Sajo
Platinum Member
- Nov 8, 2010
- 4,540
- 8,256
Maximum 4 devices?? Mbona kama uhuni huo?
Maximum 4 devices?? Mbona kama uhuni huo?
halotel mpeni miaka mitano kutoka mwaka jana 2025,mpaka mwaka 2030 soko la fiber atalitekaKinachowapa advantage Halotel kusambaza FIBER yao upesi hadi vijijini ni kwamba minara yao yote nchini wame connect na fiber (FTTT) yaani wao wakijenga mnara mpya tu wanapeleka fiber kwanza kabla hawajauwasha wala kufanya mengine... So wakiona sehemu pame changamka wanachukua tu FTTH kutoka mnara wao wa karibu waliojenga na kuupelekea fiber wanapeleka hilo eneo kwa distribution boxes kutoka kwenye mnara huo simple tu naona hata Yas anafata nyayo hizo hizo za Halotel, minara yake ana connect na FTTT kwa sasa..... Unlike TTCL wao kukuletea Fiber ni usubiri walete minguzo kutoka data centers zao mjini huko sijui, wana mambo mengi ya kizamani....
Starlink wapo mkuu. Ila bado hawajapewa kibali rasmi.Starlink watakuja linii?
Sababu zao zipii? Si waliambiwa waweke ofisi Tanzania wakakataa je hiyo ndio sababu?Starlink wapo mkuu. Ila bado hawajapewa kibali rasmi.
Watawala wanasababu zao bonafsi za kumnyima starlink license.
Kama harakati zako zinatishia msosi wa uyu j
View attachment 3693193
Jamuhuri janja janja nyingi.Sababu zao zipii? Si waliambiwa waweke ofisi Tanzania wakakataa je hiyo ndio sababu?
sawa na ttcl tuVipi kuhusu vodacom fibre huduma zao zikoje na bei zao zikoje naona wamepitisha waya zao mtaani kwetu
Una bahati, kwa wengine inaweza kuchukua muda mrefu kukufungia. Kama mdau alivyokupa tahadhari, siku ukipata changamoto unaweza kushangazwa. Kubwa zaidi wana staff wachache sana kuweza kutatua changamoto yako kwa wakati. Ila vifurusho vyao na speed ni vizuri.Ha ha ha inawezekana mkuu. Ila binafsi ile siku niliyolipia tu, haraka haraka wakaja wakafunga. Sema siku hiyo hiyo internet ilikuwa inazingua kimtindo, baada ya hapo mambo yakakaa fresh hadi leo.
Kabla mimi sijafunga kwa jirani yangu net yao ilishawahi kukwama kwa siku takribani 4 mfululizo, kama sio 4 ni 5 zile. Kilichonifanya nifunge hawa TTCL ni kwamba TV haisomi 5G ya Airtel, so upande wa kustream siinjoy sana ila kwa sasa kwa TTCL nainjoy sana.
Mkuu TTCL wakishaweka miundombinu yao, kukufungia naona ni haraka. Mimi nina watu kadhaa hapa mtaani, walivyolipia tu, siku hiyo hiyo walikuja kufungiwa. Labda inategemea na maeneo.Una bahati, kwa wengine inaweza kuchukua muda mrefu kukufungia. Kama mdau alivyokupa tahadhari, siku ukipata changamoto unaweza kushangazwa. Kubwa zaidi wana staff wachache sana kuweza kutatua changamoto yako kwa wakati. Ila vifurusho vyao na speed ni vizuri.
Sawa kivipi? Huoni TTCL wanakupa speed x2sawa na ttcl tuView attachment 3693780
kweli niliangalia vibayaSawa kivipi? Huoni TTCL wanakupa speed x2
TTCL wanajikongoja. Kuna hawa wanajiita Savanna, bwana we wanasambaza nyaya kama hawana akili.Ukitembea kwenye mitaa ya makazi Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha au Dodoma, utaona picha inayochanganya kidogo. Kwenye nguzo kama za umeme, kuna nyaya za mtandao zimetandazwa hadi mitaani ambako familia nyingi bado zinategemea bando za kawaida za simu. Wakati huo huo, TTCL wanaomiliki Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wameweka nguvu zao kwenye majengo ya serikali na mitaa ya kitajiri tu.
Kwa upande mwingine, kuna dhoruba mpya ya ruta unlimited ya mchongo ambazo zimeteka soko la nyumba nyingi. Watu wengi wanaamini kuwa ruta hizi za bila waya ndizo hatima ya baadaye ya intaneti ya nyumbani nchini Tanzania.
Lakini ukichunguza kwa umakini, ruta hizi si hatima ni suluhisho la muda tu. Vita halisi ya intaneti ya nyumbani inapigwa chini kwa chini, na mfumo unaowekwa kimyakimya mitaani ndio unaenda kumiliki soko hili lote na bado wengi hawaja jua bado.
