri tu.

Kwa upande mwingine, kuna dhoruba mpya ya ruta unlimited ya mchongo ambazo zimeteka soko la nyumba nyingi. Watu wengi wanaamini kuwa ruta hizi za bila waya ndizo hatima ya baadaye ya intaneti ya nyumbani nchini Tanzania.

Lakini ukichunguza kwa umakini, ruta hizi si hatima ni suluhisho la muda tu. Vita halisi ya intaneti ya nyumbani inapigwa chini kwa chini, na mfumo unaowekwa kimyakimya mitaani ndio unaenda kumiliki soko hili lote na bado wengi hawaja jua bado.

Ruta za nyumbani za bila waya zinapata umaarufu kwa sababu ni rahisi kuzinunua na kuzichomeka tu, lakini zina gharama kubwa na changamoto kubwa. Kifurushi cha kawaida cha Mbps 20 kwenye ruta ya bila waya kinagharimu takriban TZS 70,000 kwa mwezi, wakati gharama ya spidi hiyo hiyo na zaidi ya hapo kwenye intaneti halisi ya FAIBA ni takriban TZS 50,000 tu pengine pungufu ya hapo.

Mbali na bei, mawimbi ya bila waya yanabanwa na msongamano pindi watu wengi wanapoingia mtandaoni usiku, pamoja na kuathiriwa na hali ya hewa. Watumiaji wanaonunua ruta hizo wanaanza kugundua haraka kuwa minara ya simu inayotumiwa na watu wengi haiwezi kulingana na utulivu wa faiba inayovutwa kama umeme hadi nyumbani.

Airtel kwa sasa inatawala soko la ruta za bila waya, lakini muundo wa biashara yao una ukuta mgumu mbele yake. Airtel haina mbinu wala miundombinu mikubwa ya kebo za Fiber za majumbani. Minara ya simu haiwezi kuendelea kuongezwa uwezo bila kikomo ili kuhimili matumizi makubwa ya majumbani kama kutazama TV za 4K au kufanya kazi mtandaoni (Hususani content, creation maana kila mtu sasa hivi ni creator). Siku wateja wa ruta za bila waya watakapochoshwa na msongamano na kutaka kuhamia kwenye kebo halisi, Airtel haina faiba wala miundombinu ya kutosha mitaani za kuingiza majumbani mwao.

Kwa upande wa TTCL, wao wanamiliki barabara kuu (mkongo wa taifa), lakini wamepuuzia mitaa ya uswahilini wao wameelekeza nguvu kwenye majengo ya serikali na mitaa ya kitajiri pekee wameacha maeneo makubwa ya mitaa ya kawaida ikiwa wazi kabisa bila huduma ya faiba, na voda pia wanafanya mchezo huu huu tu. Lakini pia mtaani kwangu nguzo za Yas faiba zikisimikwa

Siku familia inagundua kuwa ruta yao ya bila waya ni ghali au ina msongamano, inagundua pia kuwa faiba ya Yas au vodacom tayari inaning'inia kwenye nguzo ya umeme nje ya geti lao. Mchakato uliopaswa kuchukua wiki kadhaa unakuwa kazi ya masaa 24 tu.

Mara tu Yas au vodacom inapotandaza nyaya zake kwenye mtaa fulani, inatengeneza ukuta mgumu wa kuzuia wapinzani kama TTCL au Halotel kuingia. Hakuna kampuni itakayokubali kuingia gharama za kutandaza nyaya zake kwenye mtaa ambao tayari Yaa ina faida ya kuwahi kwanza na gharama nafuu za kuunganisha wateja au tayari inawateja huko.

Mwingine anaye jitahidi hapa ni Savannah ila yupo Dar na Dodoma tu, kwa sasa hivyo bado mpinzani wa kweli kwenye hii sekta ni YAS au VODACOM? HALOTEL je? nasikia naye ana faiba na tofauti na mitandao mingine yeye ana kibali kabisa toka serikalini cha kusambaza mkongo.

Ruta za bila waya ni hatua ya kwanza tu ya kuonjesha Watanzania ladha ya intaneti ya nyumbani. Kadri uelewa wa kidijitali unavyokua na matumizi ya data kuongezeka, watumiaji watadai intaneti ya faiba halisi iliyo ya bei nafuu, ya haraka, na isiyo na kikomo. TTCL inaenda taratibu mno, Airtel, voda na Yas hawana nyaya za kutosha mitaani, na Halotel tayari ipo nje ya geti lako ikisubiri uichomeke tu.