Ruta za nyumbani za bila waya zinapata umaarufu kwa sababu ni rahisi kuzinunua na kuzichomeka tu, lakini zina gharama kubwa na changamoto kubwa. Kifurushi cha kawaida cha Mbps 20 kwenye ruta ya bila waya kinagharimu takriban TZS 70,000 kwa mwezi, wakati gharama ya spidi hiyo hiyo na zaidi ya hapo kwenye intaneti halisi ya FAIBA ni takriban TZS 50,000 tu pengine pungufu ya hapo.
Mbali na bei, mawimbi ya bila waya yanabanwa na msongamano pindi watu wengi wanapoingia mtandaoni usiku, pamoja na kuathiriwa na hali ya hewa. Watumiaji wanaonunua ruta hizo wanaanza kugundua haraka kuwa minara ya simu inayotumiwa na watu wengi haiwezi kulingana na utulivu wa faiba inayovutwa kama umeme hadi nyumbani.
Airtel kwa sasa inatawala soko la ruta za bila waya, lakini muundo wa biashara yao una ukuta mgumu mbele yake. Airtel haina mbinu wala miundombinu mikubwa ya kebo za Fiber za majumbani. Minara ya simu haiwezi kuendelea kuongezwa uwezo bila kikomo ili kuhimili matumizi makubwa ya majumbani kama kutazama TV za 4K au kufanya kazi mtandaoni (Hususani content, creation maana kila mtu sasa hivi ni creator). Siku wateja wa ruta za bila waya watakapochoshwa na msongamano na kutaka kuhamia kwenye kebo halisi, Airtel haina faiba wala miundombinu ya kutosha mitaani za kuingiza majumbani mwao.
Kwa upande wa TTCL, wao wanamiliki barabara kuu (mkongo wa taifa), lakini wamepuuzia mitaa ya uswahilini wao wameelekeza nguvu kwenye majengo ya serikali na mitaa ya kitajiri pekee wameacha maeneo makubwa ya mitaa ya kawaida ikiwa wazi kabisa bila huduma ya faiba, na voda pia wanafanya mchezo huu huu tu. Lakini pia mtaani kwangu nguzo za Yas faiba zikisimikwa
Siku familia inagundua kuwa ruta yao ya bila waya ni ghali au ina msongamano, inagundua pia kuwa faiba ya Yas au vodacom tayari inaning'inia kwenye nguzo ya umeme nje ya geti lao. Mchakato uliopaswa kuchukua wiki kadhaa unakuwa kazi ya masaa 24 tu.
Mara tu Yas au vodacom inapotandaza nyaya zake kwenye mtaa fulani, inatengeneza ukuta mgumu wa kuzuia wapinzani kama TTCL au Halotel kuingia. Hakuna kampuni itakayokubali kuingia gharama za kutandaza nyaya zake kwenye mtaa ambao tayari Yaa ina faida ya kuwahi kwanza na gharama nafuu za kuunganisha wateja au tayari inawateja huko.
Mwingine anaye jitahidi hapa ni Savannah ila yupo Dar na Dodoma tu, kwa sasa hivyo bado mpinzani wa kweli kwenye hii sekta ni YAS au VODACOM? HALOTEL je? nasikia naye ana faiba na tofauti na mitandao mingine yeye ana kibali kabisa toka serikalini cha kusambaza mkongo.
Ruta za bila waya ni hatua ya kwanza tu ya kuonjesha Watanzania ladha ya intaneti ya nyumbani. Kadri uelewa wa kidijitali unavyokua na matumizi ya data kuongezeka, watumiaji watadai intaneti ya faiba halisi iliyo ya bei nafuu, ya haraka, na isiyo na kikomo. TTCL inaenda taratibu mno, Airtel, voda na Yas hawana nyaya za kutosha mitaani, na Halotel tayari ipo nje ya geti lako ikisubiri uichomeke tu.
Ni mawazo yangu, na ninakubali kabisa kukosolewa.
Mbona sio unlimited hivi vifurishiSawa kivipi? Huoni TTCL wanakupa speed x2
inapatikanaje hao hallotel hy fibre yao? gharama zikojeHalotel nlikuwa nawachukulia poa, ila wamenikosha na fiber yao,, hapa home hata kelele za kununua kifurushi sizisikii tena, wamenikomboa sana
mimi hao sina ,nilikua na zuku, nikashawishiwa nihamie savannah ,sasa niko na savannah ,huu uzi nakutana na kitu kipya ,nabaki hoiMi hata sielewi,, hapa naona voda yupo chini halotel juu airtel nje.
Hata mimi nimejifunza jambo, naona kama niunge ttcl hivi.mimi hao sina ,nilikua na zuku, nikashawishiwa nihamie savannah ,sasa niko na savannah ,huu uzi nakutana na kitu kipya ,nabaki hoi
Hao Savanna kinondoni wana credit nzuri sana, watu wanaisifu service yao kuwa stable. Mimi kwa sasa TTCL naiona inaupiga mwingi pia.TTCL wanajikongoja. Kuna hawa wanajiita Savanna, bwana we wanasambaza nyaya kama hawana akili.
Shida ni kwamba wakati fiber wanaanza sambaza nyaya walikuwa wamelenga maeneo ya biashara na ya kishua ila kwa sasa internet ni kama king'amuzi hata nyumba za kupanga uswazi watu wanachanga