Ni mawazo yangu, na ninakubali kabisa kukosolewa.
TTCL washamba sana, yaani kwenye Fiber wao ndo wangekua ma pioneer nchini hadi uswahilini wangekua na jina ila ndo hivyo kama kawaida ya serikali ya hii nchi kudharau watu wake wa chini ambao ndo mgongo wa uchumi wa hii nchi ulipo, kwani wao ndio wateja wa hao matajiri...
 
Vipi kuhusu vodacom fibre huduma zao zikoje na bei zao zikoje naona wamepitisha waya zao mtaani kwetu
Bei zao zioo kwenye website yao kaka... Hizi hapa chini 👇


Screenshot_20261004-113817_System UI.png
 
Halotel fibre yao ipo mpaka wilaya ya ubungo ndani ndani,malamba,kwembe,kiluvya n.k,nasikia wamepata tenda ya kusambaza fibre hospitals na shule za serikali wilaya ya ubungo,savannah,ttcl,zuku n.k wao wananyang'ananya wateje sehemu za kishua,masaki huko
Kinachowapa advantage Halotel kusambaza FIBER yao upesi hadi vijijini ni kwamba minara yao yote nchini wame connect na fiber (FTTT) yaani wao wakijenga mnara mpya tu wanapeleka fiber kwanza kabla hawajauwasha wala kufanya mengine... So wakiona sehemu pame changamka wanachukua tu link kutoka mnara wao wa karibu waliojenga na kulink fiber ya FTTT, wanatoa nyanya za FTTH na wanapeleka hilo eneo la watu kwa distribution boxes simple tu... naona hata Yas anafata nyayo hizo hizo za Halotel, minara yake ana connect na FTTT kwa sasa..... Unlike TTCL wao kukuletea Fiber ni usubiri walete minguzo kutoka data centers zao mjini huko sijui, wana mambo mengi ya kizamani....
 
TTCL washamba sana, yaani kwenye Fiber wao ndo wangekua ma pioneer nchini hadi uswahilini wangekua na jina ila ndo hivyo kama kawaida ya serikali ya hii nchi kudharau watu wake wa chini ambao ndo mgongo wa uchumi wa hii nchi ulipo, kwani wao ndio wateja wa hao matajiri...
Mkuu nilikuwa nawatukana hawa jamaa ila kwa kasi yao ya kusambaza FIBER sio haba, jamaa wanatembeza nguzo na cable balaa.
 
Wenye kasi ya kutandaza nguzo hadi vijijini ni Yas akifuatiwa na Viettel ndizo nilizoziona kwa Kuzunguka kwangu kdg Tanzania
Mpaka Mwezi June 2027 Router za Airtel zinaenda stoo kula vumbiz
Mi nimewachoka savana kwa nilipo bado hawajafunga ila wakifunga tu hivyo vikorokoro vyao nitavipiga kiberiti mashetani hao
 
Mimi cha Airtel nimekiweka store tayari, TTCL inaupiga mwingi sana, wana speed nzuri. Ila sijaondoa mfumo wao mzima sababu yamkini siku TTCL wakazingua nkawachukua Airtel.
Ipo siku tusiyo ijua utakuja na malalamiko hapa labda wawe wameji rekebisha kwa sasa..
 
Ipo siku tusiyo ijua utakuja na malalamiko hapa labda wawe wameji rekebisha kwa sasa..
Ha ha ha inawezekana mkuu. Ila binafsi ile siku niliyolipia tu, haraka haraka wakaja wakafunga. Sema siku hiyo hiyo internet ilikuwa inazingua kimtindo, baada ya hapo mambo yakakaa fresh hadi leo.

Kabla mimi sijafunga kwa jirani yangu net yao ilishawahi kukwama kwa siku takribani 4 mfululizo, kama sio 4 ni 5 zile. Kilichonifanya nifunge hawa TTCL ni kwamba TV haisomi 5G ya Airtel, so upande wa kustream siinjoy sana ila kwa sasa kwa TTCL nainjoy sana.
 
Ha ha ha inawezekana mkuu. Ila binafsi ile siku niliyolipia tu, haraka haraka wakaja wakafunga. Sema siku hiyo hiyo internet ilikuwa inazingua kimtindo, baada ya hapo mambo yakakaa fresh hadi leo.

Kabla mimi sijafunga kwa jirani yangu net yao ilishawahi kukwama kwa siku takribani 4 mfululizo, kama sio 4 ni 5 zile. Kilichonifanya nifunge hawa TTCL ni kwamba TV haisomi 5G ya Airtel, so upande wa kustream siinjoy sana ila kwa sasa kwa TTCL nainjoy sana.
Jambo jema sana mkuu, Ila umesema TV haisomi 5G ya Airtel una maanisha 5GHz WiFi au mtandao mzima wa 5G wa ODU yako ulkua cheche?
 
Back
Top Bottom